GE2025 Devotha Minja: CCM wakiingia Madarakani wanatuletea maisha magumu zaidi, wanatuletea kausha damu

GE2025 Devotha Minja: CCM wakiingia Madarakani wanatuletea maisha magumu zaidi, wanatuletea kausha damu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Mgombea Mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Devotha Minja amesema endapo chama hicho kitapata ridhaa ya kuunda Serikali, mikopo ya asilimia 10 kutoka mapato ya ndani ya halmashauri haitatolewa kwa upendeleo.

Minja amesema hayo Jumapili, Septemba 7, 2025 wakati akiendelea na kampeni katika Jimbo la Bahi mkoani Dodoma.

Amesema sasa ni ngumu kwa wananchi kupata mikopo hii kutokana na urasimu, hali inayochangia wengi kukimbilia mikopo yenye riba kubwa. Mikopo hiyo, inalenga wanawake kwa asilimia nne, vijana (4%), na watu wenye ulemavu (2%).

“Chini ya utawala wa Chaumma, mikopo hii itatolewa kwa wananchi bila riba, kila halmashauri itahakikisha inawawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu,” amesema Devotha.

Pia amekosoa mikopo ya taasisi za fedha akisema inawaumiza Watanzania, na aliiomba jamii kumpa Chaumma ridhaa ya kuleta mfumo wa usawa. Amesema Serikali itakayoundwa itatumia rasilimali za nchi kama madini, utalii na ardhi kuleta maendeleo.

Vilevile, amezungumzia changamoto za maji, ukame na ukosefu wa mbegu bora zinazokabili wananchi wa Bahi

Soma pia GE2025 - Devotha Minja asema CHAUMMA ipo tayari kuungana na CUF kukipumzisha CCM



Chanzo: Mwananchi_official
 
Back
Top Bottom