Dhana yenye kupoteza wengi

mjarrab

Senior Member
Nov 13, 2015
108
55
DHANA YENYE KUPOTEZA WENGI. 3 in 1

********

Kwa kuwa tunaishi kwa kuamini mambo kwa njia tofauti baina ya Wakristo na waislam! kunapelekea upande mmoja kuto uelewa upande wa pili na kuweza kutambua kwa hakika kuwa hao wa upande wa pili wanaamini nini hasa!.

Hali hii huchangiwa sana na maumbile tuliyo nayo!

Kitu chochote unacho kiona kwa macho uwe ulikwisha wahi kukiona kabla au hukuwahi kukiona kabla, picha ya kitu hicho huhifadhika automatically ndani ya akili!.

Mfano:Ikiwa katika maisha yako hukuwahi kuona au kusikia kitu kinacho itwa madini ya Almasi,Laki umewahi kuona vipande vya chupa kabla,picha itakayo kujia ndani ya akili yako ni kuwa hiki ni kipande cha chupa!,Dhana yako haikuja bila sababu,imeletwa kutokana na picha zilizo hifadhiwa katika akili yako pindi ulipo wahi kuona vipande vya chupa kabla.

Kwa kuwa huna picha nyingine ya mfano zaidi ya chupa! akili itatafsiri kuwa hicho ni kipande cha chupa!

hayo ndiyo Maumbile!.

Lakini akitokea Mtu anae jua kuwa hiyo siyo chupa ni Almasi atakufahamisha kuwa Almasi ni nini na thamani yake ni ipi.

Baada ya kujuzwa Itakuwa picha mpya na fikra mpya zitaingia na huhifadhika katika akili yako.

Kwa hiyo utakapo kutana na Almasi kwa mara nyingine itakuja tafsiri mpya kuwa hiyo ni Almasi na si chupa kwa kuwa akili imepambanua kwa kule kuwa na picha zote!

Sasa tunapo kuja katika swala la kiimani,wakristo wengi hubeba sifa ya kukosa picha halisi katika kuelewa na kuutafsiri Uislamu!

wao huyatafsiri yale wanayo yaona kwa Macho kwa picha zilizo kinyume na Uhalisia,na kwa sababu ya sifa yauoni huo hutafsiri kinyume na Uhalisia Husika!.

Wakristo huitafsiri imani ya Kiislamu kuwa ni Imani ya Kimwili na Wala si imani ya Kiroho!.

Na wao huiona Imani yao(Ya kikristo)kuwa ni Imani ya Kiroho na si kimwili!.

Mtazamo wa Kikristo juu ya Uislam upo mbali na Uhalisia ni Kama kufananisha chupa na almasi!

Ukimuuliza mkristo ni kwanini anasema uislam ni dini ya mwili?

Atakujibu; Ibada za Kiislamu zinaonyesha kuwa ni Dini ya Kimwili!

1)Waislam Hawasali mpaka wasafishe miili yao kwa maji!. Wakati Mungu haangalii usafi wa mwili Bali wa roho!.

2).wanakatazana kula baadhi ya vitu wakisema ni Haram.Wakati uchafu haupo katika vitu bali uchafu upo ndani ya roho ya mtu ndiyo unao takiwa uondolewe!.

Na mengine mfano wa haya.

MADAI YA WAKRISTO

***********************

Ukiyaangali madai ya Wakristo yanamaana sana! hasa ukiwa nawe ni mmoja wao!Kwa kuwa uoni wako utakuwa kama wao.

Lakini ukiwa na Uoni wa ziada utakiona kitu wanacho kikosa wakristo!

Utajua kuwa wanacho kituhumu kipo mbali na tuhuma zao!.

Imani ya Kiislamu imejengeka Juu ya Msingi wa Ibada katika maisha yote!.

Maisha yote anayo Ishi duniani ni Ibada!.

Kwa kuwa MTU ni muunganiko wa roho na mwili!

na Mungu alimuumba hivyo kwa kujua kwake na kwa maana na kwa lengo!.

