Dhambi ya bandari haitamuacha Jakaya Kikwete

Dhambi ya bandari haitamuacha Jakaya Kikwete

Kikwete kaishastaafu yuko Msoga anakula kuku choma...wewe unamsema humu unadhani analo lipi la kupoteza?.

Kama yapo aliyokosea huo ni ubinadamu kama wewe ulivyowatelekeza wazazi wako...

Hapa ndo mwisho wako kufikiri, au utarudi tena baadae mkuu! Kama ndo mwisho, una haki ya kuandika ulichoandika

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Jakaya Kikwete alikuta mnakusanya Billioni 250 akawapeleka kwenye trillioni moja za kodi kama hamna cha kumkumbuka basi nyie wepesi wa kusahau na wachoyo wa fadhila!
Hivi haujisikii vibaya kwa uliyoyaandika?
 
Mkuu Msemaji Ukweli nini hasa lengo la bandiko lako hili na mengine ya baada ya uchaguzi yanayoelekea kukosoa utawala uliopita?

Haya madhambi makubwa yanayohusisha viongozi wa juu serikalini yanayofisidi taifa mbona yameshazungumzwa sana hapa JF na kwenye media zingine? Tunachokiona ni watu wakihangaika kujibu kishabiki kutetea ama serikali na chama tawala kwa ujumla (huku wakiwaponda sana wanaoibua kashfa hizo kama "losers") AU wakitetea awamu tofauti serikalini kama vile nchi imekuwa ikiongozwa na vyama tofauti vyenye sera tofauti tofauti.

Serikali iliyopo madarakani leo hii ni muendelezo wa tawala zilizopita tangia uhuru. Ni mapema mno kuitofautisha na zilizopita. Chama tawala ni kilekile na viongozi wake wengi si watu wageni serikalini. Hebu tuvute angalau mwaka tupate hiyo jeuri ya kuitenga awamu hii na zilizoitangulia.
 
K
Mazuri yote aliyoyafanya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete yameanza kuyeyuka kama dheluji inayokabiliana na tanuri la moto. Dhambi ya madudu ya bandari haiwezi kumuacha Rais Mstaafu, Kikwete. Dhambi hii imeanza kuyafuta yale yote mazuri aliyoyafanya katika utawala wake!

Rais Kikwete amefanya mambo mengi ya maendeleo pamoja na kwamba kwa kiasi kikubwa msingi wake ni mikopo na misaada. Ikumbukwe Mwaka 2005 deni la taifa lilikuwa shilingi trilioni 10. Leo miaka 10 katika utawala wa Rais Kikwete, limefikia karibia Shilingi trilioni 40.

Yaliyotokea/yanayotokea bandarini yanadhihirisha sababu ya ukuaji wa uchumi wetu kushuka chini. Mwaka 2005, uchumi wetu ulikuwa unakuwa kwa asilimia 6.7 lakini leo umeshuka hadi wastani wa asilimia 6.4. Mbaya zaidi hata huu ukuaji wa uchumi haunufaishi wananchi wengi.

Uchumi uliopo siyo uchumi shirikishi ambao utawanufaisha wananchi wengi. Uchumi uliopo unawanufaisha watu wachache ambao msingi wa utajiri wao ni wizi na ukwepaji kodi.

Uchumi hauwezi kukua wakati maelfu ya makontena/bidhaa zinapita bandarini bila kulipiwa ushuru. Bidhaa hizo pia zimechangia sana katika kuharibu soko (negative price distortion) matokeo yake hata viwanda vyetu vya ndani ya nchi vinashindwa kupambana kwenye soko katika usawa . Bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi zinakuwa aghari kulinganisha na bidhaa nyingi kutoka nje kwa sababu zinakuwa hazijalipiwa ushuru.

Athari hii imesababisha viwanda vingi kuwa ni magofu au magodauni ya kupokea bidhaa kutoka nje ambazo nyingi zinakuwa hazijalipiwa ushuru. Kwa nini nihangaike kuzalisha bidhaa hapa nchini wakati ninaweza kuagiza nje ya nchi na kuziingiza nchini bila kulipia ushuru as a result, ninakuwa na uamuzi mpana kwa kuamua bei ya bidhaa ukilinganisha na yule anazalisha hapa nchini.

