Dereva atwangwa makofi hadharani na trafiki

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KATIKA hali ambayo isiyo ya kawaida askari wa Usalama barabarani (trafiki) wa kituo cha Gerezani manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, amemtwanga makofi dereva wa gari hadharani kwa kile kilichodaiwa alikiuka taratibu za barabarani.
Tukio hilo la aina yake lilitokea eneo la gerezani leo ambapo dereva huyo alikuwa akiendesha gari dogo aina ya Pick-up lenye namba za usajili T 595 BMR.

Askari huyo ameshuhudiwa na watu waliokuwa karibu na maeneo hayo ikiwemo nifahamishe akifungua mlango wa gari hilo na kumtwanga makopfi dereva huyo ambaye djina lake halikuweza kupatikana mara moja mara baada ya dereva huyo kukaidi kusimama wakati aliposimamsihwa na askari huyo na kuendelea kuendesha gari yake.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Mohamed Mpinga amesema dereva huyo alikamatwa hapo kwa kuwa alipokuwa akitokea barabara ya Nyerere eneo la Tazara alitanua njia na aliposimamishwa hakusimama na alipofika eneo la mataa ya Kamata ndipo alikamatwa baada ya askari kupigiana simu.

Hata hivyo Kamanda huyo alisema ataendelea kutoa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo
 
hapo hatoki,ni kesi juu ya kesi!na ataanzaje kushitaki polisi wakati wana kesi nae duh!pole dereva
 
Lkn kuna sheria ya Trafiki kumpiga dereva ingali ameshamkamata? Mi naona hata huyo Trafki amechukua sheria mkononi. Hata nami ningekuwa huyo dereva ningemfungulia huyo trafki kesi ya SHAMBULIO.
 
Trafiki amenyimwa unyumba huko uswazi anakoishi anakuja kumalizia hasira zake kwa watu wasiohusika. Aisee ningekuwa mimi ningemalizana nae palepale on the spot.:biggrin1:
 
Huyo trafiki kakosea saaana kwani haruhusiwi kipiga m2 pasipo na sababu inayo mruhusu kufanya hivo hata kama kakosea mahakama tu ndio inayo ruhusa ya kuruhusu hilo au inaweza kutokea ambapo kuna kuwa na sababu za kiusalama kama mtuhumiwa kuleta vurugu wakakti anakamtwa na kuanza kupiga askari na vingine vinavo fanana na ivo

naona sare alizo vaa ndizo zilizo mpa kiburi na hata huyo dereva alimuogopa tu kuhusu hilo huyo dereva anaweza kumshtaki huyo trafik kwani ikiwa amegoma kusimama kuna mambo mengi aweza jitetea kuwa gari iligoma brake hivyo kushindwa kusimama kwa wakati,,, ngekuwa mimi kwanza namchapa kisawasawa huyo trafiki halafu ntasema nliona napigwa pasipo sababu hivyo nikaona nashambuliwa halfu mengine yatafuata twende mahakamani hata kama wata nyanya sa nkiwa mahabusu ila inshu mahakamani tatizo hatujui haki zetu na hata askari wanajua hilo ndo mana wanatuonea nitapost haki ta dereva anapo kamatwa na trafiki kwenye profile ya sheria
 
Trafiki amenyimwa unyumba huko uswazi anakoishi anakuja kumalizia hasira zake kwa watu wasiohusika. Aisee ningekuwa mimi ningemalizana nae palepale on the spot.:biggrin1:

Una uzoefu na hawa watu mazee,hasira zote hizo zinatoka wapi?
 
Back
Top Bottom