Hivyo Ibada kwa mwanaadamu haiangaliwi roho peke yake! Inaangaliwa Roho na Mwili(Mtu kamili).

MAANA YA IBADA KATIKA MATENDO.

************

Jambo lolote ambolo Mungu kaagiza lifanyike! Linapofanywa huwa ni Ibada!

na Roho ya Ibada ni twaa(Utii).

Na jambo lolote Mungu analo likataza! likifanywa kwa Makusudi ni Uasi!.

Na Utii au Uasi kwa mwanaadamu hufanywa kwa ukamilifu wake wa Muunganiko wa roho na Mwili(Mtu kamili).

Mtu Katika Utii: Mtu ambaye amekatazika na katazo la Mungu, hazini,haibi,hauwi,hasemi uongo n.k. hafanyi hayo akiwa pungufu! anafanya akiwa Mtu kamili Muunganiko wa roho na Mwili!.

Roho ndiyo Injini ya kuupekesha mwili! Mtu anapo izuia nafsi yake kufanya yale ambayo Mungu ameyakataza hujikataza akiwa Mtu Kamili!

Asipo iba itakuwa hakuiba kwa roho yake na Mwili wake (Mtu kamili).

Haiwezekani mwili kuiba bila roho kuamua kuiba!

Wala roho pekee haiwezi kuiba bila Mwili kutenda!.

Vile vile Mtu asipo uwa kwa kutekeleza amri ya Mungu!.

Hakataziki kwa roho yake tu!bali hukatazika akiwa Mtu kamili (Muunganiko wa roho na Mwili!).

Haiwezekani mwili uuwe bila roho kuruhusu!.

wala roho kuua bila mwili kutenda!.

Mtu Katika Uasi: Vile Vile Mtu afanyae Uasi hafanyi akiwa pungufu! hufanya akiwa Mtu kamili(Muunganiko wa roho na mwili).

Mtu akiiba wazo na Maamuzi yanatoka ndani ya nafsi yake na mwili hutekeleza!.

Kwa hivyo Mtu kufanya wema au uovu! hufanya akiwa na sifa ya Mtu kamili(Muunganiko wa roho na mwili).

Kwa hivyo Ibada ya Mtu haitekelezeki na kuleta tija nje ya Maumbile yake ambayo ni Muunganiko wa Roho na mwili.

Kwa hiyo maana ya Mtu(Muunganiko wa roho na mwili) kumuabudu Mungu ni kumuabudu kwa ukamilifu wa maumbile yake(Mtu).

Ni wazi kuwa anaye jinasibu kumuabudu Mungu kwa roho pekee anafanya usanii katika imani!(Unafiki wa kupindukia).

Jambo hilo haliwezekani na linakwenda kinyume na lengo la Maumbile!.

Maandiko yapo wazi yakifundisha Malengo ya uwepo wa Mtu duniani!.

Lakini kwa bahati mbaya ndugu zetu wakristo wameacha Mafundisho ya Mungu yanayo Muongoza Mtu kamili(Muunganiko wa roho na mwili) katika njia iliyo sawa!

Badala yake wamebeba mafundisho ya wanaadamu yasiyo tekelezeka kiuhalisia!.

Quran na Baadhi ya Maandiko katika Bibilia yameeleza wazi kuwa Mungu alimuumba na Kumfanya Mtu kuwa ni Msimamizi katika Ardhi.

Rejea: Bibilia: Mwanzo 1:28-30.

piaQuran 2:30.

Kama sote tunakubaliana kuwa binaadamu amepewa jukumu la kuisimamia na kuitunza Dunia!basi sote yatupasa kukubali kuwa tumepewa Amana ya kuitunza na kuisimamia Dunia kwa uadilifu!.

Na ikiwa tutatekeleza lengo la kuitunza na kuisimamia Dunia kwa uadilifu! bila ya Shaka tutakuwa tumetekeleza agizo la Mungu!.

