Derby ya Pepsi na Coca Konde-Boy Okoa Coca

Derby ya Pepsi na Coca Konde-Boy Okoa Coca

Kampuni zenye soda za Coca Cola hapa Tanzania ni Bonite Bottlers Ltd iliyoasisiwa na Mengi (RIP) na Coca Cola Kwanza Ltd.

Siyo kila soda ya Coca ni ya Mengi
Asante kwa ufafanuzi Mkuu, Noted with thanks 🙏
 
Bonite ya Mengi haiuzwi Dar na wala Mengi hana ushirika wa biashara na Coca-Cola Kwanza ya Mikocheni.

Coca-Cola industry imegawana maeneo ya biashara kikanda kwa nchi zote duniani. Kwa Tz iko hivi:-

1. Coca-Cola Kwanza inauza Kanda ya Pwani, Mashariki na Nyanda za Juu Kusini.

2. Nyanza Bottling ya Gachuma inauza Kanda ya Ziwa.

3. Bonite Bottling ya Mengi inauza Kanda ya Nyanda za Juu Kaskazini.

Pepsi iko nchi nzima.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Shukrani kwa Ufafanuzi Mkuu, Noted with thanks 🙏🙏
 
The power of BRANDING.

Niliwahi kuwazungukia sana hao jamaa wakati nafanya research ya CELEBRITY ENDORSEMENTS TOWARDS BRAND IMAGE IN THE SOFT DRINK INDUSTRY IN TZ.

Mtoa maada nimeona hapo umewataja hao jamaa wawili kwamba mmoja anaweza kucompete na mwenzake wakiingia kubrand vitu sidhani kama upo sahihi.....

Fuatilia sababu ya mmoja wao kutemwa na kampuni nyingi ikiwemo moja ya SOFT drinks pia utanielewa....

Sio kila msanii mkubwa anafaa kuwa brand ambassador, big NO

Baadhi ya vitu ambavyo vinakufanya uchukuliwe kuwa balozi
1. POWER DISTANCE & MASCULINITY (unaipata ukigusa consumer behaviour) .......hapa inamatter sana kama tunachagua gender ya balozi (me &ke) hizo ndo sababu za msingi.
2. Influence
3. Image
4. Credibility
5. Reputation.

Hizi sababu zinakupa swali mwenyewe ujiulize kwamba why kampuni nyingi kubwa duniani zinapenda sana kuwatumia WAHINDI kama brand ambassadors globally....kuna akina SHARUKH KHAN apple, Alia Bhatia nadhani ni MCDONALD kama nakumbuka vyema......Amir Khan....Samsung etc....


Then nimeona watu wanachanganya FRANCHISING & LICENCING......


Mkuu ni hayo tu, nimeipenda sana thread

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kinywaji cha Pepsi kinadaiwa kutamba sokoni na kutishia market share ya mtani wake wa jadi Coca.

Derby hii inadhaniwa unywaji wa Pepsi kwa kasi ya mwanga umekolezwa na Mondi kui-brand.

Haijulikani kama mkataba wa Mondi ku-brand Pepsi utapofikia ukomo mtani wa jadi Coca atatamalaki soko na kuchukuwa kombe (market share) la Derby hiyo?

Mtu pekee anayeweza kummudu Mondi ni Konde-boy.

Una-beti kwa kinywaji kipi kwenye Derby hii?
Mo Xtra at the wheel
 
Niliwahi kusikia Pepsi waliiba formula ya Coca na kuiboresha.

Huenda kwa kufanya hivi walifanikiwa kuliteka soko.

Japo Kibongo bongo hii Kampuni ya Coca inabidi ipunguze Ubahili kwenye kuipromote Soda yao.

Naona tangu Mzee Mengi afariki Dunia ni kama wale Wahindi aliowaajiri pale Mikocheni wanataka kumhujumi.
Usichokijua coca ya dar si coca ya Mengi, coca ya Mengi ipo Moshi, Arusha n Tanga kama sikosei
 
Mimi na kampuni ya Coca -Cola damu damu…yani ni pate Coca cola au Sprite weeeee…..roho kwatu
 
Mimi na kampuni ya Coca -Cola damu damu…yani ni pate Coca cola au Sprite weeeee…..roho kwatu
Nasikia kuna Msukuma wa Ushetu alileta ng'ombe Pugu Mnadani kwa mara ya kwanza kusafiri nje ya Ushetu. Alipopewa Sprite akasema auziwe mbegu yake aende apande Ushetu. Akakutana na Apaikunda Ufoo wa Machame anausa baa, akam-usia mnaanaa eti ndiyo mbegu ya Sprite. Baghosha!

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Usichokijua coca ya dar si coca ya Mengi, coca ya Mengi ipo Moshi, Arusha n Tanga kama sikosei
Okay, shukrani kwa Ufafanuzi.

Kumbe naweza kuomba kibali nikawa nazalisha Soda za Coca na kuziuza kwenye Nchi zisizo na hiyo bidhaa?
 
Back
Top Bottom