Dereva wa Lissu: Siku ya shambulio hakukuwa na ulinzi wowote, eneo lile linalindwa na askari wenye bunduki siku zote

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,216
7,908
Hiki kituo cha Radio Free Africa ni cha kihuni mno. Leo saa 7 mchana wamekata matangazo ya DW pindi tu alipoanza kuhojiwa dereva wa Lissu. Huu ni uhuni na uvunjifu wa sheria na haki ya kupata habari.

Nashauri DW wavunje mkataba na hawa jamaa make hii ni hujuma.

=====

Jaribio la mauaji dhidi ya mbunge wa upinzani, Tundu Lissu, lililofanyika Septemba 2017 bado ni mjadala mkubwa Tanzania.

Lissu amekuwa akionekana mara kwa mara akizungumza na vyombo vya habari vya kimataifa, na sasa Deutsche Welle (DW) imekutana na dereva wake Adam Mohamed Bakari akiwa mjini Brussels, Ubelgiji, kujua anachokumbuka kuhusu mashambulizi yenyewe.

Dereva wa Lissu anasema;

=> Tulikuwa tunatoka Bungeni tunaenda nyumbani, ghafla nikaona gari mbili zinatufuata nyuma kwenye gari yangu, mimi nikawa napunguza mwendo kwasababu labda kwanza niliona zina haraka zipite hazikufanya hivyo.
Nikakunja kona ya kwanza hizo gari zipo, nikakunja kona ya pili hizo gari zipo, nikaona hizi gari sio salama kwetu

Nikaongeza mwendo kidogo, lakini mpaka hapo nikawa sijamwambia chochote boss.

Tukafika karibu na nyumbani, kuna club moja inaitwa club 84,kuna gari iliyokuwa inanifuatia mimi ni V8 ikapaki pembeni, ile Nissan iliyokuwa inaifatia gari iliyo nyuma yangu ikaja spidi kunifuata mimi, nilipoingia getini na ile nayo ikaingia getini.

Tulivyo-park gari nao waka-park, walikuwa wamevaa cap na miwani wakawa wanazungumza, ghafla baada ya kuzungumza maongezi ambayo hatukuyajua,lile gari lilirudu reverse kwa spidi na kufika usawa wa gari letu, tukaanza kusikia milio ya bunduki.

Baada ya kusikia mlio wa bunduki paah,nikapiga mlango wangu na nikamvutia boss kuja kwangu, basi baada ya mimi kutoka nje wakawa wanaendelea kumimina risasi, wamepiga risasi nyingi. Mimi nilipokuwa kule nilikuwa nafuatwa na vioo.

Mtangazaji: Kuna tuhuma kwamba wewe unajua kuhusu mashambulizi hayo, unazungumzaje kuhusu hilo?

Dereva: Hayo ni maneno ya watu ambao labda wanajaribu kufikiria imekuwaje tumenusurika mpaka leo hatukufa ndio maana wengine wanadiriki kusema imekuwaje mpaka dereva wake hajapigwa risasi hata moja.

Kwanza ninachoweza kusema, lile tukio wanalijua wao ndio maana hata siku hiyo ukitaka kujua hata kwa akili ya kawaida hakukuwa na ulinzi wowote, pale siku zote kuna ulinzi wa askari wenye bunduki. Siku ile hakukuwa na ulinzi wa aina yoyote.

Na kama mimi ninahusika, mimi sikujificha na tuliwaambia sisi tupo Nairobi kama mnataka kutuhoji njooni Nairobi na waliahidi watakuja hawakutokea. Miezi minne Nairobi tulikaa.
 
Nilihisi watakata kumbe kweli. Nikaamua kusikiliza ABOOD FM kwenye TuneIn.
Rfa ni makocho sana.
Hiki kituo cha Radio Free Africa ni cha kihuni mno. Leo saa 7 mchana wamekata matangazo ya DW pindi tu alipoanza kuhojiwa dereva wa lissu. Huu ni uhuni na uvunjifu wa sheria na haki ya kupata habari. Nashauri DW wavunje mkataba na hawa jamaa make hii ni hujuma.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndio kawaida yao,hawajaanza leo hao,kwani hakuna namna ya kuipata hiyo idhaa moja kwa moja?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki kituo cha Radio Free Africa ni cha kihuni mno. Leo saa 7 mchana wamekata matangazo ya DW pindi tu alipoanza kuhojiwa dereva wa lissu. Huu ni uhuni na uvunjifu wa sheria na haki ya kupata habari. Nashauri DW wavunje mkataba na hawa jamaa make hii ni hujuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usihofu , yote yaliyozungumzwa nitakuwekeeni hapa hapa JF , Diallo kishaambiwa akiendelea kuweka hadharani haya mambo yatamkuta
 
Hiki kituo cha Radio Free Africa ni cha kihuni mno. Leo saa 7 mchana wamekata matangazo ya DW pindi tu alipoanza kuhojiwa dereva wa Lissu. Huu ni uhuni na uvunjifu wa sheria na haki ya kupata habari.

Nashauri DW wavunje mkataba na hawa jamaa make hii ni hujuma.
Hii taarifa ungewa andikia na dw ingekuwa vema ili Kama RFA wanamkataba na dw usitishwe na RFA iendelee kufa zaidi kwa kukosa wadhamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki kituo cha Radio Free Africa ni cha kihuni mno. Leo saa 7 mchana wamekata matangazo ya DW pindi tu alipoanza kuhojiwa dereva wa Lissu. Huu ni uhuni na uvunjifu wa sheria na haki ya kupata habari.

Nashauri DW wavunje mkataba na hawa jamaa make hii ni hujuma.
Kunguru mwoga anapokimbiza bawa lake....!!! Fear of the unknown....!

Jr
 
Back
Top Bottom