Na kufanya jambo lolote kwa ajili ya kutekeleza agizo la Mungu ni Ibada, Na hakuna Ibada bila ya twaa(Utii).

Kinyume cha kutekeleza Maagizo ya Mungu ni ukaidi! Na ukaidi mbele ya Mungu ni Uasi!.

Dunia ya kimaada na Mtu kaumbwa kwa mfumo wa kimaada ili aweze kuyaongoza na kuyasimamia mazingira yake!.

Ni wazi kuwa majukumu yake yatatekelezeka kwa kushabihiana na Umbile lake!.

Hivyo hukumu na Sheria zitakazo mzunguka ni lazima ziendane na Umbile lake!.

MANTIKA YA MUNGU KUTAZAMA MOYONI.

***********************

Mungu kutazama katika moyo haimaanishi kuwa Ibada zifanywazo kwa matendo ya mwili hazikubaliki!.

Hekima iliyopo katika jambo hili ni kwamba. Mtu hawezi kuyajua yaliyo moyoni mwa Mtu mwingine mfano: nia,kusudio,wazo,imani na mfano wake!.

Ila kila mtu anao uwezo wa kuyaona Matendo ya Mtu mwingine.

Mfano: Mtu anapotoa sadaka,kuwatembelea wafungwa,wagonjwa,kutoa misaada kwa wajane,Matendo hayo yanaweza kuonekana kwa kila mtu!.

Lakini sababu na nia ya kufanya Matendo hayo inajulikana na Mungu na Mtendaji wa tendo pekee!.

Hivyo hekima ya Mungu katika hilo nikuwahabarisha wanaadamu kuwa wasifanye matendo yao kiunafiki! kwani Mungu anayajua yaliyo vifuani mwao!.

Kwa hiyo tendo lililofanywa kwa nia ya kutekeleza agizo la Mungu,Mungu analikubali kwa kuitazama ile nia ya utekelezaji wa jambo hilo katika matendo ya mwili!.

Mungu analikubali tendo la Mwili lililotendwa kwa nia katika kutii agizo lake!.

Kwa kufanya hivyo mtu atakuwa amefanya Ibada akiwa katika Umbile lake kamili!.

Kwa kuwa roho ya Mtu bila ya Mwili haiwezi kutenda jambo!.

hivyo imani iliyo ndani yake haiwezi kudhihirika pasi na Matendo ya Mwili!.

Mungu kamwe hawezi kukubali Ibada za kisanii zisizo na Mantiki!.

Jiulize!: Ikiwa Mungu haangalii matendo ya Mwili bali huangalia roho kwa maana ya Imani!.

je! nikiamini katika nafsi yangu kuwa Mungu kakataza wizi,uongo,Uzinzi,Uuaji n.k. na nikaamini kuwa kweli vitu hivyo ni vibaya!.Inatosha Mungu kuniandikia thawabu ikiwa nina amini hivyo kwa moyo wangu lakini kwa mwili wangu nayafanya hayo?.

Je! Ikiwa naamini wizi ni mbaya na nikatazo la Mungu,lakini nikaiba kwa lengo la kukidhi Mahitaji yangu ya kimwili nitahesabiwa kuwa ni mwenye dhambi?.

Ikiwa nitahesabiwa kuwa ni mwenye dhambi ni kigezo gani kitatumika kunihukumu wakati roho yangu inaamini wizi ni mbaya? mwili wangu ulipo tenda wizi nilikuwa najua wazi kuwa wizi ni mbaya na nikatazo la Mungu.

Hapo utagundua udhaifu wa Imani za kutengenezwa!

FAHAMU MATENDO YA WAISLAM

**********

Mwislamu anapo chukua udhu(kuosha viungo vyake)kabla ya kutekeleza Ibada ya Sala!.

Hafanyi hivyo kwa ajili ya kuusafisha mwili!

anafanya hivyo kwa sababu kufanya hivyo ni kutekeleza agizo la Mungu!

Na kutekeleza agizo la Mungu ni twaa(Utii).

Na Utii mbele ya Mungu ni Ibada.

Kwa hiyo kwa mkristo kumdhania Mwislam anapo tawadha(kuosha viungo vya mwili) kabla ya kutekeleza Sala kuwa anajisafisha taka za mwili ni kutafsiri jambo nje ya Uhalisia wake!.

Uhalisia ni kwamba Mwislam anafanya tendo hilo mbali kabisa na dhana ya Mkristo!.

Mwislam anafanya jambo hilo kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu iliyo mtaka kufanya hivyo.

Na kutekeleza amri ya Mungu ni twaa(Utii) na twaa kwa Mungu ni Ibada.

Hebu tazama Aya hii utajifunza jambo

************

Quran 5:

6. Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi tayamamuni vumbi lilio safi, na mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.

7. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, na ahadi yake aliyo fungamana nanyi mlipo sema: Tumesikia na tumet'ii. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi sana wa yaliyomo vifuani.

*************************

Aya hii Ipo wazi kabisa kwamba hilo linalo fanywa na waumini wa kiislam si jambo la kubuni wao! bali ni agizo la Mungu kuwataka kufanya hivyo!.

Kwa hiyo wewe Mkristo unatakiwa uelewe kwamba Mwislam anapo Osha viungo vyake kabla ya Sala ana tii agizo la Mungu!.

Na kuoga janaba ni Ibada ya kutii agizo la Mungu kwa aliyekuwa katika hali hiyo!.

Pia Aya inaweka wazi kuwa agizo hili la Mungu halina Mafungamano na kuondoa taka mwili! kwani Mungu amesema "Ikiwa hamkupata Maji basi Mtayammamu(Mjipanguse)kwa vumbi safi!".

Kwa hiyo kutumika kwa Vumbi katika jambo hili kunaonyesha wazi kuwa hapazungumziwi usafi wa taka mwili! bali unao angaliwa ni Utii kwa agizo la Mungu!.

Na anae tekeleza agizo hilo kwa nia ya kutekeleza agizo la Mungu anapata thawabu.

Na thawabu kutoka kwa Mungu ni Utakaso kwa wanaadamu.

Aya ya 7 inazungumzia ahadi ya Utii kwa Mungu ambayo wanaadamu wote wali chukua!

hivyo Mungu anacho kitaka kwa wanaadamu ni Utii katika yale aliyo yaagiza!

pia Aya hiyo imemalizia kwa kusema kuwa Mwenyezi Mungu anayajua yaliyo vifuani!.

Akimaanisha kuwa chochote mnacho kifanya katika kutekeleza agizo lake anaangalia nia ya kufanya kwenu.

Na kwamba yeyote anae fanya hayo kwa Unafiki Mungu anamjua!.

Uislam ni mfumo kamili wa Maisha ya Mwanaadamu!

chochote anacho fanya Mwislam katika kutekeleza Maagizo ya Mungu ni Ibada!.

UTII USIO NA NIA YA MUNGU HAUZINGATIWI.

****************

Kuna watu wanafanya au kutofanya mambo kwa kuogopa Mamlaka za kibinaadamu, au tafiti za kisayansi lakini wako mbali na Imani juu ya Mungu.

Mfano: Mwizi anaweza kuogopa mkono wa dola na wananchi wenye hasira Kali katika kutekeleza Uhalifu wake!.

Ni wazi kuwa Mtu wa aina hii anautii wa kinafiki ! Wakati wowote akipata fursa ya kutekeleza Uhalifu wake atatekeleza kwa kuwa moyo wake upo mbali na Mungu!.

Pia kuna watu wanatoa misaada mbali mbali na hata kujenga nyumba za Ibada,Lakini nia zao ziko mbali na Utii kwa Mungu,

Wengine hutafuta Uongozi,Umaarufu na mfano wa hayo! wanafanya hayo kujionyesha kwa watu ili kutimiza malengo yao!.

