Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,422
- 5,676
Utakubaliana na mimi kuwa bwana wa mabwana na mfalme wa wafalme ni muumba mwenyewe wa kila kilichopo na katika yeye kilifanyika kila kitu na pasipo yeye akikufanyika chochote,
hivyo alitengeneza serikali iliyohusisha viumbe kama malaika, na binadamu waliokuwa na sifa ya unyoofu na utii(manabii) kuwaongoza wanadamu(wananchi) hivyo serikali ilisimikwa juu ya mbingu na dunia hata miishilio ya ulimwengu wote,
Ila moja ya sifa kubwa ya viumbe vilivyoumbwa na Mfalme wa wafalme havikunyimwa ufahamu/uhuru wa kuamua/kujua bali ilifanyika hivyo kwa mapenzi yake aliyeviumba ambaye alihitaji utii na sifa za ukweli(toka mioyoni mwao na si kinafiki) yaani za hiyari kutoka kwa viumbe alivyoviumba na kuviongoza pasipo shuruti wala shinikizo kwa maana kwake aliona ni vyema kufanya hivyo na hiyo ndo zawadi ya upendo wake kwao.
Kokote penye utawala hakukokesekani wenye mawazo mbadala au wenye kutamani vyeo na nafasi na vile vile wenye kutafakari nakuoji kwanini iwe hivi na kwanini isiwe vile
Wakatokea wapinzani waliojiunga kuunda serikali yao(waasi(malaika)wakiongozwa na kiongozi wao lucifa) na hivyo kuanza kuhoji uhalali wa kiti kile cha mfalme wa wafalme kukaliwa tu na mtu mmoja na ikaonekana kama wengine hawatendewi haki(mwanzo wa wanaharakati) basi kilichofata chama hiki cha upinzani baada ya kuona kwa njia ya mazungumzo/demokrasia haiwezekani wakapata kutawala ilibidi kiumane na haki ipatikane kwa mtutu.
Tazama vita ikapigwa mbinguni kule kati ya majeshi ya Bwana wa mabwana na yale ya waasi, mwisho upinzani ukasarenda kwa kipigo kitakatifu ila kwa kuwa mwingi wa rehema mtawala akuona ni busara kumwangamiza mpinzani kisa katofautiana nae mawazo/mtizamo kuhusu dhana ya utawala bora bali ili kumwonesha kama wazo lake si sawa alivyodhani ndipo mwishoni hamuhukumu kwa haki akammilikisha sehemu ya utawala wake(serikali ya mseto ikaundwa) duniani kwa kumtoa kabisa mbinguni nakumwamishia kule alikuhitaji sana kupatawala na akaachiwa nguvu zake zote za ushawishi na maovu apate kutawala wana wa ndimi niliye mpaka pale itapoamuliwa na yeye mwenye mamlaka yaani Alfa na Omega kuwa mwisho wa utawala wake.
Wapinzani walipofika duniani walianzisha serikali yao yenye kusaidiwa na tawala mbalimbali za wanadamu wenyewe(serikali za dunia) hili kuweza kuratibu shughuli za serikali hii kirahisi kwa kuwa ndo ilikuwa njia pekee yakuweza kuwaongoza wenye mwili ukizingatia utawala huu ni wa wale wasio na mwili(roho)
Hivyo basi shetani akawa mtawala wa dunia nzima akimiliki kila kitu juu yake na utawala wake ukafika kila mahali hata watawala wa dunia(wanasiasa na wanadini) wakamsujudia na kushiriki uzinzi wa maovu yake.
Akaweka chapa na alama zake kila mahali katika fedha,bidhaa,nembo,taasisi,ishara nakadhalika na pia akajiabudu nakuabudiwa kwa sifa zile zile za bwana wa mabwana hata ikawawia vigumu sana wana wa adamu kumtofautisha njia zake na za yule aketie mahali pa juu zaidi.
Kizazi kile cha nyoka kingi kikapotoka kwa tamaa za utawala, fahari na anasa za utawala wa uasi lakini kwa kuwa utawala huu tokea mwanzo ulikuwa mseto yaani demokrasia iliundwa kwa kuruhusu watawala wawili kuwepo katika himaya moja kila mmoja akiongoza eneo lake japo shetani aliachiwa dunia tu bali yeye aliye mwanzo na mwisho nguvu zake hazina mipaka hivyo ziko kotekote,
japo mfalme wa wafalme asingeweza kuwaachia wapinzani kabisa mamlaka juu ya watu wake pasipo kusaidia inapobidi kwa kuwa tokea mwanzo yeye ajua kuliko yeyote yule aliviumba viumbe vyake vikiwa na ufahamu wa maamuzi ya kuchagua wapi vielekee kati ya pepo au jehanamu japo vipo na vinaishi ndani ya uwepo wake(himaya yake isiyo na mipaka)
Hivyo mpaka ninapotamatisha simulizi hii tawala hizi mbili bado ziko kwenye kipindi cha uchaguzi baada ya kila mmoja kutoa sera zake katika kampeni zao, suala hapa ni juu ya nani ataibuka mshindi katika mtifuano huu ulopewa jina la vita vya kiroho huku kila upande ukimwakikishia mtawaliwa kushinda nakuleta mabadiliko makubwa,
mfano; Upande wa mtawala mkuu wa mbingu na dunia kaahaidi kushinda,kufanya ufufuo nakutunuku uzima wa milele,nchi mpya,utawala utaoongozwa na mwanawe wa pekee pamoja na wale waliomchagua(waliochagua ukweli nakujikana nafsi zao dhidi ya maovu),na pia dhambi wala kifo akitokuwepo kamwe zaidi ya furaha,upendo na amani.
Bali upande wa pili yaani wa lucifa na serikali yake wenyewe ahadi zake ni haki na uhuru wakuishi utakavyo(fanya anasa,ufisadi,kiuka miiko na amri kumi),kuamini utakacho,kupewa mamlaka yeyote,utajiri wa dunia, hakuna cha moto kwa watendao maovu, ukimtii atakupa chochote kile ukitakacho katika himaya ya utawala wake nakadhalika.
Tamati, kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa kiroho ni kirefu zaidi kwa wanadamu na kifupi sana kwa watawala, hivyo tusikazanie tu kuchagua katika utawala wa dunia nakusahau kuwa bado tunao wajibu wakuchagua katika utawala wa kiroho ambao mwisho wa kupiga kura hatuujui bora na huu wakidunia unaojua mwisho ni leo na tiyari tume...."