DHAMBI HII YA CCM NA JK itawamaliza wenyewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DHAMBI HII YA CCM NA JK itawamaliza wenyewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyumbu-, May 27, 2011.

 1. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Katika kutapatapa kwa na kwa kufanya mambo ambayo hawajajiandaa na hawajui wafanyeje CCM na JK wamejikuta wanafanya dhambi hizi , na ambazo hazitawaacha salama:

  1. Kufuta azimio la Arusha na kutokuweka azimio mbadala lenye maslahi ya nchi hii ( Ally Hassan Mwinyi)
  2. Kuuza mashirika hovyo na kutokuanznisha mbadala. Hii imeua mashirika karibu yote yaliyoanzishwa wakati wa Mwalimu na kuacha watu wengi nje ya ajra huku wachache wakinufaika na biashara hii holela. Wanaofaidika na hili ni kina Abdalla Kigoda, Chenge, Mramba, Yona, to mention a few. (BM Mkapa)
  3.Kuingia Mikataba ya kinyonyaji isiyojali maslahi ya nchi. Mikataba kama Net Group Solutions, Madini, TTCL nk, imeifilisi nchi na kuiacha hoi ( Benjamin Mkapa
  3.Kuendeleza dhana ya " It is our turn to eat" ambayo serikali ya awamu ya nne imekuja nayo. Baada ya kupigia kelele ufisadi wa watangulizi wake, JK hakufanya kazi ya kusafisha uozo wa wenziwe huko nyuma. Alianza naye kutafuta kila njia ya kujilipa au kufisadi nchi " ikiwa ni zamu yao" kula pia. Wakaendeleza mikataba ya hovyo zaid tena ya kiuporaji kama Richmond, TRL-RITES ya rail , Buzwagi etc. Hii imekomba karibu kila kilichosalia na sasa
  nchi haina kitu cha kusema inacho. Si bandari, wala ndege, si rail wala madini. Ni shamba la bibi."Eti ni Zamu yetu na sisi kula" ( Jakaya Kikwete)
  4. Kunajisi kaburi la Baba wa Taifa; CCM na JK wameenda nyumbani kwa JK Nyerere na kufanya mkutano ambao ulibariki tu Mafisadi, na ukaasis mpasuko mkubwa zaidi wa kero za Muungano. Walienda kwa sifa eti wakashughulikie mafisadi. Kilichotoka kule butiama ni aibu. Siamini kama kuna mizimu, lakini aliye juu kuliko wote aliona kejeli hii. JK hawezi kuwa salama kwa hili. Kivuli cha Mwalimu kinamlilia. Mlienda kumdhihaki? ( Jakaya Kikwete)
  5.Kumshambulia Hayati Nyerere kwa "ukatoliki" wake. JK hata kumwita Nyerere Baba wa taifa anaona kinyaa. Badala yake anamwita "Mzee Nyerere". Sasa hata kama Nyerere mnasema aliuweka uislamu kama uadui, je njia sahihi ni kuendelea na nyinyi kuuchukia ukristo? Je si mwafanya dhambi ilel ile mnayoichukia ya mfumo Kristu? Hivi ni kweli Nyerere aliwabagua waislamu kwa uislamu wao? Je kina Mkapa ambao ni wakatoliki, mnajisikiaje kwa kadhia hii inayozidi kupaa kama vile manataka taifa liangamie leo? Kwa manufaa ya nani? Leo hii kuna Redio za dini, haziwezi kupitisha siku bila kukashifu imani za wengine. Hizi redio zinataja watu kwa majina kama kwamba ndo maadui wa dini zao. Matamko mazito yanatolewa eti kuhamasisha watu waukatae mfumo Kristo. Ni upi huo? Umeanzaje ghafla hivi? Leo hii watu waliooana kutoka dini tofauti, wafanyeje....watengane.? Huu upuuzi unanyamaziwa na serikali, na CCM na Raisi wa nchi. Waziri Mkuu naye kimya , ili tu watekeleze upuuzi wao wa kutufanye tufarakane ili waendelee na unyonyaji wao. Sasa wtau kama Pinda, miaka zaidi ya 60, mnakaa kimya ili mlinde vibarua vyenu...ili uishi miaka mingapi? Pinda wake up, there is no enough money on earth. Okoeni nchi na huu upuuzi wa udini.