Pia kuna watu wanachukua majukumu ya kuzuia Majanga ya kibinaadamu, mfano kupambana na Magonjwa! kuzuia Uharibifu wa Mazingira ,

Wanazuia Magonjwa si kwa sababu ya kutii Maagizo ya Mungu! bali wanazuia Magonjwa ili kijikinga wao na kupata Magonjwa!

Wengine hupata maslahi ya kidunia kwa kufanya kazi hiyo!.

Wengine hufanya tafiti za kitiba si kwa ajili ya Mungu bali kwa ajili ya kunufaika na jambo hilo!.

Wengine hutengeneza Madawa na kutibu si kwa ajili ya Mungu! bali kwa ajili ya kupata Manufaa ya kidunia!

Vile vile wapo wanao tafiti vyanzo vya Majanga ya kimazingira! ambao hawafanyi kwa ajili ya kwamba Mungu kaagiza!,wanafanya hivyo kwa kuyaogopa Matokeo,na pia kupata Maslahi ya kidunia,

Wapo wanao tunza Uhifadhi wa misitu na wanyama na Vyanzo vya Maji kwa hofu ya kukosa Maji, na kupata maslahi ya rasilimali misitu na kuingiza fedha za kigeni kupitia Utalii!.

hawafanyi hayo kwa sababu Mungu kasema waitunze Dunia!.

Sasa wote wafanyayo hayo wanaonekana kwa Macho ya watu kuwa wanafanya jambo zuri!,Lakini mbele ya jicho la Mungu hawazingatiwi!

kwa kuwa wanafanya mambo kinyume cha lengo la kuumbwa kwao ambao ni Utii mbele ya Mungu na Utii mbele ya Mungu ni Ibada! Na ndilo lengo kuu!.

SHERIA ZA MUDA MFUPI.

Wapo watu wengi hasa upande wa Wakristo!,ambao wanazipinga Sheria za Muda mfupi ambazo Mungu aliwawekea watu ziwasaidie katika maisha yao ya dunia.

Zipo hukumu za Mungu zinazo hukumu maisha haya ya dunia na Ipo hukumu kuu itakayo tolewa na Mungu siku ya Mwisho kwa kila mtu.

Hukumu alizo zitoa Mungu zinazo tawala dunia hazina Maana nyingine zaidi ya kutuwekea kile ambacho kila mwanaadamu anakihitajia katika ufanisi wa Maisha ya kidunia!.

Kwa bahati mbaya wanaadamu walipo ikataa Sheria ya Mungu na kujitungia Imani zisizo leta tija!,wakajilazimisha kujitungia Sheria zao wenyewe ambazo si Muongozo wa Mungu.

Mungu alipo tuwekea Sheria alijua wazi mahitaji yetu! Na hekima yote Ipo kwake.

Lakini wanaadamu wengi hasa wakristo hawataki Sheria ya Mungu imhukumu Mtu Katika maisha haya ya Dunia.

HOJA ZISIZO NA MANTIKI.

****************************

Wakristo wanadai kuwa Mungu aliziondoa hukumu kwa sababu ya Unafiki wa Wayahudi!.

Ya kwamba Wayahudi walikuwa wanazipindua Sheria za Mungu kwa maslahi yao!.

hivyo hakukua na Maana ya uwepo wa Sheria ya Mungu!.

Ukweli ni kwamba Sheria ya Mungu haibatiliki kwa matendo ya wanafiki wa kibinaadamu!,Yanayo batilika ni matendo ya kinafiki ya wanaadamu.

Badala ya wakristo kupambana na Unafiki wa Wayahudi na kuifunua Nuru ya Mungu iliyo funikwa!.

wao wameamua kuizika nuru ya Mungu na kuusafishia njia unafiki uendelee!.

Kila mkristo bila ya kuweka itikadi ajiulize swali hili:

Kilicho kuwa ni Kibaya wakati wa Torati ni Sheria na hukumu za Mungu!

Au ni Unafiki wa Wayahudi walio zipindua Sheria na hukumu za Mungu?.

Ikiwa wewe Mkristo Unaamini kuwa Sheria za Mungu na hukumu zake zilizo waongoza watu katika maisha haya ya dunia zilikuwa ni za haki na kwamba zilitoka kwa Mungu!,basi ni kwa nini unapigia debe Sheria unazo ziamini kuwa zilikuwa ni Muongozo sahihi ziondoke?

Na Ikiwa Unaamini kuwa Unafiki wa watu ndiyo uliokuwa mmbaya ,kwanini usipambane na Unafiki ili Sheria na hukumu za Mungu ambazo Unaamini zilikuwa nzuri ziendelee kuongoza watu?.

SHERIA ZOTE ZINAWEZA KUINGILIWA NA UNAFIKI.

***************************

Leo hii Sheria na hukumu walizo jitungia watu zimeendelea kukumbwa na Unafafiki wa watu!.

Kwa sababu wakiukaji wa Sheria wapo na wapinduaji wa Sheria wapo tena ni wale wale waliopewa Majukumu ya kuisimamia Sheria .

Kwa hiyo tatizo walilo likimbia kwa Sheria ya Mungu wanalikuta bado lipo pale pale katika Sheria walizo jitungia wenyewe!.

Hapo Utagundua kuwa Tatizo si Sheria!,Tatizo ni Unafiki wa watekelezaji wa Sheria!.

Mfano wa Wakristo ni sawa na Mtu aliye ikataa gari nzuri katika barabara mbovu! Kwa kudhani kuwa tatizo ni gari!

hivyo wakakimbilia gari bovu katika barabara mbovu na Matatizo yakawa ni Makubwa zaidi.

Mwenye akili ni Yule anae pigania barabara nzuri ili gari yake nzuri itembee vizuri.

Yule aliye kimbilia gari bovu atapata matatizo zaidi!

kwani hata akipata barabara nzuri bado gari litamsumbua!.

MANTIKI YA SHERIA NA HUKUMU ZA MUNGU KATIKA MAISHA YA DUNIA.

*********************

Hukumu za Mungu katika Maisha haya ya dunia hazimaanishi kuwa hakuna hukumu kuu siku ya Mwisho!.

Mungu anapotoa hukumu ya mzinifu haimaanishi Mzinifu huyo hatohukumiwa siku ya Mwisho!.

Ipo hekima ya Mungu katika kutoa hukumu hiyo!

Mfano: Siyo kila mtu ana imani juu ya Uwepo wa Mungu na uwepo wa siku ya mwisho,

Sasa chukulia kwamba mtu asiye na Imani hiyo akiwa ni mwizi,Mzinifu,muuaji n.k, pindi akutapo mahali hapana Sheria ya kushurutisha asifanye, ni kipi kitamzuia asitende Uhalifu wake!?.

Kama ni mwizi ataiba!,Kama ni mzinifu atazini, Kama ni Muuaji atauwa!.

Kwa hiyo Sheria na hukumu zinakuja kumzuia muhalifu huyu asiibe,asizini,asiuwe n.k.

Hukumu hizi haziji kumfanya muhalifu amwamini Mungu! bali zinamzuia asifanye Uhalifu kwa wengine!.

Uhalifu wake juu ya Imani yake utahukumiwa siku ya mwisho katika hukumu kuu.

Aliye Ibiwa ni mtu,Aliye ziniwa ni Mtu,aliye Uwawa ni Mtu.

hivyo Muhalifu anafanya uhalifu kwa watu wote hata kwa walio wema!.

Sasa hekima ni kwamba Sheria na hukumu duniani hazina budi kuwepo ili kuwakinga wale wasio na Imani ya Mungu wasiwadhuru wale wenye Imani!

Lau dunia hii isingekuwa na hukumu za kuwahukumu wahalifu asinge salia mwenye Imani katika mgongo wa dunia.

