Dereva wa Lissu asema hana kumbukumbu vizuri kwa kilichotokea kwenye shambulio dhidi ya Lissu

Lobapula

JF-Expert Member
Jun 19, 2011
2,388
1,582
Dereva wa Lissu ambaye ndiye mtu pekee waliyekuwa wote si ya tukio hilo, Simon Bakari naye alizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu tukio hilo na kudokeza kwamba limevuruga na hana kumbukumbu sahihi.

Dereva huyo ambaye naye anaendelea kupatiwa matibabu ya kisaikolojia katika hospitali hiyo ya Nairobi alisisitiza, “Kwa sasa siwezi kuzungumza vizuri tukio hili kwani nadhani sina kumbukumbu vizuri.”

=======

Nairobi. Kwa mara ya kwanza, Alicia Magabe ambaye ni mke wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia tukio la mumewe kushambuliwa kwa risasi na kudokeza kwamba haliwezi kuwa limetokana na sababu nyingine isipokuwa kazi ambazo amekuwa akizifanya.

Pia amezungumzia kuhusu afya yake na kueleza kuwa bado siyo nzuri na kuwaomba Watanzania waendelee kumuombea.

Mbali ya Alicia ambaye pia ni mwanasheria, dereva wa Lissu naye amezungumza akisema ameathiriwa kwa kiasi kikubwa na tukio hilo huku akiahidi kuripoti polisi mara baada ya kurejea nchini.

Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), amelazwa katika Hospitali ya Nairobi tangu alipopelekwa huko baada ya kupigwa risasi akiwa ndani ya gari nje ya nyumba yake mjini Dodoma mchana wa Septemba 7 akitokea bungeni.

“Watanzania wote wanajua Lissu maisha yake yote amekuwa ni mtetezi wa wanyonge na tukio hili amelipata kutokana na kazi zake hizo hivyo nawaomba tumuombee tu,” alisema.

“Ninachoweza kusema hali ya mheshimiwa Lissu sio nzuri ingawa ni tofauti na tulivyomleta hapa, hivyo naomba Watanzania kuendelea kumuombea.”

Aliwashukuru Watanzania kwa michango, na maombi yao kwa Lissu akisema hiyo inaonyesha ni jinsi gani wanathamini mchango wake kwa jamii.

Alipoulizwa kuhusu kauli ya Serikali kwamba ipo tayari kugharimia matibabu ya Lissu popote ikiwa itaombwa na familia hiyo, Alicia ambaye pia ni wakili alisema kwa sasa hana maoni.

“Katika hili no comment (sina maoni) ndio tumesikia jana amezungumza na kwa kuwa jambo hili siyo la uamuzi wa mtu mmoja, mimi sina cha kusema,” alisema.

Hata hivyo, alisema anashukuru kazi kubwa ambayo inafanywa na madaktari wa Hospitali ya Nairobi na kusema wanaridhishwa na matibabu ambayo anapatiwa kwa sasa.

Dereva wa Lissu azungumza

Mbali ya Alicia, dereva wa Lissu ambaye ndiye mtu pekee waliyekuwa wote si ya tukio hilo, Simon Bakari naye alizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu tukio hilo na kudokeza kwamba limevuruga na hana kumbukumbu sahihi.

Dereva huyo ambaye naye anaendelea kupatiwa matibabu ya kisaikolojia katika hospitali hiyo ya Nairobi alisisitiza, “Kwa sasa siwezi kuzungumza vizuri tukio hili kwani nadhani sina kumbukumbu vizuri.”

Alipoulizwa kuhusu wito wa polisi wa kwenda kutoa maelezo, alisema atafanya hivyo pindi atakaporejea nchini baada ya matibabu.

“Nilisikia polisi wamenitaka nikatoe maelezo lakini sijisikii vizuri na bado napata matibabu. Nitakwenda,” alisema.

CHANZO GAZETI LA MWANANCHI
 
Nataman mbowe amrudishe leo hii !mie toka anapata majanga TL nilisem kbs dreva anajua !UNAjua ht km umeishi naye miak 40 huenda kapewa pesa nyingi !afu ukute huyu akap[potea tu nasisis tukasahau! ccm huenda ikampoteza au ikampeleka mbali tusijue ! MUNGU hadhihakiwi lakini
 
Ila watu tunapenda kulishwa maneno sana, kwani nani alitoa maelezo mengi ya namna tukio lilivyokuwa na hata kutaja namba ya gari lililotumika, aina ya bunduki na njemba Mwenye kapero miwani tinted?

