Dhana na Miongozo ya "Katika Utawala Wangu..."

Guys... Who is legal advisor wa Rais Magufuli? Au advisor wa namna yeyote ile?

kwangu naona hakuna jitihada kuweka mfumo, kanuni Na Sheria Imara zinazoeleweka ili uwajibikaji uwe ni kitu Na tunu ya kawaida si mfumo w utegemezi wa kiongozi mkuu wa nchi au hamasa yake kuongoza Na "kunyoosha" Taifa!

Kuna tofauti ya kufanya mambo "katika utawala wangu" kama mambo hayo hayahusu kanuni, sheria, taratibu, katiba au maamuzi yenye impact kubwa kwa jamii na Serikali.

Ni haki kusema "katika utawala wangu" uvivu,uzembe, ubabaishaji, uchelewaji, umangimeza, uhujumu nu mwiko na kamwe hautavumiliwa. Lakini kuna haja ya kuweka na kurejea misingi iliyopo na kuhoji kwa nini utovu wa nidhamu upo na au unaongezeka!
Mkuu Rev Kishoka.
Asante kulizungumzia hili

Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!.

Tuache Siasa ktk Uchumi: Wachumi tuelimisheni Dhambi ya Fixed Deposit na Faida ya Fedha Kukaa tu BoT

Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! .

Je, wajua amri za Rais sio final and conclusive?. Zinaweza kupigwa chini na mchanga kusafirishwa?

Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'!

Mkuu Mzee Mwanakijiji, Rais Magufuli Sio Alfa na Omega. Rais Sio Mungu! Na Kwenye Utawala ni Katiba!

Paskali
 
Kwa hiyo mtoa post hizi taasisi huru zinajengwa huu ya mawe? Mbona marekani ambayo mnaichukulia kama reference wanastrugle kutafuta raisi makini au mzuri kwa process nyingi? Si wangechagua kichaa tu kwa sababu wana taasisi strong? Tu nataka rais strong ambaye anaconverge mawazo ya debates za watu na kutos msimamo Wa serikali.
Soma uongozi au management ndiyo utajua dhana hii. Soma kitu kinachoitwa bcg matrix katika uongozi kijana inaelekea umekalilishwa tu na akina lisu ambao hawajui management skulls.

Management ni science ndugu yangu na ni proffesion siyo kila mtu anaweza. Mnadannganywa na akina mtatilo vilaza wasioelewa lolote na nyie mdaka kama kasuku.
In a family of strong father the family will excell and viceversa is true. Ndiyo mana mdada anastrugle kutafuta Mme mwenye maamuzi mazuri vinginevyo angeolewa na yeyote au chizi.
 
Mkuu Tetty,uliyoyaandika ni kweli kabisa. Kuna viongozi mpaka wanafikia hatua ya kutamka kabisa kwamba wao wana akili zaidi ya wengine ndio maana wapo kwenye hizo nafasi walizonazo.

Wako wengi sana na ndiyo sabababu haupigi hatua.Na pia UVCCM wanafikiria mtu akiteuliwa kuwa Kiongozi ana akili kuliko wao ndiyo sababu pia hajifikirishi zaidi kuhoji vitu mbalimbali vinavyotokea kwetu.

Mfano mzuri ni madini!Akina Lissu miaka 18 iliyopita walipokuwa wanahoji ni UVCCM wlaiowatukana na kuwakebehi kwamba siyo wazalendo wana wivu wa kike,leo yale ya miaka 18 yanaporudi kwa midomo ya the so called watawala wanakuja na moto akina Lissu wamelipwa na wawekezaji,haiingii akilini kabisa vijana wa CCM kushindwa hat hili kuhoji kwanini TAIFA lilidanganywa,na bado wanakubali waliotuingiza kwenye huo upumbavu wasiguswe,niambie ni kizazi cha aina gani Kiongozi akinga barabarani unapiga makofi,na wapinzani wakisema jamani anachafua mazingira mnawapigia makelele,leo anawatumia wale wale vijana kuzoa UCHAFU uliowekwa na watawala waliotangulia,hawahoji wako busy kutukana wapinzani.

Najiuliza hivi vijana hawa wanaakili timamu?
 
