matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,600
- 15,399
Waislam wakifunga hata usiyemuislam utafaidi. Sio wachoyo, Sio wabaguzi kwenye futari. Nimewahi kupanga nyumba moja na waislam ikifika mfungo sisi wakristo tulikuwa tunafaidi sana. Kikipikwa chakula cha kufuturu na sisi tumo kwenye bajeti hata kama wanajua hatujafunga.
Wakristo tukifunga, mara nyingi futari inakiwa ya kichoyochoyo. Mtu anajifichaficha. Asiyehusika akisogelea msosi utasikia, huu ni wa waliyefunga au haujui mimi nilikuwa nimefunga.
Ile bajeti ya chakula ambayo atakuwa ameikwepa kwa kufunga badala ya kuitumia kama sadaka kwa kuwezesha wasio na chakula wengi wanachukulia kama savings. Amesevu kwa matumizi yake ya baadae.
Tumesahau
Isaya 58:6
Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
Isaya 58:7
Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?