Kubwa zaidi, kabla ya serikali haijaanza kuwalalamikia wale wamegeuza viwanda kuwa magodauni, lazima nayo pia ijitazame kwa sababu imekuwa ni chanzo cha viwanda vya ndani kushindwa kukabiliana na soko la ndani.

Serikali inatakiwa kwanza itengeneze mazingira sawa katika soko kabla ya kuanza kuwawajibisha waliogeuza viwanda kuwa magodauni.

Kwa kumpigania JPM kuingia ikulu tayari Sir God kesha msamehe manake Kina Mboe wangewafanyia kitu mbaya waTZ na gia zao angani.
 
Jakaya Kikwete alikuta mnakusanya Billioni 250 akawapeleka kwenye trillioni moja za kodi kama hamna cha kumkumbuka basi nyie wepesi wa kusahau na wachoyo wa fadhila!
Unachokisema nimekiandika katika bandiko langu lakini kuna hatari kubwa hata hizo juhudi zake zitapotea kwa sababu ya uchafu unaoendelea kujitokeza kutokana na utawala wake.

Kuna wengine kwa sasa wanasema, tulichopoteza katika utawala wa Rais Kikwete ni zaidi ya tulichopata katika utawala wake!
 
Jakaya Kikwete alikuta mnakusanya Billioni 250 akawapeleka kwenye trillioni moja za kodi kama hamna cha kumkumbuka basi nyie wepesi wa kusahau na wachoyo wa fadhila!
Tulipaswa kukusanya zaidi ya hicho kwa fursa zilizokuwepo nchini kwetu kwa hiyo acha kumsifia mzee tezi.
 
Ila zambi ya wapinga ufisadi kumkumbatia fisadi hii zambi itamtafuna tundu lissu,mnyika,nk
Lowassa alitumia fani yake ya usanii na fimbo ya kisiasa kuwachapa CHADEMA kwa kuwapa kazi ya kumsafisha baada ya kumchafua kwa miaka zaidi ya minane.

Wengi wa viongozi wakuu wa CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana wamedhihirisha ni wachumia tumbo.
 
Jakaya Kikwete alikuta mnakusanya Billioni 250 akawapeleka kwenye trillioni moja za kodi kama hamna cha kumkumbuka basi nyie wepesi wa kusahau na wachoyo wa fadhila!
Mkuu trilioni moja sikatai lakini niliona kama alikuwa anakusanya wastani wa bilioni 700 hadi 800 sisemi kama ni ndogo lakini kwa kweli ktk serikali iliyopita tumeibiwa sana kama nchi.
 
Mazuri yote aliyoyafanya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete yameanza kuyeyuka kama dheluji inayokabiliana na tanuri la moto. Dhambi ya madudu ya bandari haiwezi kumuacha Rais Mstaafu, Kikwete. Dhambi hii imeanza kuyafuta yale yote mazuri aliyoyafanya katika utawala wake!

Rais Kikwete amefanya mambo mengi ya maendeleo pamoja na kwamba kwa kiasi kikubwa msingi wake ni mikopo na misaada. Ikumbukwe Mwaka 2005 deni la taifa lilikuwa shilingi trilioni 10. Leo miaka 10 katika utawala wa Rais Kikwete, limefikia karibia Shilingi trilioni 40.

Yaliyotokea/yanayotokea bandarini yanadhihirisha sababu ya ukuaji wa uchumi wetu kushuka chini. Mwaka 2005, uchumi wetu ulikuwa unakuwa kwa asilimia 6.7 lakini leo umeshuka hadi wastani wa asilimia 6.4. Mbaya zaidi hata huu ukuaji wa uchumi haunufaishi wananchi wengi.

Uchumi uliopo siyo uchumi shirikishi ambao utawanufaisha wananchi wengi. Uchumi uliopo unawanufaisha watu wachache ambao msingi wa utajiri wao ni wizi na ukwepaji kodi.

Uchumi hauwezi kukua wakati maelfu ya makontena/bidhaa zinapita bandarini bila kulipiwa ushuru. Bidhaa hizo pia zimechangia sana katika kuharibu soko (negative price distortion) matokeo yake hata viwanda vyetu vya ndani ya nchi vinashindwa kupambana kwenye soko katika usawa . Bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi zinakuwa aghari kulinganisha na bidhaa nyingi kutoka nje kwa sababu zinakuwa hazijalipiwa ushuru.