Dah TANZANIA ni mbelee kwa mbeleee!!!.........yaliyopita ni maneno ya wahenga......everymorning wanaanzisha new"katika utawala wangu” kwa upande wangu nahisi hii ndio asili yetu Watanzania na Afrika kwa ujumla.
 
Kwenye tawala za CCM ukiwa unafanya kazi kwa kuzingatia taaluma yako hautadumu kwenye nafasi yako.Ndiyo sababu hatuna uongozi imara na bora,tunabora uongozi na wenye matamko mubashara.Tutamaliza vipindi vyote hakuna cha maana zaidi ya Kamata weka ndani.
Shemeji Tetty ndio maana tunawajibu wa kumsaidia ili aweze.

Usaidizi wetu wengine ni huu huu wa kusema na kuandika humu kiukweli ujumbe unamfika japo huwa haishukuru JF kuwa inamsaidia kubadilika, lakini cha muhimu ni ujumbe unamfikia na anabadilika.

Paskali
 
Ulitaka au kupendelea asemeje labda!? Katika Utawala wa Mbowe!?
MAJIZI mmeshikwa pabaya sana. Mmekosa hoja kutwa kuja na vioja.
 
Tatizo la watawala wetu kufikiria wanaakili na kujua zaidi yetu.Wamelewa Madaraka wanashindwa hata kupumua.Wako ICU lakini hawajui kama wako ICU.

Mkullu hajui kwamba wako Malori tofauti na wateule wake,kuna aliowaacha kwenye TIMUA,KAMATA,FUNGA masaa 48.Bila kujua analiharibu TAIFA Kiuchumi,kisiasa na umoja wetu unagawanyika!

Tukifika 2020 hatuna TAIFA moja tena.Tuna Kibiti,Arusha,Kilimanjaro na Ukanda wa ziwa.

Maendeleo hayaji kwa one ma show ya TV na front page.Maendeleo yanakuja kwa kusikilizana na si kukomoana.

Nina uhakika unalosema likifika kwa marafiki zake utaambiwa wewe si mzalendo.Ngoja tumwachie atakapostuka ameishaanguka na kuvunjika miguu na mikono Muhimbili ipo tutampeleka.Ngoja tumuache kwanza,mwenzetu ana PhD.
 
Sisi tunafata STK- Sheria,Taratibu,na Kanuni

Hii ndio nguzo ya kuongoza nchi dunia nzima,haya mambo ya utawala wangu,utawala wangu,ni mageni kwetu,kwanza anatawala au anaongoza?

Naona hata bungeni wabunge wanasema "wananchi wangu" yaani wametugawana na wanatumiliki

Asituambie utawala wangu,atuambie kwa mujibu wa sheria fulani,kanuni Fulani,taratibu fulani zilizotungwa mwaka fulani,kifungu Fulani

Wasaidizi wake wanapata shida kujua utawala wake unataka nini kwa sababu hajaviweka wazi

Wanaofata sheria wanatumbuliwa,wasiofata wanaachwa,na wengine wanatumbuliwa,

Ili nchi iaminike lazima iwe na mfumo unaotabirika,watu wajue kesho na kesho kutwa nini kitakuwaje,kwa wawekezaji wa mabilioni na matrilioni wanahitaji kujua hata miaka ishirini ijayo
 
Ulitaka au kupendelea asemeje labda!? Katika Utawala wa Mbowe!?
MAJIZI mmeshikwa pabaya sana. Mmekosa hoja kutwa kuja na vioja.
Haya ndiyo majibu ya viongozi wenye akili. Tusitegemee maendeleo kwa vichwa hivi.
 
B
Ngoja tumwachie atakapostuka ameishaanguka na kuvunjika miguu na mikono Muhimbili ipo tutampeleka.Ngoja tumuache kwanza,mwenzetu ana PhD.
Shemeji Tetty hatuwezi kumwacha, !huo utakuwa sio uzalendo wa kweli, Tanzania ni yetu sote na sio mali ya mtu mmoja. Hata kama hapendi kuambiwa ukweli, sisi wakweli toka ndani ya nafsi zetu tutaendelea kumwambia ukweli kwa manufaa yake na manufuaa ya taifa.

