Wakati anazindua reli ya SG rais alisema yeye kama dereva hasikilizi wala kuwaangalia abiria wake.
Wakati nachukua kozi yangu ya udereva pale NIT, supervisor wangu alinieleza kuwa, ukitaka kuwa dereva mzuri hasa dereva wa magari ya abiria lazima uheshimu mawazo na maoni ya abiria uliowapakia.
Wewe ni binadamu, mwili huchoka na akili huchoka, wakati wa safari ndefu kutokana na uchovu unaweza kupitiwa na usingizi kwa sekunde kadhaa (blink of an eye) ukasababisha ajali, kutokana na uchovu unaweza kujikuta unaongeza spidi bila kujitambua, imeshatokea.
Inawezekana abiria anataka kukutaarifu ajali ya moto iliyotokea siti ya nyuma, inawezekana buti la nyuma limefunguka na mzigo umedondoka bila wewe kuwa na habari. Inawezekana vile vile abiria wanataka kukupa taarifa ya mgonjwa au mjamzito ndani ya lori (basi) unaloendesha. Kwa hiyo kuziba masikio kwa dereva kunaweza kusababisha ajali zisizo za lazima.
Mimi nafikiri dereva mzuri ni yule anayejali na kuwasikiliza abiria wake.