Athari hii imesababisha viwanda vingi kuwa ni magofu au magodauni ya kupokea bidhaa kutoka nje ambazo nyingi zinakuwa hazijalipiwa ushuru. Kwa nini nihangaike kuzalisha bidhaa hapa nchini wakati ninaweza kuagiza nje ya nchi na kuziingiza nchini bila kulipia ushuru as a result, ninakuwa na uamuzi mpana kwa kuamua bei ya bidhaa ukilinganisha na yule anazalisha hapa nchini.

Kubwa zaidi, kabla ya serikali haijaanza kuwalalamikia wale wamegeuza viwanda kuwa magodauni, lazima nayo pia ijitazame kwa sababu imekuwa ni chanzo cha viwanda vya ndani kushindwa kukabiliana na soko la ndani.

Serikali inatakiwa kwanza itengeneze mazingira sawa katika soko kabla ya kuanza kuwawajibisha waliogeuza viwanda kuwa magodauni.
thread ya bwe'ge katika ubora wake
umesema huo ukuaji wa uchumi wa 6.4% (kitu ambacho ni uongo) ulikuwa hauwanufaishi wananchi je huo ukuwaji wa 6.7% wa mkapa ulikuwa unanufaisha wananchi kwa kiasi gani?
negative price distortion ndo nini? (hii inaonesha jinsi ulivyo mpumbavu maana hata unachokiandika kwenyewe huelewi
na la mwisho kwa nini vitu vinavyozalishwa hata nchini viuzwe bei kubwa kuliko vilivyosafirishwa kutoka mbali hata kama havihalipiwa ushuru? kuna tatizo hapo zaidi ya hili unalofikiria wewe.
 
Jakaya Kikwete alikuta mnakusanya Billioni 250 akawapeleka kwenye trillioni moja za kodi kama hamna cha kumkumbuka basi nyie wepesi wa kusahau na wachoyo wa fadhila!
mkuu ni bil 170 na sio bil 250.
 
..vipi tena leo?

..dhambi ya kwanza ya JK ni IPTL.

..hizo nyingine zimefuata.

..kinachonisikitisha ni vile alivyoweza kuwarubuni wa-Tz.

..wapinzani wamepiga sana kelele. lakini mbele ya wananchi walikuwa wanaonekana wapumbavu.

..JF imepiga kelele kwa muda mrefu kuhusu utawala mbovu wa JK.

..yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Tuombe MUNGU Magufuli asije akatuhujumu.
Ukianza kuweka hoja za wapinzani kupiga kelele kuhusu uendeshaji wa serikali ya Rais Kikwete unakuwa unakosa political locus standi.

Wapinzani na hasa CHADEMA walikosa moral authority ya kuinyoshea vidole serikali ya Rais Kikwete baada ya wao wenyewe kuanza kuzigeuka hoja na ahadi zao.

Kabla ya uchaguzi walisema wakichaguliwa hawatazipokea posho za vikao kwa wabunge, lakini wakazipokea baada ya kuchaguliwa.

Mbowe alidai, hawezi pokea gari la KUB na kwa maana hiyo, serikali iliuze ili pesa zake zikasaidie huduma za jamii, lakini baada ya muda akala matapishi yake. Kwa mazingira haya, wananchi waliona kelele za wapinzani ni debe tupu na hawamaainishi kile wananchokisema au kukiahidi.
 
Mkuu Msemaji Ukweli nini hasa lengo la bandiko lako hili na mengine ya baada ya uchaguzi yanayoelekea kukosoa utawala uliopita?

Haya madhambi makubwa yanayohusisha viongozi wa juu serikalini yanayofisidi taifa mbona yameshazungumzwa sana hapa JF na kwenye media zingine? Tunachokiona ni watu wakihangaika kujibu kishabiki kutetea ama serikali na chama tawala kwa ujumla (huku wakiwaponda sana wanaoibua kashfa hizo kama "losers") AU wakitetea awamu tofauti serikalini kama vile nchi imekuwa ikiongozwa na vyama tofauti vyenye sera tofauti tofauti.