Paskali
 
Guys... Who is legal advisor wa Rais Magufuli? Au advisor wa namna yeyote ile?

Hii ziara ya Pwani yametokea matamko ya Rais ya kusema "katika utawala wangu" but kwangu naona hakuna jitihada kuweka mfumo, kanuni Na Sheria Imara zinazoeleweka ili uwajibikaji uwe ni kitu Na tunu ya kawaida si mfumo w utegemezi wa kiongozi mkuu wa nchi au hamasa yake kuongoza Na "kunyoosha" Taifa!

JPM alipokujaa alishangaa kukuta madudu na machafu kupindukia, sababu yawezekana sana kuwa JK naye alisema "katika utawala wangu" akajifanyia mambo Na maamuzi mengi ambayo Magufuli anayashangaa. Labda naye Kikwete alikuta aliyoyarithi ambayo yalifanywa kwa mantiki ya "katika utawala wangu.." iwe ni Serikalini au hata katika Chama.

Leo Magufuli anaongoza nchi Na kufanya kila kitu kwa kigezo cha "katika utawala wangu" Keaho akiondoka Magufuli, atakayekuja naye atasema "katika utawala wangu" na kubadilisha Yale yaliyofanya "katika utawala wangu" wa Magufuli !

Now nikiangalia kwa nini kuna non-responsive kutoka taasisi, mashirika, Serikali, watendaji Na hata wananchi, jibu lake ni kila mtu anajua "katika utawala wangu" utapita Na kuna expiry date Na si mfumo unaoeleweka kisheria... Wanapuuzia wanajua wakisema "ametukuta, ataondoka, atatuacha"!

Nchi imekuwa ikiendeshwa au kuongozwa na maamuzi kufanywa kwa dhana na fikra za "katika utawala wangu.." kuanzia Rais mpaka Mkuu wa Wilaya au hata mwenyekiti wa kijiji kupuuzia kabisa mipaka ya kisheria, mamlaka,kanuni hata katiba.

Zaidi, dhana hii ya "Katika utawala wangu.." si kwamba imekwamisha maendeleo ya jamii na Taifa, lakini hata imepunguza uwajibikaji wa kweli, kujenga kiburi nauungwana wa kukiri makosa, kujikosoa au kujisahihisha kunakosekana.

Mfano inawezekana DC wa Hai juzi akivunjavunja shamba la Mbowe alitumia kigezo hicho cha "katika utawala wangu.." au leo Mkuu wa TRA Arusha anaposema ukikutwa huna risiti fainielfu thelathini, naye anatumia nguvu ya "katika utawala wangu".

Keshoanapokuja mtendaji au kiongozi mwingine naye akasema "katika utawala wangu" (mfano mzuri ni Nape na Mwakyembe wizara ya habari) naye akaamua kusema anabadilisha na kufuta kila kilichofanywa na aliyemtangulia kwa kuwa "katika utawala wangu" haoni manufaa.

Kuna tofauti ya kufanya mambo "katika utawala wangu" kama mambo hayo hayahusu kanuni, sheria, taratibu, katiba au maamuzi yenye impact kubwa kwa jamii na Serikali.

Ni haki kusema "katika utawala wangu" uvivu,uzembe, ubabaishaji, uchelewaji, umangimeza, uhujumu nu mwiko na kamwe hautavumiliwa. Lakini kuna haja ya kuweka na kurejea misingi iliyopo na kuhoji kwa nini utovu wa nidhamu upo na au unaongezeka!

Leo Rais Magufuli kawasema Brela mpaka kutoa tamko (presidential executive order) verbally kuwa wenye nia ya kuanzisha viwanda au biashara wasisubiri Brela, waanze mchakato maana Brela wanajivutavuta na kupunguza kasi ya maendeleo na azma ya viwanda ya awamu ya tano. Najiuliza je kwa nini Brela leo ni miezi 20 tangu awamu ya Tano iingie madarakani bado inajivutavuta na kuwa na umangimeza au ukiritimba ambao unakwamisha ufanisi? je hawana kanuni za uwajibikaji? au usimamizi wa kanuni za uwajibikaji na majukumu zina mapengo na mianya ya uzembe, uhujumu au hata kulea rushwa na kero?

