Dhana ya wanawake kupenda Kama wanaume imeharibu sana jamii yetu

Artifact Collector

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
6,539
9,992
Kinachofanya jamii iharibike ni Ile dhana ya Wanawake nao kutaka kuchagua mtu ata Kama Hana nyuma Wala mbele, matokeo yake mwanamke anazaa na wanaume wa ajabu ajabu hawana malengo na kupelekea kuwepo kwa single mother wengi, unavyombebea mimba mwanaume kwa kigezo Cha moyo unampenda ni uzwazwa

mfano Kuna mwanamke amezaa na mwanaume ambaye ana hisia nae a.k.a anampenda, lakin kamtelekeza na mtoto, ukimfuatilia Whitney Houston alimpenda sana bobby brown, lakin hakuna mtu aliyemharibia Whitney Houston maisha yake Kama bobby brown

Moyo hauna adabu, ndo maana tukapewa akili ili zi-control moyo, sio kila mwanaume unayempenda mwanamke ni mzuri mwingine atayavuruga maisha yako kisawasawa. Kwenye maisha sababu inayomfanya mwanaume awe kichwa kwenye familia ni kwasababu ana uwezo mkubwa wa kutumia akili, mwanamke anaongozwa kwa sababu yeye anaongozwa na moyo kwenye mahusiano kuliko akili.

Tukisema tufuatilie kile moyo unachopenda kila mara tunapelekea kuharibu maisha yetu, ndo maana haijalishi ni kitu gani moyo umekipenda akili lazima iwe muamuz wa mwisho, hiki kitu Wanawake wengi hawawezi kinachopenda Moyo kamwe akili zao haziwez kupinga, Ila wanaume wanaweza ndo utofauti uliopo

Mwanamke anatakiwa kumridhia mwanaume na sio kumpenda, kwa sababu yeye ndo anayetongozwa, ni ngumu sana kwake kuwa na choice, na ni Wanawake wachache sana ambao wanajeuri ya kutongoza Kama wanaume, na wanaotongoza wanaume wanatumia nguvu ya fedha, mwanaume hatakama Hana hela uthubutu wa kutongoza anao

Swala la kumpenda mwanaume linakuja through learning. Lakin Leo hii Wanawake wanataka kupenda in first-place Kama wanaume kitu ambacho sio sahii, mwanamke anatakiwa aridhike na mwanamme atakama hajampenda mwanaume, kumpenda kutakuja mbele ya safari.

Mwanaume amepewa uwezo mkubwa sana wa kupigania penzi kuliko mwanamke, na ndo mjenzi wa familia imara na jamii imara, ni ngumu sana kwa mwanaume kukaa na mwanaume ambaye hampendi na hata akizaa nae hiyo familia ataitelekeza ndo kinachotea sahivi.


Dhana ya Wanawake kutaka kupenda Kama wanaume liliivuruga Western countries, na Sasa hivi limehamia uku kwetu na litaendelea kutuvuruga
 
Bandiko lako halina mashiko liko tu ku undermine wanawake na pia kupenda kumeharibuje western countries, wakati kule wanaheshimu utu na haki za wote kuliko huku Africa tulio na ukandamizaji. Pia upendo ni amri kuu na maandiko yanasisitiza kupemdana how come sasa unalaumu upendo
 
Bandiko lako halina mashiko liko tu ku undermine wanawake na pia kupenda kumeharibuje western countries, wakati kule wanaheshimu utu na haki za wote kuliko huku Africa tulio na ukandamizaji. Pia upendo ni amri kuu na maandiko yanasisitiza kupemdana how come sasa unalaumu upendo
Umepataje mda wa kucomment kwenye bandiko lisilo na masiko,
Utu upi na wakati wameachana na concept ya marriage ya asili, wako kwenye ushoga
 
Umepataje mda wa kucomment kwenye bandiko lisilo na masiko,
Utu upi na wakati wameachana na concept ya marriage ya asili, wako kwenye ushoga
Mashoga hata Tanzania wapo na wafiraji ni nyie wanaume, na hapa bongo pia ndoa zinavunjika so Sijaona logic ya bandiko lako Mimi. Ushoga wenyewe upo KABLA ya Yesu so duniani hamna jipya wa Africa tuache kujificha kwenye kichaka Cha kulaumu wazungu
 
Women are prone to emotional manipulations..
Nadhani hii ni sababu tosha ya kuwafanya wanawake wasiwe wachaguzi bali wawe watu wa Ndio nimekukubali au hapana sipo tayari kuwa na wewe....
 
Inashangaza sana karne hii mwanaume mwenye ndevu zake ananyanyuka na kuuaminisha umma kwamba mwanamke hatakiwi kupenda au kwa lugha nyingine mwanaume ndio mwenye haki ya kupenda
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom