Hakuna kejeli hapo wala dharau labda uwe hujapitia maoni mengine ya wadau. Posts kama zile za kibiashara lazima watu watakuwa na maswali au kutaka kuwasiliana na mtoa mada. Sasa ukiingalia post ile na kusoma maoni ya wachangiaji utaona wengi walikuwa na hamu ya kujua bei, walipo wenye biashara, aina nyingine ya bidhaa, nk. Lakini hakukuwa na majibu na wengi wakawa wanashangaa inakuwaje unatoa mada ya kibiashara halafu unapotea wakati wateja wanakiu ya bidhaa yako. Hivyo mimi kudhani kuwa inawezekana mtoa mada kakopi mahali lakini siye mjenzi au mwqenye biashara. Kama unajua kiswahili vizuri utaona nimeanza na neno "Inawezekana" kwahiyo sikusema wamekoipi kwa asilimia 100. Hiyo pia ilikuwa mbinu ya kuchochea mtoa mada ili arudi kujibu maswali. Ningeandika kwa kiingereza ningesema "May be.."Acha kejeli, sio vizuri na si busara unavyofanya.
Hakuna kejeli hapo wala dharau labda uwe hujapitia maoni mengine ya wadau. Posts kama zile za kibiashara lazima watu watakuwa na maswali au kutaka kuwasiliana na mtoa mada. Sasa ukiingalia post ile na kusoma maoni ya wachangiaji utaona wengi walikuwa na hamu ya kujua bei, walipo wenye biashara, aina nyingine ya bidhaa, nk. Lakini hakukuwa na majibu na wengi wakawa wanashangaa inakuwaje unatoa mada ya kibiashara halafu unapotea wakati wateja wanakiu ya bidhaa yako. Hivyo mimi kudhani kuwa inawezekana mtoa mada kakopi mahali lakini siye mjenzi au mwqenye biashara. Kama unajua kiswahili vizuri utaona nimeanza na neno "Inawezekana" kwahiyo sikusema wamekoipi kwa asilimia 100. Hiyo pia ilikuwa mbinu ya kuchochea mtoa mada ili arudi kujibu maswali. Ningeandika kwa kiingereza ningesema "May be.."
Alifanya hivyo baadaye lakini mwanzoni hakutoa chochote ndiyo maana wattu wakawa wanamtafuta na huenda alirudi baada ya watu kulalamika sana, Kumbuka nami nilikuwa namjibu mdau aliyekuwa anatafuta majibu kutoka kwa mtoa mada. Ukisoma maoni ya wachangiaji wa mwanzo utaona jinsi walivyokuwa wanahangaika. Na mimi nikasema :Inawezekana" neno hilo halina maana ya kuwa nilivyosema ndivyo ilivyo nami nikiwa natafuta mtoa mada. Kwa kiingereza ningesema "May be..." Hivyo sikuwa na nia ya kumkatisha tamaa ndio maana hoja yangun huenda ilichangia kumleta mtoa mada na kuanza kujibu maswali. Kuna watu ambao hutoa mada na kupotea hasa zile za kibiashara hivyo wanaporudi wanakuta wateja wamehangaika sana kupata majibu ambapo wakati mwingine wateja wenyewe huanza kutoa majibu wakati mwingine yakiwa siyo sahihi hii ni kwasababu ya mtoa mada kupotea kwa muda.Mbona namba ya simu kaweka? Na anajibu maswali ya watu? Acheni tabia ya kuwakatisha tamaa watu, ukiwa serious humuulizi maswali hapa utampigia.
Unawaambia wewe ni Dr. Preta, mwanachama maarufu wa JF na bilionea wa Yaeda chini
Mkuu. Nini maana ya kirefu cha BOQ ?.
Asante kwa maelezo yako ila usikimbie jukwaa , please endelea kujibu maswali ya raia.
Kwa ujenzi wa kawaida na ule unaofuata taratibu za mipango miji, njoo ujipatie ramani za vyumba 2, 3, 4. Mfano hiyo chini hapo ni ya vyumba viwili Ina mita 8 kwa 11 haina corido ubunifu mpya wa sasa.
Ndani kuna master, chumba kimoja kawaida, choo public, stoo, jiko, sebule na dining. Ujenzi substracture tofali 1206 size 230 mm na superstructure tofali 1758 size 150 mm kuezeka ni bati 38 tu.
Hapo mengi zaidi, join whatsapp group
Call or Whatsapp: +255787459850
Duh, bati 38? bati gani mkuu?
Unajitahidi sana kubuni mkuu, ramani zako naona ziko original na zinavutia.
Kajumba ka vyumba vitatu, kadogodogo lakini master iwe pana kidogo, pia madirisha huwa napenda narrow windows, kuna nyumba moja niliwahi kuona, madirisha yalikuwa narrow kiasi kwamba ukubwa wa dirisha kubwa umegewanya na kuwa vidirisha vitatu vidogovidogo virefu ilinivutia sana, hauna mfano wowote wa namna hiyo mkuu? Na je gharama zako zikoje kwa mchoro wa vyumba vitatu?
Mkuu. Nini maana ya kirefu cha BOQ ?.
Asante kwa maelezo yako ila usikimbie jukwaa , please endelea kujibu maswali ya raia.
Hii Ramani tafadhali atupie Floor plan yake. Ili tuweze kuona plan yake. Tusiishie tu kuisifia ni Nzuri bila ya Kuona FloorPlan yake.
Usihuzunike kwani ukiamini utajenga utajenga tu kikubwa ni kuthubutu, unajua nyumba inajengwa kwa hatua na wala usifikirie kuzichanga mpaka zifike 20 milion, hatua ya kwanza ni kuzichanga unanunua kiwanja kinakuwa pending tu sehemu alafu hatua ya pili unakusanya materials angalau ya msingi, amini usiamini ukiweza kupiga msingi na ukawa una kipato chako mdogo mdogo unamaliza na huwezi amini.
Tatizo wengi linapokuja suala la kujenga anataka kununua kiwanja na kuanza kujenga matokeo yake hela hazitoshi na kila ukipata hela zinaingia kwenye matumizi mengine lakini kwa mtu mwenye kiwanja unakuta akipata laki 2 au 3 nusu anaweza akaitumia kwa mambo yake na nusu akatupa hata tripu mbili za mchanga site kwa kuwa ana sehemu ya kuweka huo mchanga lakini ukiwa huna kiwanja lazima kama binadamu utazitumia tu kwa mambo mengine maana hazitoshi kununua kiwanja na wewe huna kiwanja