Je yawezekana huko Brela hakuna hizi kanuni kwa kuwa kila mkubwa wa sehemu anafanya mambo ya "katika utawala wangu" na kujiamulia mambo na wafanyakazi wa chini kwa kukosa mfumo unaoeleweka na kushuhudia kwao wakubwa wakifanya mambo kwa itikadi ya "katika utawala wangu" basi wanajijengea kiburi cha "alitukuta, atapita, atatuacha hapahapa"?

May be tukiongelea mambo kwa mtazamo huu, ubishi na ushabiki unaopinga kujengwa kwa mfumo huru Imara kuanzia Katiba, Sheria na Kanuni hata uwajibikaji wake utaangalia mambo kiuhalisia Na si kushangilia current happenings ambazo "baada ya utawala wangu" tutarudi kule kule au atakuja mwingine na mtazamo wake na kusema "katika utawala wangu"?
Rev.Kishoka , heshima kwako mkuu

Hili ambalo umelizungumzia , limeonekana kwa mda sasa katika jamii nyingi za Kiafrika.

Nchi nyingi za bara hili zinatawaliwa kwa utashi wa mtu binafsi aliye kwenye madaraka kwa wakati huo.

Hali hii imewafanya watu kuishi kwa wasiwasi sana maana hawajui kitatokea nini kesho.

Sheria zimebaki kuwa ni maandishi yaliyo kwenye vitabu tu , lakini hazina maana yoyote.

Tabia hii ya kuongoza nchi bila kufuata mifumo na taratibu zilizowekwa ni hatari sana endapo siku moja atakuja kupatikana kiongozi asiye na utu , aliyejaa ukatili na kiburi.

Sheria na taratibu ziliwekwa ili kuwadhibiti viongozi wasio waaminifu na waliokosa ustarabu.
 
umezungumzia Marekani yenye mifumo huru ya mizania ya uongozi: Executive, Legislative na Judicialambazo zote zina checks and balances zenye nguvu kuzuia uimla wa mambo.

Kiongozi kuja na kipaumbele si tatizo, tatizo nikuongoza nchi bila mfumo eleweka na wenye mianya mingi ya uholela.

Turudi kwenye mfano wako wa Marekani: ni wapi umesikia Rais wake akiamua matumizi ya fedha, kubadilisha kodi au hata kuingia vitani bila kuhusisha bunge na kupigiwa kura na bunge? je lini umesikia Rais akiingilia utendaji wa idara za Serikali kisa yeye Rais bila kuleta mtafaruku?

Hayo ya kuanza kubezana kama ni Rev. wa kweli au wa uongo ni udhaifu wa kujenga hoja kujibu hoja August..
Bado hujaelewa Nguvu Za kiongozi wa nchi Kama USA licha ya kuwepo Kwa hizo check and balances, Kwa maslahi ya nchi Raisi anaweza kutumia executive order kuhamisha pesa Na mengineyo.
Halafu hiyo hela anayohamisha anatumia Kwa matumizi binafsi au ya kitaifa?
Yaani sisi tulivyochelewa hujakuona? Na Bado unataka tujicheleweshe Kwa hizi siasa Za kupungua maendeleo au ku waste time Kwa vitu ambavyo ni straight fwd.
 
B
Shemeji Tetty hatuwezi kumwacha, !huo utakuwa sio uzalendo wa kweli, Tanzania ni yetu sote na sio mali ya mtu mmoja. Hata kama hapendi kuambiwa ukweli, sisi wakweli toka ndani ya nafsi zetu tutaendelea kumwambia ukweli kwa manufaa yake na manufuaa ya taifa.

Paskali

Hujamsikia akisema Tanzania ya Magufuli?Kwa miaka hii mitano Tanzania tumeishaumia tukubali maumivu tu.Tukimaliza miaka ya jamaa yako tutaanza kutibu vidonda vya chuki,visasi na ubaguzi.Jiandae tu.Hayo mengine ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu
 
Mataifa mengi ya africa yaliyoanza kupiga hatua yamerudi nyuma mara tu kiongozi aliyijitunuku ushujaa anapokufa au kuachia madaraka. Viongozi wa aina hii huwajaza hofu wananchi na kuwaaminisha wao pekee ndio wana uwezo wa kuongoza. Hawajiulizi wakiondoka wanaawaacha kina nani kuendeleza waliyoaanzisha.

