Devil's Child Follows "Devil's Father" Kikwete is Fisadi No.1 Tanzania. What Next for JK Family? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Devil's Child Follows "Devil's Father" Kikwete is Fisadi No.1 Tanzania. What Next for JK Family?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by niweze, May 1, 2011.

 1. n

  niweze JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama sisi ni Watanzania na Hatuna Hasira na Vitendo Kama Hivi vya Muaji ya Wizi Huu Basi Hakuna Haja ya Kulalamika Hapa Tanzania.

  [​IMG]

  RAIS Jakaya Kikwete anakabiliwa na kashfa nzito kutokana na utajiri wa mtoto wake, Ridhiwani. Sasa anatuhumiwa kuitumia Ikulu kumtajirisha mwanawe, ambaye anasemekana ni bilionea.

  Kwa nyakati mbalimbali, ukwasi wa mtoto huyo wa rais uliibuliwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.

  Katika moja ya mikutano yake ya hadhara hivi karibuni mkoani Tabora, Dk. Slaa alisema Ridhiwani amemaliza shule miaka michache iliyopita, lakini hivi sasa ni tajiri bilionea na kwamba ameupata utajiri huo katika mazingira ya kutatanisha.

  Jana Mtikila alizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Travertine, akidai Ridhiwani amegeuka bilionea kwa muda mfupi “kwa mgongo wa baba yake.”
  Akibainisha zaidi uwezo wa kifedha wa kijana huyo, Mtikila alisema hivi karibuni mtoto huyo ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), aliingiza magari makubwa ya mizigo aina ya “semi trailer” zaidi ya 100 na kudai kuwa yanafanya kazi ya kusomba mizigo DRC na mengine ameyauza.

  Alidai pia mtoto huyo wa rais anamiliki makampuni ya ujenzi wa barabara na maeneo mengi ya ardhi kwa lengo la kujenga maghorofa ya kupangisha.

  “Huyu ni mtoto mdogo, kamaliza shule juzi, pesa za utajiri wote huu kazipata wapi?” alihoji Mtikila.

  Hata hivyo, wiki iliyopita, Ridhiwani alikaririwa na moja ya vyombo vya habari akisema kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano kwa Dk. Slaa kuonyesha kila anachomiliki.

  Kutokana na tuhuma hizo, Mtikila alimtaka Rais Kikwete naye ajivue gamba kwa kuonyesha mfano, vinginevyo ni uendawazimu kujivua gamba bila mkuu huyo wa nchi kujiuzulu urais na uenyekiti wa CCM.

  Huku akionekana kuwatetea Edward Lowassa (Monduli), Andrew Chenge (Bariadi Magharibi) na Rostam Aziz (Igunga), Mtikila alisema Kikwete anawachezea wana CCM na Watanzania kwamba ana nia ya kuwatimua makada hao kwa madai kuwa ni mafisadi wakati yeye ni mshirika wao.

  “Kikwete aanze kutoka yeye ndipo awanyoshee vidole hawa Mapacha Watatu alioshirikiana nao kwenye ufisadi wa EPA, Richmond na Dowans, vinginevyo anawadanganya Watanzania. Aanze yeye,” alisema Mtikila.

  Alisema anashangazwa na Kikwete kuibuka na dhana ya kujivua gamba kwa kuwatosa marafiki zake watatu wakati chama hicho kina mafisadi lukuki.

  Mchungaji Mtikila pia aliorodhesha miradi ya ufisadi aliyomhusisha nayo Kikwete na watendaji wengine serikalini kuwa ni pamoja na IPTL, uuzaji wa iliyokuwa Benki ya NBC, Meremeta, Richmond, Dowans, EPA na nyingine, kwamba zinawahusu watendaji wengi na si mapacha watatu pekee.

  ”Kikwete aliunda tume kubaini waliochota fedha za EPA na kutakiwa warudishe, lakini hadi sasa hatujui kina nani wamehusika, na kiasi gani cha fedha kilichorudishwa. Kama rais hahusiki na ufisadi huu, usiri wa nini?” alihoji Mtikila.