  6. Ukabila. Leo hii JK, na serikali yake wanawabagua Wachaga kwa uchaga wao. Kisa , waasisi wa CHADEMA. Lakini, Lyatonga ambaye siyo CHADEMA, ni Mchaga Mzuri. Wa CHADEMA, ni wachaga uchuro. PAMBAFU! Hivi akina Mramba, Anna Mkapa, na wengineo mliobahatika " kuwa wajasiriamali" kupitia CCM, manjisikiaje wanapobaguliwa ndugu zenu ili tu mjenge uhalali wa kuendelea kulinda maslahi yenu kupitia CCM? Kama mndhani hizi siasa za ukabila hazitawwathiri, jiulizeni kinachotokea Zanzibar sasa. Yanachomwa makanisa ....dhambi ya kile kinachoitwa mfumo Kristo. Wamechomewa maduka "Wachaga" na bado mengi yanakuja. Hivyo Wachaga, jambo hili msilichukulie juu juu, act! Na Watanzania kwa ujumla act! Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005 akina Mwandosya waliitwa Wanyakusa ghafla. Baada ya Wachaga , Wambulu wanafuata?
  7. Ukatili wa kupita kiasi: Polisi leo hawana udugu na raia yeyote anayeonekana kuikosoa serikali. Wabunge wa upinzani wanapigwa hovyo, ingawa tuna kumbukumbu ya baadhi ya Ma OCD wetu waliopigwa mitama na wabunge wa CCM, na bado hao wabunge wasikamatwe. Si unajua Mbunge ana kinga? Lakini hiyo kinga iko kwa wabunge wa CCM tu, si upinzani. Sasa kwa dhambi hii hii, ikitokea Chama cha "upinzani" kikachukua dola kwenye uchaguzi halali, noa wakaamua kunyanyasa wabunge wa kitakachokuwa Chama cha upinzani, CCM tutajisikiaje? Upumbavu huu uachwe mara moja!
  8.Ushirikina wa hali ya kutisha. Ni awamu hii imeshuhudia ukatili wa ajabu kwa Maalbino kwa sababu ya ushirikina. Pinda hadi machozi alitoa, lakini mpaka leo wafanya biashara hii haramu hawajakamatwa. Wamekamatwa wauaji tu, ambapo ni dhahiri wamewataja wanunuzi wa viungo vya Albino. Mbona hatuwasikii? Je wanunuzi ndo hao hao wanasiasa? Maana taarifa zinasema kuna wabunge wenye tuhuma hizo, lakini kwa nini hawakamatwi? Je serikali inafaidika nini na ukatili huu? Au ndo makafara ya kuendeshea CCM? Maana , hata Sheikh Yahaya amejinadi kwamba anamlinda Raisi wetu kwa nguvu za ushirikina, CCM haijakanusha. Sasa kama ushirikina unaingia mpaka ikulu, kwanini tusitunge sheria ya kuutambua uchawi kama nyenzo ya kutawala? Kwanini watu Shinyanga wanaua vikongwe kwa tuhuma za uchawi na serikali inakemea? Isikemee basi, maana hata ikulu ina wachawi wanailinda! Mbunge wa CCM, HARRISON Makyembe, ametamka kwamba kuna wauaji walipanga kumuua kwa njia yoyote ile ikiwemo uchawi wa waganga kutoka Songea. Hakuna aliyekanusha. Hivyo, uchawi umeingia rasmi kama nyenzo ya ulinzi na silaha ya maangamizi katika taifa letu. Ah......Mungu tumekukosea nini?


  JAMANI, dhambi hizi hazitaiacha salama CCM. Ni ishara ya alama za Nyakati: CCM is bound to die....and it will die with heavy cost to lives of many Tanzanians. CCM leaders are desparate, they will do anything to survive. Ni wakati muafaka kwa wanaharakati, wananchi kwa ujumla, kulaani hii hali, na kuindoa katika fikra za watawala waliolewa madaraka, kabla hatujaingi kwenye historia za Kossovo, Rwanda na Biafra.
  Tupambane, vita hii ni ngumu.
  Wakatabahu!
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Usikate tamaa endelea kupigania nchi yetu hata kwa kukemea kama unavyofanya popote ulipo waraka huu wasammbazie watu unaweza kuprint ukawapa wananchi ikaw kichocheo cha mjadala
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mawazo yako ni mazuri sana na yanahitaji yawafikie wengi na hasa wahusika wakuu ambao ni wananchi kwa upande mmoja na wale viongozi kw aupande wa pili.. Ni fikra pevu ambazo hazitakiwi kuishia hapa bali kwenda kwa wanaohusika
   
Loading...