Nakumbuka ziara ya Rais aliepita wa Us alipokuja Africa sina uhakika wapi nafikiri alipohutubia AU Addis Ababa alisema Africa iondoke ktk dhana ya watu kuwa mashujaa na hasa kipindi cha kumtoa mkoloni mashujaa wetu kama Nyerere,Nkwame N.k wengi walipatikana kipindi hicho kwa sasa Africa inahitaji taasisi imara

Itakuwa kila mtawala anakuja na maelekezo yake kutokana na utashi wake na wala hatujishughulishi kuweka mifumo imara ya kitaasisi na hii itasaidia na haitajalisha nani anakalia ofisi kuu anakuta mifumo ya kitaasisi ipo madhubuti
 
Rev. Kishoka, hilo unalosema ni tatizo mtambuka, ni kasoro/kosa/udhaifu uliyo wazi kabisa lakini tumekuwa na tabia ya kuuzunguka mbuyu tu.

Tanzania inalilia na inahitaji sana Katiba Mpya. Sambamba na kuhitaji mabadiliko chanya ya muundo wa Serikali na mabadiliko makubwa ya mfumo wa utendaji wa serikali, Tanzania inalilia kupata viongozi wenye maono na uwezo wa kuongoza.

Rais wa 40 wa Marekani Bw. Ronald Reagan alipata kusema hivi:-
"In this present crisis, government is not the solution to our problem; government is the problem" Jan. 1981

He was right then and he's still very right today.
 
Rev. Kishoka nakuunga mkono. Tatizo kubwa viongozi wengi wa Afrika wanatawala badala ya kuongoza. Na kiongozi haogopi kabisa kusema "Katika utawala wangu" badala ya "Katika uongozi wangu". Hapa ndipo shida ilipo. Itatuchukua muda kufikia maendeleo ya kweli.
 
Rev. Kishoka, hilo unalosema ni tatizo mtambuka, ni kasoro/kosa/udhaifu uliyo wazi kabisa lakini tumekuwa na tabia ya kuuzunguka mbuyu tu.

Tanzania inalilia na inahitaji sana Katiba Mpya. Sambamba na kuhitaji mabadiliko chanya ya muundo wa Serikali na mabadiliko makubwa ya mfumo wa utendaji wa serikali, Tanzania inalilia kupata viongozi wenye maono na uwezo wa kuongoza.

Rais wa 40 wa Marekani Bw. Ronald Reagan alipata kusema hivi:-
"In this present crisis, government is not the solution to our problem; government is the problem" Jan. 1981

He was right then and he's still very right today.

Ni kweli tunahitaji KATIBA ituongoze na si Mawazo ya mtu mmoja.Tunahitaji viongozi watakaoiogopa Katiba kama wagopavyo Mungu ili tuweze kwenda mbele
 
Guys... Who is legal advisor wa Rais Magufuli? Au advisor wa namna yeyote ile?

Hii ziara ya Pwani yametokea matamko ya Rais ya kusema "katika utawala wangu" but kwangu naona hakuna jitihada kuweka mfumo, kanuni Na Sheria Imara zinazoeleweka ili uwajibikaji uwe ni kitu Na tunu ya kawaida si mfumo w utegemezi wa kiongozi mkuu wa nchi au hamasa yake kuongoza Na "kunyoosha" Taifa!

JPM alipokujaa alishangaa kukuta madudu na machafu kupindukia, sababu yawezekana sana kuwa JK naye alisema "katika utawala wangu" akajifanyia mambo Na maamuzi mengi ambayo Magufuli anayashangaa. Labda naye Kikwete alikuta aliyoyarithi ambayo yalifanywa kwa mantiki ya "katika utawala wangu.." iwe ni Serikalini au hata katika Chama.

