Dhana ya msukule kukatwa ulimi

Dhana ya msukule kukatwa ulimi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,456
Reaction score
872,092
Ulimi ni kiungo kimojawapo kwenye milango nane ya fahamu... (inayojulikana na wengi ni mitano) ni kiungo kidogo sana lakini chenye hatari kubwa kama kikitumiwa vibaya lakini chenye manufaa mengi kama kikitumiwa vizuri.

Msukule ni mwanadamu anayechukuliwa kimazingara ili akatumikishwe kichawi huku ikionekana kama kafa.Msukule hua anaona na kujua kila kitu kinachoendelea hivyo kuepuka asije akaropoka baada ya kufanyiwa madawa mengine yote cha mwisho huwa ni kukatwa ulimi.

Ulimi ndio huumba matamshi kiambishi cha matamshi ni matamko...tunapoandika chochote ulimi huongea nafsini mwetu...tofauti ni kwamba hatutoi sauti.

Ulimi umewaponza wengi kwenye maisha yetu! kuna watu wako huko magerezani kwasababu tu ya ulimi!matamshi! Ulimi umechonganisha, ulimi umeharibu mahusiano mengi, ulimi umeleta mifarakano mingi kwenye jamii kwakuwa tu ulitumika vibaya.

Tumeaswa hata katika vitabu vya dini kuwa makini sana na kiungo hiki ulimi.Matamshi yetu yatokayo midomoni mwetu yanataji tafakuri kubwa kabla ya kuyatoa hadharani kwakuwa neno likishatoka limetoka ni sawa na risasi huwezi kuizuia irudi ilipokuwa.

Ni rai yangu kwa viongozi wetu(bila kujali habari za uchaguzi na kila kilichotokea)kuwa makini mno na matamshi yao!wana dhima kubwa sana kwenye ustawi na usalama wa nchi.

Matamshi yao yana impact kubwa sana(mkubwa akisema ni sheria)maneno yasemwayo kama hayajasemwa kwa uangalifu hekima na tafakuri yanaweza kuleta mtafaruku mkubwa sana kwenye nchi.

Chungeni ndimi zenu Chungeni kauli zenu nyie ni viongozi mnategemewa na wengi.

Tuhamasishe uzazi wa mpango! Elimu yaweza kuwa bure sawa lakini kuna huduma nyingine nyingi zinazohusika kabla ya elimu.

Kuhamasisha watu wazaane ni kukinzana na mipango rasmi ya maendeleo tuliyojiwekea.

Tunahitaji familia bora si bora familia kiafya kiulinzi kielimu na hata maadili na ustawi.
 
Naomba kujua milango ya fahamu mitatu tofauti na ile mitano inayojulikana mkuu
 
Samahani mkuu mshana jr naweza kuwa nje ya mada lakini naomba kujua kama misukule wa kike wanaweza kuzaa watoto?
Kama wanazaa,Je hao watoto wanaweza kuwa kama binadamu wengine tofauti na hao wazazi wao? au wanawapeleka wapi?
Je misukule inaweza kurudishwa tena ikawa kama binadamu wa kawaida?
 
Msukule kabla ya kukatwa ulimi huweza kurudi katika hali ya kawaida kinyume chake ni ngumu
Kuhusu uzazi jibu ni hapana lakini nitalitafiti zaidi hili
 
Sijaelewa msukule ni nani? Mchawi ni nani? Anayetakiwa kuchunga ulimi (haujakatwa) ni nani? Confused.
 
Ni nani hasa huwa anatumia misukule? Mchawi au mganga?
 
Kuna What's-up clip nililetewa inasema: Ulimi ni kiungo ambacho hakina mfupa lakini ni hatari sana, ukitaka kujua hatari ya ulimi, umewekewa walinzi 32 wanaokizunguka kiungo hicho. Ulimi ni gate la moyo wako na dunia, yaliyo moyoni kama ulimi hautayatoa utaingia kaburini hakuna anaeyajua.
 
Tuna matatizo mengi, ila la kwanza kujenge uwanja wa ndege chatu.....
 
Kuna What's-up clip nililetewa inasema: Ulimi ni kiungo ambacho hakina mfupa lakini ni hatari sana, ukitaka kujua hatari ya ulimi, umewekewa walinzi 32 wanaokizunguka kiungo hicho. Ulimi ni gate la moyo wako na dunia, yaliyo moyoni kama ulimi hautayatoa utaingia kaburini hakuna anaeyajua.
Nimeipenda hiyo sentence ya mwisho
 
Back
Top Bottom