Denti darasa la sita afumaniwa muda wa masomo

Denti darasa la sita afumaniwa muda wa masomo

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,335
Na Dustan Shekidele, Morogoro
BINTI wa Shule ya Msingi Chamwino amefumaniwa akiwa kimahaba na kijana mmoja aliyedaiwa kuwa ni dereva wa bodaboda mkoani hapa.

Denti aliyefumaniwa (nyuma ya wa kwanza kushoto) akipelekwa shuleni na ndugu zake baada ya kufumaniwa.​
Tukio hilo limetokea hivi karibuni ambapo chanzo makini kimeeleza kuwa mtego wa kunaswa kwa denti huyo anayesoma darasa la sita, uliandaliwa na dada zake wanaomlea kufuatia wazazi wao kufariki dunia.
Baada ya paparazi wetu kujiridhisha na picha za tukio hilo, aliwafuata dada zake pamoja na walimu wa shule hiyo lakini walikataa kutoa ushirikiano.
“Utuhoji ili iweje? Swala hili tumelipeleka pale shule na tutalimaliza shuleni kwani hawa wote ni vijana wetu, hatuhitaji habari hizi zitoke kwenye vyombo vya habari,” alisema kwa ukali dada mmoja wa mwanafunzi huyo ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Alipotafutwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na kuulizwa juu ya tukio hilo, alikataa kuzungumzia chochote akidai shule yake haihusiki na tukio hilo kwa kuwa lilitokea nje ya maeneo ya shule.
“Sioni sababu ya kutaja jina langu, mimi ni mwalimu mkuu wa shule hii, fumanizi hilo halituhusu kwa sababu halikutokea kwenye madarasa wala vyoo vya shule yetu,” alisema mwalimu huyo.

 
hao dadazake nia yao kupata pesa toka kwa huyo bodaboda (kama faini), na wala hawana uchungu kwa tukio hilo. PESA MBELE.
 
wanafunzi wa siku hizi yani hayo mambo yamekuwa kawaida
embu waadabishwa wanaokutwa nao na hao wanafunzi
 
Huyu boda boda apewe adhabu kali sana ili liwe fundisho kwa wanaume wote wenye tabia kama yake!
 
kwa shule hiyo hilo ni tukio la kawaida saaaana! amini usiamini unaweza kwenda kuwapima wanafunzi wa darasa la nne ukachanganyikiwa ukakuta walio tunza ubikira wao ni asilimia 30 (30%) wengine wote wanawajua wanaume vizuri tena waume za watu.
lakini kijana ana kesi ya kujibu tena ya kubaka
 
Sasa huyo msichana wakati anatoka nyumbani kwenda shule hao dada zake walimuona? Mbona hajavaa uniform? Au yeye uenda shule na nguo zake za nyumbani?

Sioni kama limetumika neno sahihi kwenye hii habari. Hivi kweli tunaweza kusema msichana ambaye hajaolewa na mvulana ambaye sio mume wa mtu unaweza kusema wamefumaniwa? Mimi nafikiri lugha sahihi ni kwamba hawa vijana wamekutwa wanafanya mapenzi, sio kufumaniwa bwana!!!!

Tiba
 
train uwa haimgongi mtu, mtu ndiye anayegonga train... Mwenye makosa ni huyo dereva wa boda boda. Wanafunzi walaumiwe ila ni akina nani wanaowatongoza na kuwarubuni kama sio sisi wanaume.
Unamuona mtoto mdogo sawa na wanao, mdogo wako, mjukuu wako still unamtongoza unamshawishi mpaka anashawishika.
 
Sasa huyo msichana wakati anatoka nyumbani kwenda shule hao dada zake walimuona? Mbona hajavaa uniform? Au yeye uenda shule na nguo zake za nyumbani?

Sioni kama limetumika neno sahihi kwenye hii habari. Hivi kweli tunaweza kusema msichana ambaye hajaolewa na mvulana ambaye sio mume wa mtu unaweza kusema wamefumaniwa? Mimi nafikiri lugha sahihi ni kwamba hawa vijana wamekutwa wanafanya mapenzi, sio kufumaniwa bwana!!!!

Tiba

UZINIFU sio MAPENZI
 
mbona kwenye hiyo picha binti anaonekana mkubwa kabisa huyo?
 
Darasa la sita au kidato cha sita?
Kwa sababu ni wa shule ya msingi, itakuwa nia darasa la sita(vijijini wapo wanaochelewa kuanza shule).

Kidato cha sita wengi wao wamezidi umri wa miaka 18, kwa hiyo kesi hiyo isingekuwa na nguvu, ili mradi tu hakubakwa alikubali kwa hiari yake.
 
Kama ni kweli ni mwanafunzi wa darasa la 4 kazi ipo!hawezi kumaliza shule huyo!umri umeshamtupa mkono!na mazingira hayo ataolewa haraka tu!au mimba fasta tu!
 
Wazazi/walezi wa siku hz ndo tabia yao kugeuza vibinti vyao kitega uchumi kwan hata akickia binti yake anajihucsha na tabia hizo anatulia tu lakini likishatokea tatizo tu anafunga hadi kibwebwe duuh
 
Kawaida sana hiyo mbona. Hata bibi yangu aliolewa na babu akiwa darasa la tatu akaachishwa shule
 
Hapa ni kuwa tu na huruma na huyu binti kwani kutokana na mujibu wa mheshimiwa waziri mtarajiwa ​@MziziMkavu ni kwamba msichana mwenye umri kati ya miaka 13 mpaka 19 yupo katika wakati mgumu sana psychologically. Umri huu wa kuvunja ungo msichana anakuwa katika kipindi cha kujifikiri ama kujitambua where her ego inakuwa at a low point. Nyege za hapa na pale haziishi na bahati mbaya huyo msichana kama katoka katika familia ya kifukara basi ujuwe kuwa njaa, ukata, na nyege zilichangia yeye kwenda gesti badala ya darasani. Kwa pamoja tumpe pole😱hwell:
 
Back
Top Bottom