Hapa tuwe makini jamani, kuna watu wanaona akili zetu zinaweza kuchezewa kwa watakavyo ili turaruane wenyewe!
 
Pitia hii link kutoka kwenye gazeti la Mwananchi usome swali aliloulizwa na majibu yake yan leo eti hana kumbukumbu vizur?Hayo matibabu anayopata ndio yanafanya aanze kupoteza kumbukumbu mbona mwanzo alisimlia tukio zima

Mke wa Lissu avunja ukimya
 
nataman mbowe amrudishe leo hii !mie toka anapata majanga TL nilisem kbs dreva anajua !UNAjua ht km umeishi naye miak 40 huenda kapewa pesa nyingi !afu ukute huyu akap[potea tu nasisis tukasahau! ccm huenda ikampoteza au ikampeleka mbali tusijue ! MUNGU hadhihakiwi lakini
Huyo kafunzwa hapo tena na mawakili wa Nje ya nchi.
Kwasbb amechukua zile action kama.za nchi za watu.kua anahaki asemalo..
NDIO MAANA TULITANGULIZIWA KUA ANATIBIWA KISAIKOLOJIA...
UKISHAJUA MAANA YA SAIKOLOJIA TU.
JIBU LINAKUJA HAKUNA KUMBUKUMBU
 
Kwani CCM ndo wamemficha huko Naii?Halafu unaendeshwaje na ndugu yako wakati hana vigezo utegemee kuwa salama.
 
Pitia hii link kutoka kwenye gazeti la Mwananchi usome swali aliloulizwa na majibu yake yan leo eti hana kumbukumbu vizur?Hayo matibabu anayopata ndio yanafanya aanze kupoteza kumbukumbu mbona mwanzo alisimlia tukio zima

Mke wa Lissu avunja ukimya
Hivi wameenda kumtibu kisaikolojia au wameenda kumwekea sumu ya kupoteza kumbukumbu?I smell a Rotten rat somewhere
 
Huyo kafunzwa hapo tena na mawakili wa Nje ya nchi.
Kwasbb amechukua zile action kama.za nchi za watu.kua anahaki asemalo..
NDIO MAANA TULITANGULIZIWA KUA ANATIBIWA KISAIKOLOJIA...
UKISHAJUA MAANA YA SAIKOLOJIA TU.
JIBU LINAKUJA HAKUNA KUMBUKUMBU
Halafu mbona gharama za matibabu yake hazijawekwa hadharani? Au anatibiwa bure?

Kuna mchezo tunafanyiwa, wasituvuruge tafadhali, bora wanyamaze kimya mpaka mpendwa wetu aje kueleza mwenyewe!
 
Paso ya kisogo chenga ya mwili, tuasdume hayupo ila walinzi walimuona action zake , hizo nyumba haishi mtu akatoa ushahidi wakati wa tukio alibehave vipi, CCTV hakuna, kuanzia bungeni alipomchukua behavior ilikiwaje. Hata intern wa security anaweza kuandika Japp preliminary artchitectutre
 
Halafu mbona gharama za matibabu yake hazijawekwa hadharani? Au anatibiwa bure?

Kuna mchezo tunafanyiwa, wasituvuruge tafadhali, bora wanyamaze kimya mpaka mpendwa wetu aje kueleza mwenyewe!
Kabla hajaanza kupata hayo matibabu alikua na kumukumbu sawa na akaelezea tukio vyema lakini sku 14 tangu kaanza kupata matibabu kumbukumbu zimeanza kupotea hahaaaa sisi sio majuha
 
Halafu mbona gharama za matibabu yake hazijawekwa hadharani? Au anatibiwa bure?

Kuna mchezo tunafanyiwa, wasituvuruge tafadhali, bora wanyamaze kimya mpaka mpendwa wetu aje kueleza mwenyewe!
Mkuu kitaeleweka tu..NA ukitaka kujua hii serikali ni Mafia,,imenyamaza kimyaaaaa,,!!!!wala hawajapapatika.
Lkn Ingekua huyu NDIO angekua upande wa serikali,CDM ingeitisha Press Conference hadi Brazil.Wabunge ndio wangegeuza ni Dili haasa ya kuliongelea majukwaani na ktk Medias
 
Back
Top Bottom