Kwa hiyo Sheria na hukumu zinazo ongoza maisha ya Dunia ni kinga dhidi ya Uhalifu wa aina yoyote!.

hivyo kwa wenye Imani hupata fursa ya kutekeleza Ibada kwa njia salama na ndiyo hekima ya Mungu ilipo!

ambayo kwa bahati mbaya hekima hiyo inaonekana ni upuuzi kwa wakristo!

Inaweza kuja hoja kwamba mbona Sheria za kibinaadamu zinaweza kutenda jambo hilo?

Ni kweli lakini Sheria za kibinaadamu hazikidhi lengo la Maumbile!,

Hazipo kwa ajili ya twaa (Utii) kwa Mungu ambalo ndilo lengo la Maisha.

Zipo kwa ajili ya maslahi ya kidunia!.

Ili Mtu awe kwenye lengo yampasa kufuata kile ambacho Mungu ameagiza kifanyike na Sheria na hukumu za Mungu ni agizo lake!

hivyo kutekeleza ni kutii! Na Utii mbele ya Mungu ni Ibada.

Na Ibada ndiyo lengo la Uwepo wa mwanaadamu.

N:B. SOMO HILI LINA JIBU HOJA DHAIFU ZA IMANI ROHONI.

PIA LINAJIBU SABABU ZA MATENDO YA KIMWILI KATIKA IBADA ZA KIISLAMU.

PIA LINAJIBU USAHIHI WA KUISHI KWA MALENGO KUSUDIWA.

UAMUZI NI WAKO KUTETEA WAJIBU NA MALENGO YA UWEPO WETU KWA KUTETEA HAKI NA MUONGOZO WA MUNGU.

AU KUENDELEA KUUSAFISHIA NJIA UNAFIKI.

MAAMUZI NI YAKO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uislamu ni tatizo kubwa duniani kwani ukiangalia nchi karibu zote za kiislamu zina ugaidi na mauaji makubwa ambayo kimsingi yanatokana na mafundisho potofu ya kiislamu.
Dini zote ni za kiroho lakini roho yupi; wa Mungu au shetani.
 
Nimejaribu kuvaa viatu vyako,,,kwanza nilidhani uko neutral lakini nikakuta sivyo,,,nikaona pia ukijaribu kutoa mtazamo uliouona kwa mkristo kumbe nao umeuchukua kwa mtu mmoja au wawili,,,lingine umeisoma biblia hukuielewa ukabakia na mtazamo ambao waislam Wenzio walioisoma biblia bila kuielewa walikuelewesha.

Mimi ninadhani ukitaka stick moja kwa moja kwenye aya za Qur'an ufundishe uislam kwa waislam e.g ndoa,,mirathi,,dhaka nguzo za uislam nk.
Ukiwa kama hivi unavyoeleza utajiletea kitu wazungu wanaita "unnecessary attention" na watu ambao ni mapovu makubwa kama mimi ni rahisi kupasuka.

Pia Angalia usijekuwa wewe si muislamu unajaribu kuwachafua waislam wa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uislamu ni tatizo kubwa duniani kwani ukiangalia nchi karibu zote za kiislamu zina ugaidi na mauaji makubwa ambayo kimsingi yanatokana na mafundisho potofu ya kiislamu.
Dini zote ni za kiroho lakini roho yupi; wa Mungu au shetani.
Kabla ya huo unao uita ugaidi marekani na nato walizivamia Iraq Afghanistan Libya Syria ( kulikuwa hakuna shida) iila hao USA na NATO kwa uwizi wao wa mafuta wakavuruga kila kitu Sasa sijui hao wakristo wenzako USA na NATO hujaona ugaidi wao kumbuka IS ni kundi lao na juzi baada ya kifo Cha yule general wa Iran magaidi ya hao wakristo wenzako wameshangilia kifo chake ujajua kwanini wameshangilia? Muiran ndio Alie wasambaratisha IS sasa USA hakupenda kundi lake lisambaratike ikabidi general auliwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom