Developer Account Azam Pay

Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
14,007
13,799
Habari na poleni na majukumu wanajukwaa,
Hivi karibuni nimekuwa nikijihusisha na kutengeneza web applications zinazojumuisha maswala ya malipo. Kwa kipindi hicho chote, nilikuwa natumia APIs za Stripe. Kama mnavyojua, Stripe ni ya nchi za magharibi hivyo ukiwa nchi zetu hizi mara nyingi utaweza kuitumia upande wa test mode tu na si upande wa production labda kama una biashara nchi hizo.
Basi nikapata wazo la kutumia azam pay ili nicheze na APIs zao kwenye test mode. Kweli nikaona wanatoa hiyo huduma. Ila shida inaanza wakati wa kujisajili sasa. Nimejaza taarifa zote kwa usahihi ila napewa error. Error yenyewe ni ile ya console sio ile ambayo inafaa umrudishie client ajue nini kakosea; "cannot read properties of undefined".
Kujisajili na kuexplore Stripe kama unajua unachokifanya basi haichukui zaidi ya dakika 15. Nilitegemea azam pay iwe hivyo kwa sababu kwanza ni dedicated payment gateway. Hivyo hawana makando kando mengine ambayo unaweza sema yanaweza waongezea traffic kwenye server zao. Kingine nina uhakika traffic yao si kubwa maana imebase Afrika Mashariki na ukizingatia ukanda huu ndo tunaanza kuamka upande wa online payment. Ni tofauti na Stripe ambayo inaoperate ile zone yote ya juu. Hivyo nilitegemea mambo yawe fasta upande wa Azam Pay kama kweli wanatarajia kuteka soko huku kwetu.
Nitajaribu tena kwa mara nyingine baadaye sana huku nikiendelea kutafuta mbadala. Ila kusema kweli it's disappointing.
 

Attachments

  • Screenshot 2024-03-04 100103.png
    Screenshot 2024-03-04 100103.png
    4.4 KB · Views: 3
Back
Top Bottom