Dereva wa Dr. Mwakyembe anatakiwa RUMANDE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dereva wa Dr. Mwakyembe anatakiwa RUMANDE

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kandambilimbili, May 25, 2009.

 1. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #1
  May 25, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Haya endeleeni kuchangia, tume imeundwa wataalam wamechunguza na imeoneka dereva wa Dr. Mwakyembe alikuwa na makosa, aliendesha gari kwa speed anatakiwa apelekwe akajibu mashitaka. MIMI NILIJIULIZA SANA INAKUWAJE UGONGWE KWA NYUMA NA GARI AMBALO MWENDO WAKE NI MDOGO KILINGANISHA NA LA KWAKO? Haya siju huyu dereva katumwa na mafisadi?????
   
 2. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mtaalam wa kutoa maelezo ya ajali hapa JF ni mwanakijiji,huwa anajua kuunganisha vitu na mara zote amekuwa akitupa msaada sana

  Mie sheria hizi huwa sijui,Mwanakijiji kwa uzoefu ule ule na maneno uliyowahi kutumia wakati Mama mbatoia anapata ajali,wangwe..

  ILi haujalipa nafasi sana,ebu tuambie makosa ni ya nani?Ka nzi kako kana habari gani?
   
 3. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2009
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Acha uzushi. Kama dereva wa Mwakyembe ni mzembe, si dereva wa lori angesimama. Yuko wapi?
   
 4. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #4
  May 25, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wewe subiri habari alizoleta Mwanakijiji wako au nenda kabisa kwa mwanakijiji forums au PM kwa invisible, lakini HABARI NDIO HIYO.....


  MZUSHI ni wewe kwani mimi nilikuwa kwenye hiyo TUME, we mwanjelwa kweli......
   
 5. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #5
  May 25, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Yule dereva akiulizwa jambo gani limetokea,lazima atatafuta kitu au mtu wa kumsingizia,hawezi kusema yeye ana makosa.
  Kama kulikuwa na gari mbele kwa nnini amefanya overtake? Yule dereva mwenye lori labda alikuwa hataki apite kwa sababu kule mbele alikuwa ameliona gari linakuja.
  Na kama kuna watu wana njama ya kumdhuru Mwakyembe hao watu ni akina nani? Ni wale wa Richmond,au watu wa CCM ambao alikuwa amebishana nao huko Mbeya. Kwa sababu lile sakata la wana ccm kupigana Mbeya lilikuwa linamhusu Mwakyembe.
  Kwa hiyo ni juu ya Polisi kutafuta kujua kati ya mbivu na mbichi,kati ya pumba na mchele,ili Watanzania wasipoteze muda kubishana.
   
 6. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #6
  May 25, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ukiacha ubinadamu, kuna sababu gani ya DEREVA wa Lori kusimama kama kweli hakuhusika na ajali hiyo?
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Dereva hana kosa la moja kwa moja....pia Dr nae anajua udereva na alikuwa anafuatilia mwendo wa gari lake hadi lina overtake...ni bahati mbaya tu.....ila Dr aache kusafiri usiku nasikia anasafiri sana usiku sijui ingekuwaje ingekuwa uck
   
 8. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #8
  May 25, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huwa wanalala usingizi hao kapewa story na dreva wake.... ila kama ni kweli yuko makini, katika hali ya kawaida uone ajali inakaribia alafu ukaze macho kwenye speed meter na rpm na sio kwenye ajali inahitaji akili za ajabu.
   
 9. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Si lolote ni ajali tu kama ajali nyingine,Dr.aache kumtetea dereva wake mzembe!!Tena ninamkanda alipojitetea alionyesha alikuwa mbio sana.Hata alipopoteza control akasingizia aligongwa kwa nyuma.Sikubaliani kabisa na dhana ya kusema kulikuwa na nia mbaya katika ajali hiyo ya Mwakyembe.Tatizo hapa ni kuwa akili za mashabiki wengi wa Mwakyembe wanahisi kuwa yuko hatarini akiwindwa kila akiingia na kutoka, hata akianguka kitandani kwake watasema kuna mkono wa mtu.Jamani tuondokane na dhamira hizo kilajambo huja kwa wakati wake na kwa namna yake.Kilamtunchi hiiakifa auakipata ajali basi nyumayake kuna mbaya wake?Hebu tufikirie jinsi madereva wetu walivyo mbumbumbu barabarani,tufikirie kuwawekea vyuo maalium vya kuwafunza waache ubabaishaji.Vinginevyo kelele za ajali za kizembe hazitakoma kabisa.Dreva wa Dr.Harisson Mwakyembe anakabiliwa na mashtaka yasiyopungua matatu.Nitashangaa sana kama hatafikishwa mahakamani,Kama hakufikishwa basi kamanda wa kikosicha usalama barabarani wa Mkoa wa Iringa achunguzwe na PCCCB na afikishwe mahakamani mara moja,
   
 10. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mwakyembe na Dereva wake wanadai kuwa waligongwa kwa nyuma na (walichomekea) baada ya kuona gari mbele yao. Kwa hiyo wao ndo wamegongwa kama wanavyodai wote vinginevyo polisi watuambie kuwa si kweli hawakugongwa bali wamepinduka tu.
   
