Dhambi ya usaliti ni mbaya sana

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,793
Reaction score
5,042
Dhambi ya usaliti, mbaya dhambi ya usaliti, yaani dhambi ya usaliti ndio dhambi kubwa kwenye usaliti. Yes, dhambi ya usaliti. Mwaka 1960, Kasavubu alimsaliti Patrice Lumumba, akashiriki kupanga, kuinjinia na kuratitbu kuuawa kwa Lumumba, sio kuuwawa tu, bali mauaji ya kinyama, mipango yote alipewa Mobutu kuratibu.

Baada ya Lumumba kuuwawa Kasa-Vubu alimpandisha cheo jeshini Mobutu kuwa Luteni Jenerali, na kumteua kuwa mkuu wa majeshi, yote hayo yalifanyika mwaka 1965. Ona Sasa usaliti unavyotafuna, Mobutu baada ya kupandishwa cheo nae akampindua Kasavubu siku 6 baadaye. Ukila nyama ya mtu huwezi kuacha.

Siku 2 baada ya Kasavubu kupinduliwa Mobutu akapanga njama ya kumkamata Kasavubu, Kasavubu aliposikia akataka kutoroka, Mobutu akamkamata na kumuweka Kasa-Vubu chini ya kizuizi cha nyumbani (under house arrest). Alikaa hapo kwa miezi 15 mpaka alipokubali kutangaza kustaafu siasa na kutojihusisha na siasa, akapigwa kufuli, ubaya hauozi.

Kasavubu alipewa sharti la kuishi nyumbani tu yaani katika shamba lake huko Mayombe, hakuna kutoka nyumbani bila kibali cha Mobutu. Kasa-Vubu alifariki katika hospitali ya Boma miaka minne baadaye yaani mwaka 1969, baada ya kuugua kwa muda mrefu na kukosa uangalizi. Hii ndio dhambi ya usaliti.
 
Historia nzuri yenye funzo
 
Safi sana Mobutu alifanya jambo zuri sana.
 
Bado Sa100 na wahuni wenzake kwa kumsaliti JPM na Watanzania wazalendo .....
Kwake sa100 uzalendo ni maviii
 
Samweli Doe alitumwa kwenda kumuuwa Rais William R. Tolbert, aliyekuwa anaiyongoza Liberia muda huo.Samwel Doe kwa tamaa baada ya kumuuwa Rais akaenda kuwauwa na wale waliyomtuma na kisha akajitangaza kuwa yeye ndiye kiongozi mpya wa Liberia na rafiki yake Charles taylor akampa uwongozi.

Charle taylor akaiba pesa nyingi akakimbia nchi akaenda kutengeneza waasi alivyorudi akanzisha vikundi vya waasi zidi ya swaiba wake.mwisho wa siku Samwel Doe alikufa kifo kibaya na cha aibu huku swaiba wake akichukua kiti chake
 
Liberia ni nchi ukisoma siasa zake utaenjoy sana..kuna kulikua na makundi mawili wazawa masikini na matajiri ambao walitokea usa wenye asili ya liberia walio rudi liberia baada ya utumwa kukomeshwa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Bado Sa100 na wahuni wenzake kwa kumsaliti JPM na Watanzania wazalendo .....
Kwake sa100 uzalendo ni maviii
Jpm anatesema motoni kwa kuwatesa wana wa nchi na kuwaua na kupoteza maelfu
 
Liberia ni nchi ukisoma siasa zake utaenjoy sana..kuna kulikua na makundi mawili wazawa masikini na matajiri ambao walitokea usa wenye asili ya liberia walio rudi liberia baada ya utumwa kukomeshwa.

#MaendeleoHayanaChama
Unakitu Cha kuhadithia alafu hutaki kutuhadithia.
 
Polen sana
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…