wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,931
- 4,549
Wana jamvi kila utendalo hapa duniani huwa linalipwa kwa kadri ulivyotenda,rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy alipewa $ milioni 50 na hayati Gaddafi ili zimsaidie ktk kampeni zake,na walikuwa marafiki wakubwa, na Gaddafi alijua siri nyingi sana kuhusu rais Sarkozy,lakini ajabu ni huyo huyo rais aliyeongoza kihelehele cha NATO kuivamia Libya,Ufaransa chini ya Sarkozy ndo iliongoza mashambulizi ya anga dhidi ya Libya na kisha rais mnafiki yule akatuma majajusi waliojichanganya na waasi na kisha kumuua Gaddafi kwa kumpiga risasi ya kichwa,leo hii ufaransa wanalia kilio cha mbwa,wananchi wasio na hatia wamekufa kwa dhambi ambayo hawajaitenda,mataifa ya magharibi hususan Marekani,Uingereza,na Ufaransa yenyewe wamekuwa wakitengeneza silaha na kisha kuziuza kwa mataifa maskini huku wakichochea ugomvi,Marekani na kampuni lake kubwa la Martin Lockheed ndo inaongoza kufanya unyama huo,hebu ingia hapa www.who killed gaddafi?.com ndo utajua kuwa wazungu si ndugu zetu sisi watu weusi,na africa kwa ujumla.