Yaliyojiri bungeni - April 04, 2017: Mama Salma Kikwete aapa kuwa Mbunge, Kikwete ashangiliwa...

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
BUNGE LA 11 LA JAMHURI YA MUUNGANO
MKUTANO WA SABA-KIKAO CHA KWANZA


Bunge linaanza kwa kuapishwa kwa mbunge wa kuteuliwa mama Salma Rashid Kikwete.

Wageni waliofika bungeni wanatambulishwa na mgeni aliyefika leo ni rais mstaafu Dr Jakaya Mrisho Kikwete, bunge linalipuka kwa makofi huku zikisikika 'sauti za tumekumis'

MASWALI NA MAJIBU
Swali: Serikali haioni ipo haja ya kuongeza ruzuku ya TASAF?
Majibu: Serikali tayari imeongeza ruzuku na walengwa wameweza kujikwamua kiuchumi

Swali la Nyongeza: Ni kwa kiwango gani mpango huu umeleta matokeo chanya?
Majibu: Mpango huu umewasaidia hata watoto waliotoka waliotoka familia duni kuweza kujikimu hasa wakiwa shuleni

Swali la Nyongeza(mama Salma Kikwete): Serikali ina mpango gani wa kuongeza huduma hii katika mkoa wa Lindi?

Majibu: Mpango wa TASAF umefanikiwa kwa asilimia 70. Na utekelezaji utaendelea hadi huko katika mkoa wa Lindi.

Swali: Ni lini serikali itarekebisha sheria ya mamlaka ya hifandhi ya Ngorongoro?

Majibu: Wakazi wa Ngorongoro hugawiwa mahindi bure, ambapo tani 5600 hugawanywa. Na wale wanaojiweza huuziwa kwa bei nafuu. Aidha serikali ipo mbioni kufanya marekebisho ya sheria hii ili kuweza kupatikana maeneo yatakayotengwa kwa ajili ya kulima na kunywesha mifugo

Swali: Serikali ina mpango gani wa kuwapatia zao mbadala wa pamba baada ya kushuka katika soko?

Majibu: Wakulima wanaweza kulima zao la pamba samabamba na mazao mengine kama mazao ya bustani.

Serikali imeandaa mpango mzuri ili kuhakikisha wakulima wanatumia mbegu bora ili kuhakikisha wanapata mazao mengi.

Serikali imeandaa mpango wa kuwekeza katika viwanda vinavyoongeza thamani ya pamba ghafi na kuweza kuuza pamba katika soko la ndani.

Swali: Serikali imewekeza kiasi gani kwenye zana za kisasa za kilimo?

Majibu: Serikali imewekeza mikakati ya muda mrefu na muda mfupi, kama skimu za umwagiliaji, mpango wa matone. Kuna matreka makubwa zaidi ya elfu 10 na madogo zaidi ya elfu saba.

Swali: Ni lini serikali itaanza kuchimba ges ya Helium?

Majibu: Ni kweli taarifa za awali zinaonyesha kuna uwezekano wa uwepo wa gesi hiyo ya Helium katika bonde za ziwa Rukwa.
Kazi zinazofanyika kwa sasa ni upembuzi yakinifu na utafiti kina na punde vikikamilia gesi hii itaanza kuchimbwa.

Swali: Ni wananchi wangapi wa Kakonko ambao nyumba zao zimewekewa alama ya X wanastahili kulipwa?

Majibu: Hakuna mwananchi anayekidhi vigezo vya kulipwa nyumba iliyowekwa alama ya X katika hifadhi ya barabara kwani wananchi ndio waliofuata barabara.

Swali: Una uhakika kwamba hakuna nyumba zilizokuwepo kabla ya mwaka 1967 na je serikali iko tayari kufanya survey upya?

Majibu: Kurudia survey ni upotezaji wa fedha

Swali: Ni lini serikali itajenga barabara ya Tarime-Serngeti?

Majibu: Barabara hii inahudumiwa na TANROADS, wizara imekuwa ikijenga barabara hii kwa awamu na hadi sasa km 7 zimekwishakamilika kwa kiwango cha lami. Aidha upembuzi yakifinifu na usanifu wa kina unaendelea kwa barabara yote na punde ukikamilika ujenzi utaanza.

 
Katika hali inayoonyesha kuwa Watanzania kupitia kwa Wabunge wao wamemmisi Jakaya Kikwete Rais mstaafu, leo Bungeni wakati wa kuapishwa mama Salma, Wabunge wameshangilia kwa zaidi ya dakika 17. Naamini JPM atakuwa amechukia kuona JK akishangiliwa leo.
 
Back
Top Bottom