Dhana hii ni mbaya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dhana hii ni mbaya.

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Jrafiki, May 9, 2012.

 1. J

  Jrafiki Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi nimekuwa msomaji wa mambo yanayohusu ajira na kazi,humu watu hutoa mawazo yao na wengine kuomba ushauri nini wafanye ili either wapate kuajiriwa ama kujiajiri kulingana na elimu zao ama matakwa ndani ya mioyo yao ili mwishowe wajinasue na hali ngumu ya kimaisha iliyopo sasa.Ki ukweli sifurahishwi na baadhi ya wachangiaji ambao hushauri wenye hizo shida kujiajiri pasipo KUWAAMBIA NI KWA NAMNA GANI WATAJIAJIRI.Na pia kuna wengine hufika mbali na kuwaona wasioajiriwa ni wale wenye matokeo mabaya kitaaluma.Haitoshi kuna wengine huwaona wanaosema KUJIAJIRI PASIPO MTAJI HAIWEZEKANI wameshndwa kutumia elimu zao kujinasua mwishowe huwabeza.
  Nataka niseme kitu hasa katika eneo la kujiajiri:
  Safari ya kuanzisha biashara ama mradi huanzia ktk mawazo ya mtu/watu kwanza,ili ufanye biashara kisasa ni vema uandae business plan.Kuandaa business plan peke yake kunahitaji pesa.Ili uandae business plan ni lazima ufanye study ya mambo mengi juu ya hicho kitu unachotaka kukianzisha ie upatikanaji wa malighafi,upatikanaji wa wateja,njia ktk kufanya uzalishaji n.k.
  Ili hiyo study itimie inabidi ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa/walioshndwa ktk hilo unalotaka kulianzisha(ikiwa ni biashara ama mradi ambao tayari kuna wengne walishaufanya),kwa hiyo huna budi kuwatembelea na kuongea nao.Pia study itakuhitaji uwe na nyenzo za kukusaidia kujua kinadharia pia juu ya hilo ulifanyalo,kwa hiyo utahitaji kusoma vitabu vinavyoelezea maswala hayo,computer iliyounganishwa na internate kukusaidia kufahamu zaidi juu ya hicho ukiwazacho.KWA HAYO YA KUFANYA STUDY ILI UANDIKE BUSINESS PLAN KUTAKUHITAJI PESA NA MUDA.Ikumbukwe hapo ni study tu ambayo itakuja na jibu la nini ufanye bado hujafika ktk mtaji.Tuache siasa,mtu asiongee kwa sababu yeye ana kazi basi akachukulia haya mambo kirahirahisi na KUSEMA PESA HAZIHITAJIKI Kwa wenye mawazo ya kujiajiri.
  Jiulize?unawezaje kuandaa business plan ukiwa nyumbani kwako tu?hakika haiwezekani.
   
 2. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Mkuu wengi wanaongea tu kama fashen...wakishapata vibarua vya kubadilisha mboga wanajisahau
   
 3. m

  manasa Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana.......... ndo binadamu jinsi walivyo kusema ni rahisi kuliko kutenda....
   
 4. Edoedward1

  Edoedward1 JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 799
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 60
  Kaka mimi binafsi ni muhanga wa hili swala na limekuwa likiniumiza kichwa kiukweli hadi nikawa naji re-asses kwamba labda am not thinking straight ndio maana am stack....well hawa watu wapo tu na huwa wanasema hivyo kwa kusikia tu hawajawahi kuwa in that situation in practical.
  Nakuheshimu kwa mawazo yako mkuu!!!
   
 5. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,728
  Likes Received: 12,797
  Trophy Points: 280
  kweli kabisa
   
Loading...