  Alisisitiza kuwa hana maana kuwa Lowassa, Rostam na Chenge ni wasafi, bali anataka orodha ya kuwatimua mafisadi wa CCM iwe kubwa, akiwamo Rais Kikwete kwani ndilo gamba kubwa kuliko yote.

  Kuhusu hatima ya CCM na kile alichokiita usanii wa kujivua gamba, Mchungaji Mtikila alisema chama hicho kina ugonjwa wa ‘Nambulila’ ambao mgonjwa hufa na kuzikwa akijiona.

  “Wapangwa wana ugonjwa unaitwa Nambulila. Ni ugonjwa unaotokana na tego la mke. Mtu akitembea na mke wa mtu anaupata na anapokufa, anawaona watu wanavyomlilia, wanavyomuingiza kwenye kaburi, lakini hana uwezo wa kusema, hivyo anazikwa akiwa hai, akiona kila kitu. Ndivyo ilivyo CCM, inakufa ikijiona. Hii ndiyo Nambulila,” alisema Mtikila.

  Alisema usanii wa kujivua gamba hauwezi kuinusuru CCM kwani ni dhana ya uendawazimu yenye lengo la kuwaghilibu Watanzania.

  Sambamba na hilo, Mtikila aliwataja mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye, Joseph Warioba na Cleopa Msuya, kuwa ni miongoni mwa watu wachache wasafi ndani ya CCM.

  Alipobanwa kueleza usafi wa Sumaye wakati miaka sita iliyopita alipata kumtaja kwamba ni fisadi namba moja, Mtikila alikiri kutoa kauli hiyo na kuongeza kwamba baada ya kufuatilia walibaini kashfa dhidi yake zilikuwa za uongo na zilipikwa ili kumrahisishia Kikwete njia ya kuwa rais.

  “Kweli niliwahi kumtaja kama fisadi namba moja, tulipofuatilia tulibaini kwamba haikuwa sahihi na ndiyo maana leo namtaja kama mmoja ya viongozi wachache wasafi,” alisema.

  Aliwataka wana CCM kutobeza ushauri wa viongozi hao wachache wasafi na kutolea mfano wa Warioba na Sumaye walivyoshambuliwa na UVCCM walipotoa mawazo yao.
  Utajiri wa Ridhiwani wamweka pabaya JK

  Kikwete na Mafisadi wanachokifanya ni kuwapa watoto wao sasa ili Kuendelea kuwalinda na kuvuna resources za Taifa. Kilichompa utajiri Ridhiwani ni nini? Amepata wapi uwezo wa kujenga na kuishi maisha ya kifahari wakati Watanzania hawana umeme, maji, chakula, fedha za kusomesha na huduma. Kitu ni kimoja tu, SISI WATANZANIA TUKICHOKA KUONEWA TUTAFANYA MAAMUZI YA KUWAONDOA KWA NGUVU NA KUNYANGANYA HUO UTAJIRI, Untili now lets educate everyone their rights first.

  Swali ni Hili kama Mtanzania atua gani unachukua kuhakikisha these kinds of families are stopped? Hatuwezi kunendelea kuishi kama Waonewaji Siku Zote - Cycle of Violations Must be Stopped.
   
 2. n

  niweze JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Alipata wapi fedha kujenga hii nyumba. What's sources of income Ridhwani? Tupe paper trail na ushahidi wako.

  [​IMG]

  Thats why katiba mpya ni muhimu kila raisi na viongozi wa serikali wakiingia, wanatumia ofisi ya raisi na mamlaka yake, BOT, treasure na idara zingine za serikali kuwaibia watanzania. Katiba ya Watanzania tu ndio solution hapa Tanzania.
   
 3. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2015
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,139
  Likes Received: 3,328
  Trophy Points: 280
  fisadi rizi ameshaiba vya kutosha na mshua wake wanasubili muda uishe tu waendelee kutusua vizuri
   
 4. WILLAFRICA

  WILLAFRICA JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2015
  Joined: Nov 12, 2013
  Messages: 4,034
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hakika huu ni wizi wa hatari tena unatisha!
   
