Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,826
- 730,248
Ni kiini macho na aina fulani hivi ya utapeli..kwamba eti mchawi ajisalimishe na kukabidhi mikoba yake yenye matunguli ya kila aina, huyo hawezi kuwa na maisha tena! Asipouliwa na wenzake atakufa mwenyewe
Uchawi ni fani inayojitegemea yenye kanuni taratibu na masharti yake tena magumu, ndio maana si wengi wanaweza kuwa wachawi! Uchawi una mahusiano ya moja kwa moja na ulimwengu wa giza na mambo yasiyoonekana ulimwengu wa roho kuna viapo vyake huko! Tunguli na mapembe ni vibebeo tu vya nguvu isiyoonekana ni catalysts, kwahiyo mchawi wa kweli ana uwezo wa kuihamisha nguvu husika na kuacha mitunguli mitupu isiyo na nguvu yoyote kama mikasha tuu
Mchawi wa kweli hawindiki na wale wanaojifanya kutoa wachawi, mkikaribia nyumba yake msipokutana na bahari basi mtakutana na msitu au kiwanja kitupu... ..na huyo anayefanya hiyo kazi ni lazima awe amejizatiti kwa kinga za kila aina na zenye nguvu kubwa sana
Hii ni kwakuwa uchawi una wataalam na madaraja yake . kwahiyo kama daraja langu ni dogo na nikiona kuna mapambano yanakuja haraka sana hutafuta msaada kwa aliye juu yangu au aliyenifundisha kazi...lakini hapo hapo pia naweza kuwa ninamiliki silaha zangu za kinga za maangamizi kwa yeyote yule atakayejaribu kunichezea!
Hawa kina manyaunyau walikuwa ni matapeli na wapigaji tu wakikamata matapeli na wapigaji wenzao wanaojua mazingaombwe na kujifanya ni wachawi ama waganga mahiri wa kienyeji. Kundi lingine la kitapeli ni hili la manabii na mitume wa kileo ambao wamegeuza vitu vyao kama kliniki za washirikina kwa kutumia jina la Yesu Kristo
Tunguli halisi haiungui kwa moto wa kawaida..upo moto wa kichawi ambao ndio unaweza kufanya hiyo kazi au moto wenye nguvu ya kimungu na ni aina ya moto ambao hauunguzi kingine chochote zaidi ya kilichodhamiriwa
Wale wabebao matunguli na kuyapeleka kanisani kuombewa kisha kuchomwa moto wanakuwa tayari(hata kama ni wakweli)hawana nguvu tena na walishafukuzwa kilingeni na kupokonywa nguvu zote.
Ni wachache mno wanaoamua kutoka wenyewe tena kwa kutoroka na kwenda kupata ulinzi wa Kimungu kabla wenzao hawajawastukia kwwakijua
Hizi operations nyingi vijijini za kutoa wachawi ni ujinga tu wa jamii yetu na kutoelimishwa dhana nzima ya uchawi na jinsi unavyofanya kazi
Kanda ya ziwa Kumekuwa na mauaji mengi ya kutisha ya vikongwe wakihisiwa ni wachawi....ujinga mkubwa huu!!! Tuache maskhara mchawi wa kweli hukuona na kukuwahi kabla hujamfikia
Jinsi tunavyozidi kulipuuzia suala zima la uchawi na ushirikina ndio jinsi tunavyozidi kuiumiza jamii
Wenzetu ulaya wanafundisha uchawi kama somo hii imesaidia kuepusha matatizo mengi sana...tusifungwe na nira za kiimani na kuonekana kuzungumzia uchawi na ushirikina ni jambo baya sana..tunapotoka na kukosea sana...kwakuwa hata katika hizo imani zetu zinaukubali na kuukiri uchawi kama nguvu hasi inayofanya kazi duniani juu hufiki popote