Dereva mzuri ni yupi?



Kwa maana hiyo unakiri kuwa Magufuli ni dereva mzuri maana anatafakuri sahihi na anatetea wanyonge ambao ndio wengi hapa Tanzania.
 
mtu mwenyewe anakwambia kabeba abiria kwenye lori, tangu lini lori likabeba abiria,
 
Kusema kwamba dereva mzuri ni yule asiyesikiliza abiria wake sidhani kama ni sahihi.
Yaani dereva we ukae tu macho mbele hata kama mizigo inaanguka usikilizi we mwendo "mbere"
Basi sawa, kuna mtu anataka kuchimba dawa, ukimwambia atachimba 2020 atachafua hali ya hewa kwenye lori tulilopanda.
 
Lori ni gari la kubeba mizigo. Lakini hutokea mara chache likabeba watu hasa nyakati za misiba wakati wa kwenda kuzika au kubeba wafuasi wa Chama Cha Mashinani kwenda kwenye mikutano ya kampeni.

Sasa la ajabu dereva wa lori aliyepakia mizigo unaomba ushauri kwa watu ambao hawapo ndani ya gari kwa kuandika maandishi haya nyuma ya roli lake HOW AM I DRIVING? au NAENDESHAJE? na kuweka namba ya simu ili apigiwe kuelezwa juu ya uendeshaji wake, inakuwaje huyu wa kwetu hataki kutusikiliza sisi abiria wake tuliomo ndani ya lori lake? Kama anayumba hovyo barabarani, anaturusha kwa spidi kwenye matuta na wemgine ni wajawazito tusimwambie? Kuna wengine wamezidiwa wanataka kuchimba dawa na dereva hataki kusikiliza abiria je wajisaidie humo humo? Je tukisema anaendesha kidikteta tutakuwa tunakosea? Na je tukisema hakupitia mafunzo ya udereva na ana leseni ya mtaani tutakuwa tumekosea. Maana dereva mzuri ni yule anayepokea maoni na ushauri wa abiria wake na walio nje. Sasa mfano abiria anakwambia amepigiwa simu kuwa huko mbele kuna roli jingine limeanguka barabarani au daraja limebomoka sasa anakwambia dereva uchukue tahadhali na wewe hutaki si mwisho utaenda kuwa bwaga na wewe mwenyewe kufa. Tafadhali dereva wetu wa lori nenda NIT ukasome!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…