Deodatus Balile: Afya ya Rais si jambo la siri wala siasa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,638
2,000
Salaam

Mwandishi na Mhariri wa siku nyingi pia Mwanachama wa JamiiForums, Deodatus Balile amesema suala la Afya ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni suala nyeti linalohitaji kufikirika kwa kina sana.

674515FD-78D8-4B21-8900-92141443A97A.jpeg


NUKUUU ZA BALILE:

Lakini tuanze kuangaliwa kwanini tumefika huko, kwa sababu tukiangalia misingi ya Uandishi wa Habari, wenzetu wakenya wanatulaumu kwamba hatujafanya jambo lolote, na habari zote huanza kama uvumi.

Zikianza kama uvumi ndipo jukumu la uandishi wa habari linapoanzia, mimi sipendi kuona wanahabari wakizungumza lugha ya wanasiasa, kuzungumza kama kuna vita, kuna nini. Hapa kuna vitu vingine ni self induced kisheria, kwa maana kwamba Jambo likitokea ukilitafutia ufumbuzi ndani ya muda mfupi haupati tatizo lolote lakini ukiliacha likaendelea utafika katika msigishano ambao hauna msingi sana.

Hapa nchini tuna Sheria kadhaa.
Tuna Katiba - ile ibara ya 18, tuna Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari kifungu cha 7 kifungu kidogo cha kwanza (a) na (b), tuna Sheria ya Haki ya kupata Taarifa, kifungu cha 5 na 9 inatoa utaratibu wa kupeana taarifa kunapotokea tatizo au jambo lolote.

Awalaumu watendaji Serikalini kwa kukalia habari/taarifa

Si kweli kwamba tumekaa kimya. Kama kuna yeyote anayehusika na kutoa habari, hakuna ambaye anahusika kutoa habari ambaye sijawasiliana naye juu ya hili suala.

Mimi nasema wanalo jukumu la kutoa habari. Ukisoma kifungu cha 7 kifungu cha kwanza (a), cha Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari, kinataka vyanzo vya habari kutoa habari kwa vyombo vya habari. Bahati mbaya ndugu zetu wamekaa kimya.

Wana hababari tumefanya kosa, wanahabari wenzetu walioko serikalini, badala ya kujua wako pale kurahisisha upatikanaji wa habari, wako pale kudhibiti habari. Hizi Sheria tatu hakuna hata mmoja anayetekeleza inavyostahili.

Unapouliza kuhusu hili kwa mfano afya ya Rais si kwamba unashiriki vita ya kisiasa, hapana! Ni jukumu letu kama ambavyo Polisi akisikia kuna mwizi sehemu fulani anakwenda kufuatilia.

Lakini bahati mbaya Waandishi wa habari wakifuatilia masuala kuhusu nchi wanaambiwa wametumwa, wanataka kuthibitisha kwa ajili ya wapinzani, hii ni cheap thinking.

Kuna ombwe, kimya hakitatui tatizo

Unapoacha ombwe, unaruhusu watu kutafuta majibu wanayoyajua wao.

Rais ni binadamu kama binadamu wengine, tunamwombea heri, ila kama watu wanahoji yuko wapi si sahihi kuendelea kukaa kimya.

Kauli ya Waziri Mkuu haijitoshelezi

Tunashukuru tumeusikia ufafanuzi wa Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa, ametoa kauli ila hii haiondoi ukweli kuwa wapo wenye imani kama Thomas. Yesu ilipoelezwa kuwa amefufuka, Thomas alisema hataamini hadi amguse.

Yesu hakupata tabu. Alimwita Thomas, akamgusisha makovu na Thomas akaamini. Naamini kuna Watanzania ambao ni sawa na Thomas. Si vibaya Mhe. Rais Magufuli akijitokeza hawa kina Thomas wakagusa makovu yake na kuamini.

Utamaduni wa kujulishana afya ya Rais

Tanzania tumejenga utamaduni wa kupeana taarifa za hali ya afya ya viongozi wetu. Mwaka 1999 kwa tuliokuwa tayari tunafanya uandishi, Serikali kupitia kwa Godfrey Nkurlu, ilitujulisha kuwa Mwalimu Nyerere anaumwa.

Rais Benjamin Mkapa alipougua, Msaidizi wake, Maura Mwingira alitufahamisha kila hatua hadi aina ya upasuaji aliofanyiwa.

Rais Jakaya Kikwete alipougua, tulitajiwa hadi ugonjwa unaomsumbua kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kwa Salva Rweyemamu.

Nchini Uingereza Waziri Mkuu Boris Johnson alipoumwa, dunia ilijulishwa kupitia kwa mwandishi wake. Vivyo hivyo, Rais Donald Trump wa Marekani au Angela Merkel wa Ujerumani, hawa walipougua dunia ilijulishwa.

Hivyo kama Rais wetu anaumwa, ni vyema tuelezwe na wala si jambo la kushangaza kwani naye ni binadamu kawaida.

 

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
3,326
2,000
Sasa Balile yani Rais atoke kisa Lissu na wewe mmetaka atoke? Aje kujionyesha tu?
 

Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
4,498
2,000
Watu bwana,wanamuamini muhuni mmoja tu huko twitter ambaye hawaijui hata jinsi yake achilia mbali hali ya afya yake ya akili
 

Ivan said

Member
Feb 14, 2021
82
150
Tangu tetesi za kutokuonekana kwa Rais JPM moyoni mwangu nimekosa amani kabisa na itarudi nikimuona anaongea Yeye kama yeye! Upo wapi Rais wangu mpendwa uliyeleta nidhamu ya utumishi kwa taifa letu; upo wapi Mheshimiwa Magufuli?. Shime jitokeze nikuone na kusikia sauti yako!. Mungu akulinde na kukuepusha na mitego yote mibaya popote pale ulipo.
 

pakaywatek

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,210
2,000
Watanzania wenzangu lazima tujue kuwa kuna watu WATU WASIOJULIKANA hapa Tanzania huenda wameshafanya yao.
 

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
5,312
2,000
MUNGU anachotaka ni kauli kutoka Kwenye vinywa vyenu kuwa magufuli ni mgonjwa vinginevyo mnazidi kumtesa Tu mgonjwa...

MUNGU anasababu zake mpaka TANZANIA ikubali kuwa raisi anaumwa ndipo Afya yake itaimarika, endeleeni kuficha na MUNGU nae anasubiri kukiri kwenu ni Bora mtangaze kuwa ni mgonjwa pengine watu wangefunga na kuomba na MUNGU angesikia sala zetu
 

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,668
2,000
Hatutaki mambo ya Mabeberu. Huku kwetu sio kwao. Mabo ya Ngoswe mwachie Ngoswe .

Rais wetu hawezi kuumwa. Ana ulinzi mzuri na pia yupo safi kabisa. Kwani Shida ipo wapi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom