Dereva mzuri ni yupi?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,924
Reaction score
831,405
Hili swali ukiwauliza wengi watakupa majibu yasiyo sahihi na kati yao tena wasomi kabisa watakwambia dereva mzuri ni yule asiyesikiliza abiria wake wanasemaje
sahihi kabisa lakini ni makosa makubwa kujiaminisha kwenye dhana hii ama kudhani ndio jibu sahihi

Dereva naye ni binadamu kama binadamu mwingine yoyote sio mkamilifu ana mapungufu yake ....udereva ni fani ni ujuzi wa kusomea darasani kwa kufundishwa na wataalamu ambao nao ni binadamu vile vile

Dereva ni mmoja tu na hapaswi kuwasikiliza abiria ila hiki si kigezo cha dereva bora

Dereva bora ni yule ambaye pamoja na kufuata sheria za udereva na barabarani lakini ana tafakuri ya kuweza kuepusha ajali na kuhakikisha abiria wake wanafika safari yao salama salimini

Dereva mzuri ni yule anayehakikisha chombo chake ni kizima na hakina kasoro yoyote

Kuwa dereva mzuri kuna hitaji zaidi ya kutokuwa na misimamo isiyozingatia hekima weledi na tafakuri
 
Kweli kabisa chief hapo umenena, dereva angalau awe na elimu ya kawaida ya chombo chake na akikague kabla ya kukiondoa na awe makini na dalili yoyote inayoonyesha hitilafu ya chombo na pia akili na mawazo yake kwa kiasi kikubwa yawe barabarani.
 
Mkuu samahani kwa swali lililo nje ya mada
Wewe ni freemason?
Nilikuuliza kwenye ule uzi wa kumzika chande sikuona jibu
Na niliona mahali ukiwa umeandika kama ulikuwa mgeni mwalikwa kwenye msima wa freemason Chande.
 
Mkuu samahani kwa swali lililo nje ya mada
Wewe ni freemason?
Nilikuuliza kwenye ule uzi wa kumzika chande sikuona jibu
Na niliona mahali ukiwa umeandika kama ulikuwa mgeni mwalikwa kwenye msima wa freemason Chande.
Hapana mimi sio Mason bali nilisoma tu hiyo elimu juzi nilikuwepo pale kama mwombolezaji wa kawaida
 
but not to that extent
 
huwezi kuwa dereva mzuri bila kufwata sheria za barabarani ikiwemo kuwa na mwendo husika kwa mahali husika.

sasa kama abiria wanakupigia kelele lazma ujiulize kama unafaa kuendesha hicho chombo ama unapaswa ufwate sheria za barabarani yakinifu ili abiria waweze kukuamini kwenye udereva wako.
 
Dereva mzuri ni yule ambae akiwa barabarani mawazo yake yote huwepo barabarani,Ili kuweza kuleta usalama Kati yake na watumiaji wengine wa barabara,anakuwa makini Ili asiwe chanzo cha ajali,pia anakuwa makini Ili kuepuka ajali ambazo zinaweza kuepukika bila uzembe wake.
 
K Laɓda gari lina vyoo
Kwa iyo ata sisi abiria tukimwomba dreva tuchimbe dawa,, dreva azibe masikio?
 
baba vivi upo?
Mimi nipo aisee,
mishe za kumzika ndugu yangu chande,tulipewa masharti makali kutotumia mitandao ya kijamii mpk tumalize kazi ya mazishi
 
Mimi nipo aisee,
mishe za kumzika ndugu yangu chande,tulipewa masharti makali kutotumia mitandao ya kijamii mpk tumalize kazi ya mazishi
Duuh kumbe ulienda nawe?
 
Hahaha unajua kuna wakati ukimsikiliza kiongozi tena wajuu unatamani uzibe masikio maana unakuta hukutarajia kusikia maneno fulani kutoka kwa mtu huyo na hasa ukizingatie level yake ya elimu inahitaji analysis ya mambo kwa hali ya juu.

Hivi kumbe zile namba za simu za makamanda wa polisi wanazoweka kwenye mabasi ili dereva kama hawasikilizi abiria wawapigia ni upuuzi mtupu??Barabara ina alama za kuzizingatia, ina sheria na kanuni za kufuata..... lakini nashangaa dereva anasema hapaswi kusikiliza abiria ikumbukwe Mr. dereva hii si gari binafsi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…