Dhambi isiyokuwa na msamaha (unforgiven sin)

Mkuu usiwape kiburi wauwaji...hasa hawa viongozi . nakwambia tena dhambi kubwa kuliko zote ni ile ya kumwaga damu ya Mwanadamu wenzako hasa isiyo na hatia.
 
Mr Ndege John haupo makini,kinachozungumziwa ni kukufuru roho mtakatifu sio roho takatifu.
KUKUFURU ROHO MTAKATIFU NI PAMOJA NA KUITUKANA HYO NAFSI YA TATU
 
Dini zote ni mafumbo ya imani, zina maswali yasiyojibika au ambayo kila mtu anaweza kutoa jibu au tafsiri yake. Binafsi siamini dini yoyote naomba kukaa pembeni.
 
Tuanzie hapa Roho mtakatifu ni Mungu...
 
Mkuu usiwape kiburi wauwaji...hasa hawa viongozi . nakwambia tena dhambi kubwa kuliko zote ni ile ya kumwaga damu ya Mwanadamu wenzako hasa isiyo na hatia.
Ukitubu na kujiangusha kwa Mungu Utasamehewa ila kukufuru roho mtakatifu husamehewi maishaa
 



Mkuu Heri lee,

Kuna vitu hivi yakupasa uvitambue maana zake;-
(1) kukufuru ni neno linalo patikana kwa asili katika lugha za Semitic kama kiarabu, kiebrania, kiarmaic, nk, na maana yake ni kupinga au kukataa jambo au kumkataa mtu nk.

(2) Roho mtakatifu;- ni nguvu za utendaji wa Mungu, yaani Mungu anapotaka kufanya jambo lolote daima dawamu hutumia roho mtakatifu kwa lugha nyingine roho mtakatifu ni nguvu inayobebwa na malaika wa Mungu na ndiye yule Malaika aliyemtokea bikira Maria kumpasha habari ya kuzaliwa yesu.

(3) Kumkufuru yesu maana yake ni:- kumkataa au kumpinga yesu.
(4) kumkufuru roho mtakatifu maana yake ni:- kukataa/kupinga nguvu za utendaji za Mungu, sasa ukipinga nguvu za Mungu maana yake moja kwa moja umempinga Mungu na hapo hutasamehewa katika ulimwengu huu na ule ujao.

👆🏻Hapo Yesu alikuwa anawaambia Wana waisrael ambaye yeye alikuwa ni mtume wao (mathayo 12:24).
 
Nimekuelewa sana ila naomba tofauti ya kukufuru Mungu
Kukufuru roho mtakf
Na kumkufuru Yesu Kristo
Je aliemkufuru Mungu na Yesu hukumu yao ni ipi
 
Roho mtakatfu kama yuko ndani ya Yesu mbona dhmb yake inasameheka
 
Maana kamili ya kumkufuru roho mtakatifu ni pale unapojua kosa au dhambi lakini unashupaza shingo kutubia kadili unavyoendelea kfanya hivyo inafikia hatua roho mtakatifu ambaye anakaa ndani yetu huanza taratibu kuondoka hatimaye mtu huyu anafikia hatua hata akitenda dhambi hajutii wala hauni kosa kutenda dhambi , yani ile roho inayokwambia ilinikosa inaondoka , ukifikia hatua hii wewe huwezi tena kusamehewa maana yake hauwezi kufikia hatua ukajutia matendo yako maovu yani unakua umepotea jumla , kipimo kizuri ukiona unajutia dhambi zako ujue bado roho yupo ndani yako lakini ukiendeleza uovu utafikia hatua utahalalisha dhambi kuwa jambo la kawaida kama matokeo ya kucheza dhambini.
 
Huu ni uongo kamili hakuna mafundisho ya roho kuishi baada ya kifo katika ukristo , haya ni mafundisho ya shetani ambayo alisema hakika hamtakufa mtakua mkijua mema na mabaya , imani ya umizimu imeingizwa ndani ya kanisa kwa mafundisho kama haya
 
Kumkufuru Roho Mtakatifu ni ile Haki ya kutokuamini licha ya kila kitu(uwezo wa MUNGU kuwekwa wazi)mf kitendo cha viongozi wa Kiyahudi kumkataa Yesu Kristo licha ya kuonyesha Miuhiza isiyo ya kawaida kama kumfufu Lazaro baada ya kuwa kaburini kwa siku 3 na zaidi,Yesu aliweza hadi kusoma Fikra na Mawazo yao juu ya wao kupanga njama za Kumua lakini walibishana na Nguvu uliyokuwa ndani yao ikiwashuhudia kwamba yeye ni Masihi.
kumbuka katika Yohana 16:9 Yesu anasema "kwahabari ya Dhambi sababu hawakuniamini mimi" na Pia Yohana 3:18 inasema ".. asiye mwamini yeye amekwisha kuhumiwa.."
kwahio Kukufuru ni Hali ya kutokuamini wokovu wa MUNGU kutipia Yesu Kristo
 
Hi pia ni maana nyingine mkuu , pia nimetoa maelezo yangu hapo juu
 
Sio kweli kukufuru ni kunena maneno kinyume chake na kutoa kashfa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…