Dhana ya kuombewa

Watu wanatishwa kila siku, watu hawaruhusiwi kukosoa, watu hawaruhusiwi kumchallange, watu wanakosa haki zao, wanafunzi wamefukuzwa km mbwa na wazazi wao wakalia machozi, wengne wamebomolewa nyumba zao, mama ntilie wanavunjiwa vyombo vyao na kumwagiwa vyakula. Hao wote wanalia machozi. Hakika machozi yao hayatakuwa bure.

Alafu unakuja kuwaambia hao hao wakuombee? Mungu anaona na anasikia kilio chao. Labda tumuombee hiki kilio kisije kikageuka laana kwake.
 
Tafsiri ya mkuu sio hii...tafsiri yake ni kwamba anapambana na mfumo wenye nguvu kubwa hivyo tumuombee apate nguvu zaidi za mapambano pia tumuombee ulinzi kwakuwa anaziba na kuua mirija ya upigaji
Lakini je ni kweli hiki ndio anachokifanya kwa asilimia mia moja? Mbona kuna ishu nyingine very sensitive zimefunikwa chini ya kapeti? Naona makengeza kila pahala kuanzia huko kwenye kuombewa mpaka kwenye utendaji na hata maamuzi. ..naona rangi nyingi kama za kinyonga kwamba anabadilika kulingana na rangi ya mazingira aliyopo, ni ngumu na kwa hakika kuijua rangi halisi ya kinyonga..kwenye uongozi hili ni jambo baya sana....
 
Ktk viumbe aliowaumba Mungu ni binadamu pekee ndiye aliyempa utashi zaidi..
Lakn kwa bahati mbaya Sana binadamu huyohuyo ndiye kiumbe hatar zaidi na ndiye anajitengenezea uadui zaidi kwa Mungu..

Hata Jesus pamoja na kuwatendea mema na kuwafufua wafu, kuwaponya viwete, vipofu wenye pepo mbaya bado hawakuutambua wema wake ule wema waliugeuza ukawa ubaya..

Hata walipo mkamata simon peter alipomkata sikio mmoja Wa waliokuja kumkamata Yesu alimponya huyo mtu lakn bado hawakuweza kumtambua Bali hasira na chuki ndio ziliwajaa..

Huyo ndio binadamu
 
Umeongea point moja ya maana sana ivi kweli unamuombea mfalme badala ya kumuombea maskini anayelala bara barani apate tahafifu ya mwenyezi mungu inashangaza
Mtu anayeitwa maskini kwa mujibu Iman unamjua?
 
Usidanganyike Mungu adhihakiwi chochote mtu apandacho ndicho avunacho..Anataka aombewe wakati anapanda visasi,uonevu,uadui,vitisho na ubabe daah ngoja tusubiri mavuno yake
 
Hapa sikosoi dressing code na jinsi shati lilivyokaa vibaya..fulana ya blue na si vest nyeupe...
bali ile dhana nzima ya kuombewa kwamba mgonjwa ndie anamuombea mzima
ubinafsi wa kiwango chake
 
Nchi hii wajinga hawatakaa waishe ..kuna watu hawataelewa ulichoandika mijitu haijionei huruma..Upuuzi huu nimeukataa Kanisani Mchungaji wangu anamkubali sana huyo jamaa sasa ikawa kila Ibada hakosi kulazimisha kumuombea asee Tangu uchaguzi wa Mwaka Jana tena ilitengwa siku maalum ya J5 sikuwahi kwenda...Honestly Watz%kubwa ni watu wapuuzi sana Asante mshana jr kuleta mada fikirishi
 
Itafika hatua tutaelewana tu..
Kwakuwa hatujui tukitakacho lakn pindi tukijua tutakuwa sawa
 
Halafu ni wachafu wazandiki waongo. ..mdomo mmoja unaomba kuombewa mdomo wa pili unatoa vitisho kuwa wewe hujaribiri
Hilo nalo neno... Mungu ameruhusu kujaribiwa kwa zaka...

Sasa mkulu hataki hata kujaribiwa kwa maandamano tuu.... Je ukimjaribu kwa kodi si ndio balaa kabisa.

Naunga mkono hoja ya kumuombea abadilike aliongoze taifa la mungu kwa HEKIMA zikiisha atumie BUSARA na aenende Katika HAKI na kuzishika SHERIA za BWANA na kuheshimu KATIBA tulilojiwekea watu wa MUNGU.

Mungu ibariki Tanzania Mungu mmbadili mkulu ku mwamo.

AMEN
 
Inafika wakati maombi yanageuka laana kama uadilifu hauzingatiwi..!
Hapa dunian ukitaka upendwe na uwe maarufu ww kuwa mnafki na muongo lakn ukiwa mtenda haki watu watakuchukia na kukuzushia kila aina ya ubaya..
Hata kwenye maandiko hayo yapo
Rejea akina petro na akina yohana
 
Mkuu hiyo dozi yako si haba.
 
I sometimes fail how to comment and term you Mr Mshana jr. You are so challenging and analytical on faith matters. You speak openly, if ironically the truth is apparently. You are the one of the great thinkers in jf.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…