Serikali iliyopo madarakani leo hii ni muendelezo wa tawala zilizopita tangia uhuru. Ni mapema mno kuitofautisha na zilizopita. Chama tawala ni kilekile na viongozi wake wengi si watu wageni serikalini. Hebu tuvute angalau mwaka tupate hiyo jeuri ya kuitenga awamu hii na zilizoitangulia.
Ninakosoa utendaji wa serikali katika mlengo wa kujenga!

Binadamu tunatofautiana, wengine ni pessimistic na wengine kama mimi ni optimistic.

Serikali ya Rais Magufuli haiwezi kufanana na serikali zilizopita. Take my word!
 
Mbona amkuwa mkisema haya wakati yuko madarakani wana CCM kwa asilimia kubwa mlikuwa mnamsifia na kumtetea kwa kila jambo serikari imeenda kutumia mabillioni ambayo yangeweza jenga vituo vya afya katika kila wilaya vyenye hadhi kwenye katiba mpya leo hakuna chama cha siasa, waandandishi wa habari na viongozi wengine wa asasi za kijamii wanaotaka kujua kura ya maoni inafanyika lini.

Leo tena tunarudi pale pale ukisikiliza watu wa dini, waandishi wa habari, wanasiasa active, watumishi wa umma kwa sasa na wastaafu kila anachofanya magufuli ni sahihi 100% kama walivyokuwa wakisifia JK wakati yuko madarakani (ukiona kila mtu anakusifia kwa kila kitu jua auko na watu sahihi mafanikio ni team work and compromising on ideas sio kwamba utakuwa sahihi muda wote).

Kila mtu ana style yake ya uongozi JK kwake ilikuwa laissez faire trust kwa wasaidizi wake kufanya kazi kwa ufanisi bila ya kuwaingilia (unless una ushahidi wa yeye mwenyewe kubariki makosa) labda tatizo kubwa ni kudhani na kutoelewa technical abilities watu wanazohitaji kwa sehemu zingine alizokuwa anawateua.

Leo kuna raisi mpya na yeye anastahili yake magufuli ni autocratic na anataka kila mtu anayemteua aone result kwa kupima mwenyewe kutokana na kile wanachodhani kinapaswa kufanyika bila ya kujali quality fulani inapatikana; kutakuwa na mabadiliko kwa sababu magufuli ni mtu wa kuchukua hatua pale penye uzembe lakini not to the highest possibilities kwa sababu na yeye anarudia vile vile kuweka watu wasio na technical abilities vinginevyo ungeweza kuona watu wana scrutinize processes kwanza kabla ya ziara (jana Mwigulu kabaini wizi wa kodi machinjoni wakati TRA walitakiwa wafanya kazi ya audit za kodi zinaweza kupotea wapi sio waziri na kuchukua hatua za kuziba mianya na kuna sehemu nyingi tu kodi aikusanywi vilivyo)

Naweza kuwa mimi ndio siko sahihi lakini ni muhimu kuangalia mambo kwa ufahamu wako na kuyatolea opinion lakini kwa wana CCM kikawaida kwa raisi hakuna makosa mpaka atakapo toka mimi binafsi naona bila ya kufanya audit processes za serikari kwanza hakuna mafanikio tutaona ziara na watu kutumia nguvu sana badala ya akili kwenye kujaribu kubadilisha mambo so far hiyo ndio trend labda kama mambo yatabadilika mbele na yakibaki hivi basi sitarajii tofauti za vile; Magufuli mwenyewe miezi miwili tu ukimwangalia uso ushachoka inaoenakana ugumu wa kazi yenyewe tayari kesha anza kuulewana jinsi alivyo serious na mabadiliko.
 
Last edited:
Jakaya Kikwete alikuta mnakusanya Billioni 250 akawapeleka kwenye trillioni moja za kodi kama hamna cha kumkumbuka basi nyie wepesi wa kusahau na wachoyo wa fadhila!

Na kipindi hicho inakusanywa 250Bl dola moja ilikuwa ina thamani gani kulinganisha na wakati anaondoka kwa makusanyo ya trilioni moja?
 
Back
Top Bottom