Dereva wa Pikipiki Atekwa na kuchinjwa Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dereva wa Pikipiki Atekwa na kuchinjwa Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuji, Feb 9, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Feb 9, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KIJANA mmoja anayejishughulisha na kubeba abiria kupitia usafiri wa pikipiki ametekwa na kuuawa.

  Kijana huyo anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 20 hadi 22 ameuawa kwa kuchinjwa na abiria ambao aliwabeba kuwapeleka sehemu husika.

  Tukio hilo limetokea maeneo ya Kimara Golani.

  Kijana huyo ambaye jina lake kamili halikuweza kupatikana mara moja anayejulikana kama “Chinga” alikodishwa na watu wawili awapeleke huko Kimara Golani.

  Inasemekana kuwa wakati wako njiani akiwapeleka wateja wake hao ndipo walipomtaka ashuke na wao waondoke na pikipiki hiyo.

  Taarifa zilizomfikia mwandishi wa Nifahamishe, zilisema kuwa kijana huyo alipotakiwa aachie pikipiki hiyo alikuwa anasita kuachia mali yake hiyo, na ndipo walipotoa shoka na kumpiga nayo sehemu za kichwa na kufariki papohapo.

  Baada ya kuona kijana huyo amefariki dunia wezi hao ambao walikuwa ni abiria waliondoka na pikipiki hiyo na kumuacha kijana huyo mahali hapo.

  Source: http://www.nifahamishe.com
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huku mafisadi wanafuja fedha ambazo zingetumika katika kutoa huduma (afya, elimu, maji nk), Albino wanawindwa na kuuawa, vikongwe wanauliwa, majambazi nayo yanaua (kama huyu waliyemuua), raia wenye hasira wanaua wanaohisiwa kuiba hata Kuku, polisi waliopewa dhamana ya kulinda raia wanaua (Zanziba, Wahanga wa msitu wa Pande). Hili Taifa linaelekea wapi?
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Feb 10, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Taifa linaelekea KUZIMU
   
 4. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Inatia uchungu sana kwa kijana anaejitahidi kujikwamua kimaisha kwa usafiri wa pikibiki bado watu wanatoa roho yake kisa pikipiki tuu. Wizi huu unaashiria kiwango cha umaskini kilichopo nchini kwetu serikari inapaswa kuchukua hatua kuboresha maisha ya watanzania kwa kuhakikisha watu wanafanya kazi.
   
 5. M

  Mkubwa Dawa Member

  #5
  Feb 10, 2009
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi huyo dereva wa pikipiki aliyetekwa kweli hali imezidi kuwa mbaya na taifa limefika njia panda sasa.
   
 6. B

  Babuji Senior Member

  #6
  Feb 10, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hali hii watanzania walio nje lazima waogope kurudi Tanzania
   
 7. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kwani huko nje kuna madogo? Kama ni suala la crimes tena inaweza kuwa bora hapa kwetu!
   
 8. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Siku za mwisho matukio ya uasi yataongezeka, familia zitatengana, ndugu watasambaratika, magonjwa yasiyotibika yatatokea, you name all. Yaani kila wakati unamuona binadamu mwenzio ni hatari. Tutaishi maisha ya kujihami na wasiwasi hadi lini?? Tumrejee Mungu wa rehema.
   
 9. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Jamani waandishi wetu watajifunza lini uandishi? Ni kwanini mtu aandike habari kama alikuwepo vile, na kama alikuwapo eneo a tukio alichukua hatua gani kuokoa maisha ya huyo dereva?

  Na watanzania tutajifunza lini? Pikipiki ni kwa ajili ya dereva na abiria mmoja, inakuwaje mtu anabeba zaidi ya mtu mmoja?

  Somo limetufikia...
   
 10. B

  Babuji Senior Member

  #10
  Feb 10, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nje sawa kuna crimes kibao tu lakini Tanzania kumezidi kwa crimes za ajabu ajabu
  Mtu anauliwa Tanzania kwa mambo ya kuoneana wivu, mambo ya kishirikina na sabau zingine za ajabu.

  Mara kibao tumesikia kwenye vijiji vyetu watu wakivamiwa na kuuliwa au kutishiwa kuuliwa kwasababu ya TV tu

  wewe fikiria mwenyewe utaona Tanzania bado sana mpaka tutoke!
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  :mad:Huyu jamaa tumemzika wenyewe.Mii ninaishi SUKA.ukweli hata mwili wa marehemu hatukuruhusiwa kuuangalia,ninahisi hakukuwa na kichwa.

  Ninachokiangalia katika kizazi hichi ni kupotea kabisa kwa utu.Watu wamekuwa wanyama zaidi.Fikiria kama jambazi anamkaba mtu wa PIKIPIKI........!huyo ni jambazi wa aina gani?na anategemea kupata nini kwa waendesha tukutuku?

  IT IS THE SIGN OF TIMES.....!hizi ni zama na kizazi kingine!
  A VIPER GENERATION!

  Lord bless the dead
   
 12. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...Mkuu BabuJ, una uhakika na kauli yako hii?? Huko nje si ndio tunasikia mwanafunzi anaamka asubuhi na kwenda kuwafyatulia risasi wanafunzi wenzake na kisha na yeye kujimaliza??
  Huku nje si ndio tunasikia mtu anamuua mpenzi wake na kumkatakata na kisha kuweka viungo vyake ndani ya friji huku akikaanga vingine na kuvila???
   
 13. B

  Babuji Senior Member

  #13
  Feb 10, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu Babadesi unajua Tanzania mambo ya media bado hayajakuwa advanced kama nje hivyo nadhani Tanzania kama vituko vyote kama vile vya kuchuna watu ngozi na maalbino na vingenevyo kadhaa vingekuwa vinarushwa kwenye media zetu basi ingekuwa noma
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ningekuwa mimi ndo Kova,
  Namsaka mwandishi wa habari hii as prime suspect...
   
 15. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwa muda wangu wote niliokaa ugaibuni sijawahi sikia wizi wa simu, kuchomolewa pesa mfukoni, kuibiwa walet bali nimekuwa nikistuliwa hallo is this your walet, or your phone. Of cause wizi kwa ujumla sikatai upo lakini polisi wanafanya kazi yao vizuri sana hivyo hata wezi wanalazimia kutumia akili ya ziada na kwa staili hiyo wizi mdogo mdogo si common sana. na inapotokea basi hata alieibiwa alifanya uzembe kidogo kwa kuweka mwanya wa wezi. Bongo hali si swali kabisa, mtu akiwa town hata kupokea simu yake tu issue mpaka aishikilie kwa nguvu zote au ajifiche maana wakwapuaji wanaweza katiza kwa speed ya light na kutaambaa nayo. Pili kumuua mtu kwa sababu ya kuiba baiskeli au pikipiki ni wizi wa kiumaskini sana ambao pia unaonyesha jeshi letu la polisi limelala.
   
Loading...