Dhana ya mafanikio kiroho na kimwili

Dhana ya mafanikio kiroho na kimwili

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
4,042
Reaction score
16,872
Kila kitu lazima utumie nguvu kukipata,siyo uganga,nguvu ya mchungaji au Nani bali ni wewe kuandaa mipango sahihi ya kupata vitu unayotaka walau Kwa asilimia 50 ya malengo yako.

Hata wale unaowaona au kuwasikia kuwa waliirithi mali kutoka kwa Baba na babu zao,bado wanapambana kuhakikisha hawashuki,tena hawa ndiyo wenye msongo wa Mawazo Kwa wanaumia kuhakikisha wanabaki na profile yao.

Pesa za kamari hazitakupa utajiri.

Pesa za uchawa hazitakupa utajiri badala yako zitashusha heshima na thamani yako.

Hakuna mganga wa kienyeji atakufanya ufanikiwe badala yake anakupa Imani ya kupambana,ni kama tu upo na mshikaji wako then anakushauri kuwa fighter.

Fanya mambo haya sita tu utafikia malengo

1.Punguza WIVU.

Kumnunia mtu aliyekuzidi ni kujipa ugonjwa na vitu visivyozungumzika.we pambana kivyako.

2.Jipe muda wa kujifunza.

Kujifunza vitu vipya na kujiuliza Kwa watu ni njia bora pia,si rahisi mtu kukwambia njia zake lakini ni wazi kuna vitu utakopi kutoka Kwa watu tofauti.

3.Jipongeze.

Hapa watu tunapatafsiri vibaya Kwa kudhani kwamba lazima uteketeze pesa , hapana.

Nunua vitu unavyovipenda,
Tembelea sehemu unazozipenda,
Kula na kunywa unavyotaka.

4.Samehe unapokosewa

Changamoto ni nyingi na binadamu hatufanani vitu vingi kuanzia misimamo,maamuzi na itikadi zetu hivyo unapokosewa kosa ambalo ni la kijinga samehe itakuongezea nafasi ya ushindi kiroho.

5.Mwache aende.

Watu wengi wameshuka kiuchumi, kwasababu ya kumbembeleza na kung'ang'ania,watu ambao kimsingi hawapo nao mwisho wa siku wakapoteza vitu.

6.Soma vitabu

Quran,biblia na vingine vitakupa uadilifu,vitakuongezea maarifa,vitakupa hofu na kukutengenezea usawa kwenye jamii.

Bonus.

ACHA PUNYETO

Ukifanya kila kitu Kwa kiasi ni dhahiri utaishi kwenye good life.

Chukua yanayokufaa.
 
Once you understand the power of your words, you won't just say anything.
Once you understand the power of your thoughts, you won't just think anything.
Once you understand the power of your presence, you won't just be anywhere.

"Know your Value"
 
Life is unpredictable journey , Good people die young while bad people live longer .

So I agree with you
 
Back
Top Bottom