Wanajamvi Leo katika pita pita zangu mtandaoni nikakutana na swala ambalo limekuwa likinigusa kwa muda mrefu,ni kuhusu usemi kutoka kwenye kitabu kitukufu unaomuasa mwanaume kuushi na mwanamke (mke wake kwa akili) Kusema ukweli hata mimi nawaza ni kwa nini mungu aliligusia swala hili katika mtazamo huu,Hebu tupeane mawaiza juu ya hili kwamba "uishi naye kwa akili kwamba yeye anaakili nyingi zaidi,au ni kwa kuyaona mapungufu ya mwanamke ndiyo akatoa hadhari hiyo Ili kumuepusha mwanaume kutokana na madhara yanayoweza sababishwa na mapungufu hayo.Kwenu studio🎤🎧