 11. F

  Fataki Senior Member

  #11
  May 26, 2009
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  YAPO MASWALI MENGI YA KUJIULIZA KUHUSU SUALA HILI AMBAYO POLISI YA TANZANIA LAZIMA IYAJIBU:
  (1) Kwa nini, immediately after the accident na kabla hata ya kuwahoji dereva wa Mwakyembe, dereva wa lori na Mheshimiwa Mwakyembe mwenyewe, RPC wa Iringa Bw. Advocate Nyombi alikuja na kauli ya kufunga upelelezi kuwa " tumethibitisha kuwa hakukuwa na njama yoyote katika ajali hii. Tumegundua kuwa chanzo cha ajali ni gari la mbunge kuingia kwenye shimo barabarani". (Angalia gazeti la The Citizen tar.22 Mei, 2009) RPC alikuwa anakimbilia wapi kutoa tamko hilo kabla ya upelelezi kukamilika? RPC alikuwa anataka kuficha kitu gani? Nani alimwambia kuwa kulikuwa na njama?
  (2) Kwa kuwa Meneja wa TANROADS, Iringa, amekanusha taarifa ya RPC kwa kusema shimo (pothole) lililopo sehemu hiyo ni la cm 2 ambalo haliwezi kusababisha gari aina ya Landcruiser VX na mataili yake makubwa kupoteza njia na kupinduka, Polisi wanasemaje?
  (3) Mashahidi wakuu katika kesi hii ni Mwakyembe na dereva wake, kwa nini ushahidi wao wa kwamba waligongwa na semi-trailor haufuatiliwi na Polisi? Polisi wanaogopa nini kuufuatilia ushahidi huo? Au lori hilo ni lao?
  (4) Dereva wa lori hilo ameibuka kukana kuligonga gari la Mbunge Mwakyembe kupitia gazeti la Tanzania Daima. Ni nini kinawazuia Polisi wa Tanzania kumpata dereva huyo kupitia kwa mwandishi wa Tanzania Daima?
  (5) Dereva huyo wa lori anadai (kama hatudanganywi na Tanzania Daima) kuwa aliliona gari la Mbunge likipinduka mbele yake lakini hakusimama. Je, Polisi wa Tanzania hawajui kuwa dereva huyo alikuwa na wajibu kisheria kuwasaidia waliopata ajali? Mbali na hoja hiyo ya kisheria, kupitiliza bila kusimama kunajenga hoja ya guilty consciousness upande wa dereva wa lori!
  (6) Amri ya kumkamata dereva wa Mwakyembe na kumshitaki, ita achieve nini wakati shahidi mkuu, Mwakyembe, tayari amedai kuwa anayetakiwa kuwa kizimbani ni dereva wa lori!
  (7) Raia anapotoa ushahidi kama huo wa Mwakyembe na dereva wake, kazi ya Polisi ni kuufanyia kazi na kuupeleka mahakamani kwa uchambuzi wa kitaalamu. Uwezo wa Polisi kutoamini ushahidi wa upande mmoja nje ya mahakama, unatokana na sheria ipi?
  (8) Hivi Polisi wanaelewa implications za kuukataa ushahidi wa Dk. Mwakyembe ambaye siyo tu kiongozi kisiasa bali vilevile ni afisa wa mahakama (kwa msingi kwamba ni wakili)?
  (9) Jopo la wachunguzi wa Polisi linasemaje kuhusu taarifa ya awali ya RPC, taarifa ya meneja wa TANROADS na taarifra zingine kwamba ajali hiyo ilisababishwa na taili kuchomoka?
  (10) Abiria waliokuwa kwenye mini-bus iliyotokea Iringa na kuona ajali hiyo, wanasemaje kuhusu madai ya Dk. Mwakyembe na dereva wake na madai ya Polisi?


  Wakuu, naishia hapo.
  Fataki
   
 12. k

  kamaudoulton Member

  #12
  May 26, 2009
  Joined: Apr 13, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Fataki, now you are talking! Ahsante kwa kuibua hoja zinazo add value ya JF badala ya bla bla bla za kusikia na kudhania.
   
Loading...