Desturi za wasukuma

  • Mwanamke akimletea maji ya kunywa mwanaume atapiga goti kwa heshima mpaka amalize kunywa
  • Zamani walikuwa na utamaduni wa kutoa mahari na kuoa mimba. Akizaliwa wa kike atakuwa mke, akiwa wa kiume atakuwa rafiki.
  • Rangi ya mwanamke na shape ndio zinatoa thamani ya mahari. Mwanamke mweupe ni kama lulu usukumani mahari yake inakuwa kubwa sana (ng'ombe wengi). Akiwa na mwili wanaamini atakuwa na uzao mwingi (watoto wengi). Familia zinaona fahari wakipokea mahari kubwa( ng'ombe wengi)
  • Utajiri unahesabiwa kwa idadi ya ng'ombe na ukubwa wa familia (wake na watoto). Mtu anaweza kuwa na ngo'mbe 5,000 lakini analalia ngozi ya ng'ombe badala ya godoro.
 
Wasukuma ni wakarimu sana hasa wa maeneo ya shinyanga, sio wachoyo wa chakula. Ukifanya nao kazi wakati wa mavuno watakuletea zawadi kama viazi,maziwa karanga za kutosha.
 
Ugali ni chakula cha bei rahisi sana, labda ungesema nyama, kuku na samaki havina bajeti wala kupima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…