Dhambi ya bandari haitamuacha Jakaya Kikwete

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Mazuri yote aliyoyafanya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete yameanza kuyeyuka kama dheluji inayokabiliana na tanuri la moto. Dhambi ya madudu ya bandari haiwezi kumuacha Rais Mstaafu, Kikwete. Dhambi hii imeanza kuyafuta yale yote mazuri aliyoyafanya katika utawala wake!

Rais Kikwete amefanya mambo mengi ya maendeleo pamoja na kwamba kwa kiasi kikubwa msingi wake ni mikopo na misaada. Ikumbukwe Mwaka 2005 deni la taifa lilikuwa shilingi trilioni 10. Leo miaka 10 katika utawala wa Rais Kikwete, limefikia karibia Shilingi trilioni 40.

Yaliyotokea/yanayotokea bandarini yanadhihirisha sababu ya ukuaji wa uchumi wetu kushuka chini. Mwaka 2005, uchumi wetu ulikuwa unakuwa kwa asilimia 6.7 lakini leo umeshuka hadi wastani wa asilimia 6.4. Mbaya zaidi hata huu ukuaji wa uchumi haunufaishi wananchi wengi.

Uchumi uliopo siyo uchumi shirikishi ambao utawanufaisha wananchi wengi. Uchumi uliopo unawanufaisha watu wachache ambao msingi wa utajiri wao ni wizi na ukwepaji kodi.

Uchumi hauwezi kukua wakati maelfu ya makontena/bidhaa zinapita bandarini bila kulipiwa ushuru. Bidhaa hizo pia zimechangia sana katika kuharibu soko (negative price distortion) matokeo yake hata viwanda vyetu vya ndani ya nchi vinashindwa kupambana kwenye soko katika usawa . Bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi zinakuwa aghari kulinganisha na bidhaa nyingi kutoka nje kwa sababu zinakuwa hazijalipiwa ushuru.

Athari hii imesababisha viwanda vingi kuwa ni magofu au magodauni ya kupokea bidhaa kutoka nje ambazo nyingi zinakuwa hazijalipiwa ushuru. Kwa nini nihangaike kuzalisha bidhaa hapa nchini wakati ninaweza kuagiza nje ya nchi na kuziingiza nchini bila kulipia ushuru as a result, ninakuwa na uamuzi mpana kwa kuamua bei ya bidhaa ukilinganisha na yule anazalisha hapa nchini.

Kubwa zaidi, kabla ya serikali haijaanza kuwalalamikia wale wamegeuza viwanda kuwa magodauni, lazima nayo pia ijitazame kwa sababu imekuwa ni chanzo cha viwanda vya ndani kushindwa kukabiliana na soko la ndani.

Serikali inatakiwa kwanza itengeneze mazingira sawa katika soko kabla ya kuanza kuwawajibisha waliogeuza viwanda kuwa magodauni.
 
Kikwete kaishastaafu yuko Msoga anakula kuku choma...wewe unamsema humu unadhani analo lipi la kupoteza?.

Kama yapo aliyokosea huo ni ubinadamu kama wewe ulivyowatelekeza wazazi wako...
 
Dhambi hii haisameheki, duniani hata mbunguni, haita iacha na itazidi kuitafuna CCM na serikali yake,
Kuna watu wako mitaani kwa kukosa kazi baada ya bidhaa ambazo hazijalipiwa ushuru kujaa kwenye soko na kusababisha bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini kukosa soko la ndani.
 
Jakaya Kikwete alikuta mnakusanya Billioni 250 akawapeleka kwenye trillioni moja za kodi kama hamna cha kumkumbuka basi nyie wepesi wa kusahau na wachoyo wa fadhila!
 
Mwacheni apumzike. Alichofanya kinatosha ila ametuangusha sana!
Hakuna aliyesema asipumzike!

Hata Katiba yetu ya 1977 inawataka Watanzania kutomsumbua Rais Mstaafu kwa kumfungulia mashitaka kwa makosa aliyoyafanya akiwa Rais wa Tanzania.
 
Jakaya Kikwete alikuta mnakusanya Billioni 250 akawapeleka kwenye trillioni moja za kodi kama hamna cha kumkumbuka basi nyie wepesi wa kusahau na wachoyo wa fadhila!
Richmond, Escrow, tembo, twiga, drugs, makontena, division 5, hospitali kukosa dawa na vitendea kazi, rushwa ...,
 
Jakaya Kikwete alikuta mnakusanya Billioni 250 akawapeleka kwenye trillioni moja za kodi kama hamna cha kumkumbuka basi nyie wepesi wa kusahau na wachoyo wa fadhila!
Utupigie na hesabu Wakati anakabidhiwa nchi $ ili ngapi dhidi sh/=. Usijekuwa unashangilia wingi wa magoli Wakati umetanua lango.
 
..vipi tena leo?

..dhambi ya kwanza ya JK ni IPTL.

..hizo nyingine zimefuata.

..kinachonisikitisha ni vile alivyoweza kuwarubuni wa-Tz.

..wapinzani wamepiga sana kelele. lakini mbele ya wananchi walikuwa wanaonekana wapumbavu.

..JF imepiga kelele kwa muda mrefu kuhusu utawala mbovu wa JK.

..yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Tuombe MUNGU Magufuli asije akatuhujumu.
 
Jakaya Kikwete alikuta mnakusanya Billioni 250 akawapeleka kwenye trillioni moja za kodi kama hamna cha kumkumbuka basi nyie wepesi wa kusahau na wachoyo wa fadhila!
tatizo malezi, tembelea maeneo ya bagamoyo ndio ujue uchapakazi wao
 
JPM piga kazi utuvushe hapa pia Dola ishuke maana hali ilikuwa mbaya kwa sisi wajasiriamali wadogo tukiagiza vijinguo vya kuuza kariakoo
 
Back
Top Bottom