Destructive mentality inavyozidi kuharibu ubinadamu

Destructive mentality inavyozidi kuharibu ubinadamu

streat Anthem

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
395
Reaction score
476
Ni mara nyingi jamii zetu zimekuwa zikiishi katika mifumo ambayo inazorotesha utu na ubinadamu na kufanya maisha yawe ya kinyama.
Jambo la kushangaza ni kuwa watu hawana habari na mabadiliko haya na cha kushangaza zaidi hujikuta wakifurahia,kuumizwa na kushangazwa na mifumo hiyo!
Mifumo hiyo imepelekea kutengenezwa kwa destructive mentality kwenye kila nyanja ya maisha ya mwanadamu.
Mfano unaweza kuta mvulana au mwanamume anasema "nilishamla huyu demu" au mwingine akimuona msichana anapita atamwambia mwenzake "huyu demu lazima nimle" yaani tunawaza kuwala binadamu wenzetu!
Mbaya zaidi tumetengeneza destructive mentality kiasi kwamba ukimuona msichana utatamani umle tu alafu umuache kiasi kwamba hujali utu wake wala hisia zake.
Hata wasichana/ wanawake nao wametawaliwa na hii destructive mentality kiasi kwamba pale unapomtongoza yeye atachokiwaza nikukudestroy either financially or emotionally.
Ukimuita msichana/mwanamke hata kwa lengo la kumuulizia tu, kitakacho click kwenye mind yake ni "kuliwa tu" hivyo atajitahidi ajidefend kivyovyote.

Destructive mentality ipo mashuleni, maofisini mfano ukimuona mwenzako anachapa kazi vizuri utataka umfanyie fitna, umuletee zengwe au kumkaisha tamaa ili kuharibu kabisa ufanisi wake.
Hata kwenye biblia watoto wa Yakobo walimuuza ndugu yao Yusufu baada ya kutawaliwa na hii destructive mentality.

Msanii au mwanasiasa anaweza kuamua kumutungia au kumsemea vibaya mwenzake ili tu haonekane hafai mbele za watu rejea Dudubaya (konki)

Ukiachana na msichana utafanya uwezalo kumharibia hata kuposti picha zake za faragha.

Siku hizi kabinti kakianza kupendeza/kunawili mababa mazima yataanza kukanyemelea na kumhadaa ili "yamle" bila kujali kuwa binti huyo anahitaji muongozo ili afikie malengo yake.

Inasikitisha na kuhuzunisha sana pale tunapokimbilia zaidi kwenye unyama na kuuacha utu ambao ndio msingi mzuri wa maisha. Tujitahidi kutengeneza creative mentality hasa kwa kuthamini wengine,kuwapenda wenzetu na kuwasamehe wengine hasa pale wanapotukosea.
 
Back
Top Bottom