 5. yomboo

  yomboo JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2015
  Joined: May 9, 2015
  Messages: 4,268
  Likes Received: 2,316
  Trophy Points: 280
  Wabongo wengi ni mang'ombe so mabadiliko yataletwa na sisi wenyewe tuki amua kubadilika
   
 6. E

  Escrowseal1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2015
  Joined: Dec 17, 2014
  Messages: 869
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 60
  Watanzania viumbe adimu duniani. Sasa mlijua na bado mkagawia ubunge. Basi kaeni kimya mliwe vizuri.
   
 7. bmbalamwezi

  bmbalamwezi JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2015
  Joined: Mar 12, 2015
  Messages: 788
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Acheni maneno ya vijiweni yasiyo na mashiko. Hivi utamsikilizaje mtu kama Mzee Mtikila ambaye ni kigeugeu. Leo anasema hili kesho anakana kama alivyothibitisha mwenyewe hapa kweny forum. Shida yenu watanzania wengi mmegubikwa na umaskini hata mkiona mtu kanunua kigari kama vitz mnasema ni fisadi. Huu ni umaskini wa fikra. Mh. Ridhiwan kawekeza ninnyi kwa wivu wenu mnamwita fisadi. Mlitaka awe omba omba. Wewe mwenyewe na kajumba kako ambako hakajakamilika unaitwa fisadi kwa kuwa waliokuzunguka ni maskini. Acha hizo jitume mfanye kazi na muwekeze badala ya kusemasema watu.
   
 8. bmbalamwezi

  bmbalamwezi JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2015
  Joined: Mar 12, 2015
  Messages: 788
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Hii mbona ni nyumba ya kawaida tu ambayo mtu yeyote makini anaweza kujenga. Tatizo wengi mmezoea kukaa kwenye nyumba kama vichuguu, kwenye tembe za shemeji zangu mikoa ya kati. Hivyo mkiona nyumba ya bati na tofali za sementi mnapagawa. Kuwaeni na mawzo chanya mtoke kwenye roho za kichawi zisizo za kimaendeleo. Mbona Ndesa na Mbowaa ni matajiri lakini kwao hamchongi!
   
 9. bmbalamwezi

  bmbalamwezi JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2015
  Joined: Mar 12, 2015
  Messages: 788
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Wewe ndiwe mwizi kwa kuwa kila saa unatamani kuwaibia matajiri ili utoke unashindwa. Kama ni wezi hao unaowatuhumu mahakam zimefungwa? Wapeleke mahakamani. Watanzania mbona mmeugua ugonjwa wa kulalamika badala ya kufanya kazi. Achaneni na kulalamikalia disease
   
 10. bmbalamwezi

  bmbalamwezi JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2015
  Joined: Mar 12, 2015
  Messages: 788
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Kama wengi ni mang'ombe wewe ni fisi au nguruwe? Naona unastahili kupelekwa Milembe ukapimwe akili kabla hujachangia tena kwenye forum. Haya safari njema ukakuta e na wanochukua fomu watakuongezea nauli ya kurudia ukishapona.
   
 11. bmbalamwezi

  bmbalamwezi JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2015
  Joined: Mar 12, 2015
  Messages: 788
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Nenda kafanyiwe maombi inaonekana umechukuliwa ufahamu. Bahati yako kidogo tu hujawa msukule
   
 12. Senior Boss

  Senior Boss JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2015
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 3,285
  Likes Received: 2,025
  Trophy Points: 280
  Cyber Crime Law itavuna wengi humu....nimebana pembeni kimya naangalia tu. Lol
   
 13. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2015
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,294
  Likes Received: 8,393
  Trophy Points: 280
  mada ni ya 1st May 2011.sina hakika kama cyber crime law iliyopitishwa mwaka 2015 inaweza kuwa applicable hapo,ila kama ni hivyo,basi wale wote tulio waudhi wakuu wa nchi hii kwa kuwajadili vibaya mtandaoni siku za nyuma,tutasalimika.hakika itatuvuna wengi. :glasses-nerdy:
   
 14. Senior Boss

  Senior Boss JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2015
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 3,285
  Likes Received: 2,025
  Trophy Points: 280
  Nafaham im just being playful here Joh. I'm not into politics btw. Tehe
   
 15. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2015
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
  Napita tu
   
Loading...