Leo Magufuli anaongoza nchi Na kufanya kila kitu kwa kigezo cha "katika utawala wangu" Keaho akiondoka Magufuli, atakayekuja naye atasema "katika utawala wangu" na kubadilisha Yale yaliyofanya "katika utawala wangu" wa Magufuli !

Now nikiangalia kwa nini kuna non-responsive kutoka taasisi, mashirika, Serikali, watendaji Na hata wananchi, jibu lake ni kila mtu anajua "katika utawala wangu" utapita Na kuna expiry date Na si mfumo unaoeleweka kisheria... Wanapuuzia wanajua wakisema "ametukuta, ataondoka, atatuacha"!

Nchi imekuwa ikiendeshwa au kuongozwa na maamuzi kufanywa kwa dhana na fikra za "katika utawala wangu.." kuanzia Rais mpaka Mkuu wa Wilaya au hata mwenyekiti wa kijiji kupuuzia kabisa mipaka ya kisheria, mamlaka,kanuni hata katiba.

Zaidi, dhana hii ya "Katika utawala wangu.." si kwamba imekwamisha maendeleo ya jamii na Taifa, lakini hata imepunguza uwajibikaji wa kweli, kujenga kiburi nauungwana wa kukiri makosa, kujikosoa au kujisahihisha kunakosekana.

Mfano inawezekana DC wa Hai juzi akivunjavunja shamba la Mbowe alitumia kigezo hicho cha "katika utawala wangu.." au leo Mkuu wa TRA Arusha anaposema ukikutwa huna risiti fainielfu thelathini, naye anatumia nguvu ya "katika utawala wangu".

Keshoanapokuja mtendaji au kiongozi mwingine naye akasema "katika utawala wangu" (mfano mzuri ni Nape na Mwakyembe wizara ya habari) naye akaamua kusema anabadilisha na kufuta kila kilichofanywa na aliyemtangulia kwa kuwa "katika utawala wangu" haoni manufaa.

Kuna tofauti ya kufanya mambo "katika utawala wangu" kama mambo hayo hayahusu kanuni, sheria, taratibu, katiba au maamuzi yenye impact kubwa kwa jamii na Serikali.

Ni haki kusema "katika utawala wangu" uvivu,uzembe, ubabaishaji, uchelewaji, umangimeza, uhujumu nu mwiko na kamwe hautavumiliwa. Lakini kuna haja ya kuweka na kurejea misingi iliyopo na kuhoji kwa nini utovu wa nidhamu upo na au unaongezeka!

Leo Rais Magufuli kawasema Brela mpaka kutoa tamko (presidential executive order) verbally kuwa wenye nia ya kuanzisha viwanda au biashara wasisubiri Brela, waanze mchakato maana Brela wanajivutavuta na kupunguza kasi ya maendeleo na azma ya viwanda ya awamu ya tano. Najiuliza je kwa nini Brela leo ni miezi 20 tangu awamu ya Tano iingie madarakani bado inajivutavuta na kuwa na umangimeza au ukiritimba ambao unakwamisha ufanisi? je hawana kanuni za uwajibikaji? au usimamizi wa kanuni za uwajibikaji na majukumu zina mapengo na mianya ya uzembe, uhujumu au hata kulea rushwa na kero?

Je yawezekana huko Brela hakuna hizi kanuni kwa kuwa kila mkubwa wa sehemu anafanya mambo ya "katika utawala wangu" na kujiamulia mambo na wafanyakazi wa chini kwa kukosa mfumo unaoeleweka na kushuhudia kwao wakubwa wakifanya mambo kwa itikadi ya "katika utawala wangu" basi wanajijengea kiburi cha "alitukuta, atapita, atatuacha hapahapa"?

May be tukiongelea mambo kwa mtazamo huu, ubishi na ushabiki unaopinga kujengwa kwa mfumo huru Imara kuanzia Katiba, Sheria na Kanuni hata uwajibikaji wake utaangalia mambo kiuhalisia Na si kushangilia current happenings ambazo "baada ya utawala wangu" tutarudi kule kule au atakuja mwingine na mtazamo wake na kusema "katika utawala wangu"?
The Obama administration.
Bush Administration
Clinton Administration.
Sema jingine
 
Back
Top Bottom