comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,950
Waziri mwenye dhamana ya Viwanda na biashara Mh Charles Mwijage amekua akileta utani na matamko yenye komedi linapokuja suala la ukweli wa mafanikio ya viwanda vikubwa vitakavyoingizia serikali mapato, Mwijage amekua akiorodhesha maelfu ya viwanda ambavyo sio uhalisia wa dhana ya serikali ya viwanda, amebaki kutaja msururu wa viwanda vidogo vidogo ambavyo kimsingi havina mahusiano ya moja kwa moja na kuinua uchumi nchini sana sana ni watu binafsi mfano wanaogonga kokoto, watengeneza vibatari nk kama ni moja ya viwanda, hivyo amebaki kuleta utani bungeni na majibu ya kuchekesha afahamu kuwa agizo la Rais ni amri kwake hivyo utani wake ni kumtania Mh Rais mwenye dhana ya ukweli na amemaanisha kweli kweli hivyo ninaweza kusema haitendei haki kauli ya Mh Rais, hata
Waheshimiwa wabunge wameshindwa kumuelewa anasimamia wapi hiyo dhana ya viwanda, linapokuja suala la idadi ya viwanda vilivyoanzishwa na serikali, Aidha Mh Mwijage ameshindwa kuelewa nini maana ya neno viwanda vyenye tija ya moja kwa moja na serikali amebaki kuchekesha tu miaka inakatika, akumbuke yeye ndio anayebeba kauli mbiu ya serikali ya viwanda kwa maana ya kuandaa mazingira mazuri ya wawekezaji viwanda, na wala sio kupiga debe kama anavyoita huo ni utani kabisa ninamshauri akutane na watu wa vitega uchumi waondoe mikwamo ya uwekezaji, aweke mazingira wekezi, kuondoa utitiri wakodi pingamizi kwa mazingira ya uwekezi viwanda nchini ambayo ndio sumu ya kukwamisha viwanda, vilevile jinsi ya kupata malighali za viwanda, soko na fursa za uwekezaji,amebaki kuhesabu viwanda visivyo na tija na serikali, ni bora akaishauri serikali ikatumia nguvu moja tu kufufua kiwanda kimoja cha matairi ya magari ambacho kitakua na tija kubwa na serikali kuliko kupigia hesabu viwanda vya watu binafsi bila hivyo ndoto hizo hazitafanikiwa kwa uharaka huo, viwanda ni dhana nzito inayopsawa kufanyiwa maandalizi rafiki ya muda mrefu ikiwemo kipaumbele, malighafi, maeneo wekeze na soko, tukirejea mapinduzi ya viwanda ya nchi za ulaya ilichukua miaka mingi sana kwanza walianza na mapinduzi ya kilimo kwa kuandaa malighafi halafu wakaja na mapinduzi ya viwanda ndipo wakafanikiwa.