Deni la Taifa: Nani atalilipa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Deni la Taifa: Nani atalilipa?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Aug 31, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Benki Kuu imetoa ripoti yake kwa ajili ya mwaka wa fedha 2007/2008 ambayo inaonyesha deni la Taifa kuongezeka kwa takriban 25% katika mwaka mmoja! Deni letu la nje bado ni kubwa ingawa deni la ndani linapungua.

  Deni hili la Taifa ni 33% ya GDP ya nchi.

  Je deni hili linaloongezeka kila siku ni nani atalilipa na ni lini litalipwa?

  Ama ni kwa nini deni hili linalongezeka kutokana na kuendelea kukopa na riba itokanayo na mikopo ambayo tayari bado iko katika vitabu na majedwali ya mapato na matumizi ya nchi yetu?

  Nimetatizwa sana na kauli ya Naibu Waziri wa Fedha Jeremiah Sumari ambaye amedai kuwa tusiwe na shaka kuhusu kuongezeka kwa deni hili na ni deni ambalo tunaweza kulihimili na kulilipa! Zaidi ni kitendo cha Sumari kudai kuwa kuna nchi nyingine ambazo zina uwiano mkubwa wa Deni lao la Taifa kuliko Tanzania hivyo hakuna haja ya kuogopa!

  Je wewe Mtanzania mwenzangu unaipokeaje kauli hii ya kusema usiwe na wasiwasi tunaendelea kukopa huku hali halisi ni kuwa hatuna nguvu za kiuzalishaji mali na ukusanyaji mapato ambazo zitalipa Taifa pato la kuweza kujitegemea na kupunguza mzigo huu wa kutegemea mikopo na misaada kujiendesha?

  Kama unaridhika na kauli ya Sumari, basi nakwambia wazi kuwa wewe utaendelea kuwa masikini na ombaomba na kamwe hutaweza kujitutumua na kujitegemea.

  Kama umeshikwa na hasira kama Mchungaji ya kusikia kauli hasi kutoka kwa kiongozi mkubwa kama huyu, basi itakulazimu ujiulize ni vipi tunaendelea kukopa na hata kuongeza deni na ni nani anayetuongezea mzigo huu wa deni hili!

  Je ni wewe Mtanzania au ni Viongozi ambao wamekosa mwamko wa kujenga uchumi unaojitegemea?

  Tunapofikia mahali tunajigamba kuwa deni letu ni bora kuliko la Rwanda, Kenya hata Msumbiji, tujiulize je nao wana rasilimali sawa na zetu? je uzalishaji mali wetu wa ndani ni sawa? je mikopo na deni ni kutokana na matumizi sawa na kimaendeleo?

  Nina uhakika kwa asilimia 85% kuwa sehemu kubwa ya mikopo (70%) imetumika kwa matumizi yasiyo ya lazima na yangeweza kupunguzwa.

  Cha kutisha ni kuwa Tanzania si kwamba haina fedha wala uwezo wa kujitegemea, bali ni mazoea mabaya ya kukopa ambayo yamejenga mizizi mibaya inayoeta uzembe na hata ufisadi na hivyo dhana ya kuwa wabanifu na kutumia kwa uangalifu tulicho nacho haiko tena.

  Tatizo kubwa la Serikali ya Tanzania ni matumizi yasiyo na kikomo wala kuwa na hamasa ya kubana matumizi na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima au kama wenzetu wanavyoyaita Wasteful spending!

  Mfano wa matumizi yasiyo na faida wala manufaa ni Serikali kung'ang'ania kuwa mshiriki wa uzalishaji mali katika sekta ambazo kuna ushindani tosha wa sekta binafsi. Hili husababisha kuanzishwa kwa mashirika, taasisi na miradi ambayo inaweza kufanya na watu binafsi na Serikali wajibu wake uwe ni kwenye uratibu.

  La zaidi katika matumizi mabovu na yasiyo ya lazima ni kule kuhalalisha vitu ambavyo vinaweza kufanywa kwa kutumia teknolojia ya simu, barua pepe au watendaji wachache.

  Mfano, kuna tabia kubwa ya kukimbilia kuandaa makongamano, semina, warsha na hata mikutano isiyo na ulazima ambayo hutumia fedha nyingi za walipa kodi na kudonoa fungu la misada na mikopo ambalo lilipaswa kutumika kwa miradi ya kimaendeleo na kuishia kuwa matumizi ya kawaida. Kwenye hivi vikao, kuna malipo ya usafiri na malazi, kushiriki kikao na mengineyo kwa ajili ya watu ambao hulipwa mishahara kwa kufanya kazi ambazo ni wajibu wao.

  Ama misafara ya kila mtu inapofika mahali kiongozi anafanya ziara ya kutembelea sehemu, utakuta kuna zaidi ya watu 100 ambao kazi yao ni upambe kwa kudai eti wanapaswa kuandamana na kiongozi.

  Sasa matumizi kama haya, yanaipunguzia Serikali mapato ukiongezea uzalishaji mali wetu ulio duni na wa kijima ambao hauna uwezo imara kusimama kidete katika ushindani wa kimataifa.

  Rushwa na Takrima nayo ni mchangiaji mkubwa wa kukua kwa deni letu. Mwaka 2007, asilimia 20% ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya Bajeti zilipotea katika mazingira ya rushwa. Mwaka uliofuatia, Rushwa katika ufujaji wa bajeti uliongezeka kwa asilimia 10% hivyo kufanya upotevu wa Bajeti katika miaka miwili kuwa asilimia 50%!

  Sasa kama tunapoteza mapato na kufuja hazina yetu kwa kiwango hiki, iweje Sumari atuambie tusiwe na wasiwasi tunapoona deni la Taifa linaongezeka?

  Ninauliza ni nani atalilipa deni hili huku hata uzalishaji mali ni duni, rasilimali tunazitapanya na mapato kupitia kodi ni madogo kutokana na kutoa misamaha ya kodi na ukosefu wa uhakiki wa mapato ya wawekezaji?

  Kama tungepunguza matumizi na mfumuko wa deni, tungeongeza kipato cha Mtanzania hata kwa asilimia 25% ya kima cha chini, hii ni zaidi ya shughuli nyingine za maendeleo na ulazima kama elimu, afya, miundombinu na hata nishati.

  Kauli ya Sumari inanifanya niamini kuwa kamwe kama hatuta leta mabadiliko ya kweli ndani ya mfumo wetu wa kisiasa na utendaji kazi na maendeleo, tutaendelea kujilundikia madeni.

  Sumari katuambia, pondamali kufa kwaja, je nawe wakubali hilo? mwanao na mjukuu wataishije?

   
 2. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Amani iwe kwako Rev KS:

  Nadhani waziri wako anatumia takwimu hili kupata kisingizio cha matumizi mabaya tu. Kusema kuwa madeni ni 33% ya GDP ya nchi. Na kuwa tunafanya vizuri kuliko Kenya, Uganda au Rwanda ni kutokuwa na busara tu.

  Ratio ya madeni kwa GDP ni lazima itumie takwimu nyingine ili iwe na maana. Kwa mfano GDP ya Tanzania inategemea kwa namna moja au nyingine bajeti ya serikali ambayo inategemea 50% ya misaada kutoka nje. Wakati bajeti ya Kenya inategemea 5% -10% ya misaada kutoka nje.
  Hivyo basi waKenya, intuitively wana uwezo mkubwa wa kulipa madeni yao kuliko watanzania na vilevile wanaweza ku-bargain madeni yenye interest ndogo.
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Zakumi,

  Nilijua nitakutoa mekoni mchumi wewe. Sasa wajamaa wenzangu Mkandara na Companero sijui wamekimbilia wapi!
   
 4. C

  Choveki JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2009
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Rev Kishoka,
  Deni hilo tutalilipa sisi watanzania kwa vizazi vyetu vijavyo.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Aug 31, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Huyo Companero ni utopian huyo....subiri aje na nadharia zake za jinsi ya kulipa hilo deni...Lol
   
 6. Aiseam

  Aiseam Member

  #6
  Aug 31, 2009
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Waziri anasahau anaongea walipa kodi,nakumbuka kunamsemaji aliyesema"fungu lenu wahisani halijaliwa bali la wananchi"wake up call my friend
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  tusubiri msamaha wa madeni
   
 8. Insurgent

  Insurgent JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2009
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 469
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii kali...te he he hehe
   
 9. Sungi

  Sungi Senior Member

  #9
  Aug 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hili swala la government deficit ni jambo ambalo haliongelewi kabisa. Kujibu tu swala lako kabla sijaendelea na hoja yangu ni kwamba deni hili linaweza kuja kulipwa na vitukuu vyetu ambao hawatakuwa wamechangia katika ufilisi huu mkubwa kwa nchi.

  Serikali zetu pamoja na kwamba eti ni "maskini" inafuja fedha kwa mambo mengi ambayo hayana faida kwa wananchi. Marekani hivi sasa kuna mjadala mkali kuhusu "health care". Ingawa watu wengi wanaonyesha kutaka "universal health care", lakini swali linakuja kwamba fedha zitapatikana wapi kulipia hii project ya kuwapatia wamerkani wote (karibu Milioni 300) health care? Wananchi wapo very sensitive na matumizi ya serikali. Kwetu serikali inakuwa kubwa, wizara nyingi, nyingine ambazo zinashughulikia mambo yanayofanana, manaibu mawaziri wengi. Rais anapokuwa katika safari za kikazi anabebana na waofisa hata mia moja, fedha za ndege, malazi, n.k. zinatoka wapi? Ukijaongezea na maswala ya ufisadi, inasikitisha sana.

  Issue hapa kwangu mimi sio jinsi gani ambavyo deni letu lilivyo "dogo" n.k. kulinganisha na nchi nyingine, bali ni ukuaji wa deni lenyewe na nani atakeyelipa deni hili. Mimi sitaki kitukuu changu ambacho bado hata hakijazaliwa kiwe kimezaliwa kikiwa na deni tayari .... kweli huu ni uungwana?
   
  Last edited: Aug 31, 2009
 10. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Mwaka huu kuna uchaguzi mkuu Norway, ambapo chama cha Progressive Party (populist far-right) kimeahidi kukata kabisa misaada yote ya Norway kwa Serikali ya Tanzania (na Uganda) kama kikiingia madarakani. Na wana chance nzuri tu ya kushinda.
   
 11. Kipunguni

  Kipunguni Senior Member

  #11
  Aug 31, 2009
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo itasaidia sana maendeleo yetu hapa nyumbani; inabidi "tujifunze" kuendesha maisha yetu bila kutegemea misaada!
   
 12. G

  Genda Member

  #12
  Aug 31, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Halafu wa BoT watatoa siri ya madeni yaliyosamehewa kwa mafisadi kuchota!
   
 13. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Rev. Kishoka:

  Nikijihita mchumi nitawashushia hadhi waliopoteza muda wao mashuleni kubobea uchumi.

  Hiki ni kitu kinachohitaji common sense tu. Katika posti moja Lost Decades na ya wahujumu tulichambua sana mambo haya. Na kiundani zaidi umahiri wa uchumi wa nchi unategemea sana na data zilizopita.

  Kisiasa namlaumu sana Babu Nyerere lakini quite Frankly, yeye hakuwa na data zozote za kumsaidia ku-frame policies zake. Hivyo miaka ya 60,70 na 80 nchi ilitegemea sana intellectual perceptions na makosa makubwa yakafanyika ambayo yalitufanya tu-accumulate madeni ambayo hayakuwa mazuri na GDP yetu.

  Wakati wa Mzee Mwinyi na Mkapa zaidi ya robo ya mapato ya nchi yalikuwa yanatumika ku-service madeni. Tunaweza kuwalaumu kuwa hawakujenga universities au huduma za afya, lakini walikuwa wamebanwa na mtego wa madeni.

  Tanzania haikuwa na uwezo wa kulipa deni lake. Na juhudi za Mkapa zilisaidia nchi kusamehewa madeni. Lakini juhudi hizi zimekuja kwa gharama kubwa sana kwa sababu nchi ililazimika kuuza assets zake kwa give away prices.

  kilichotakiwa sasa ni kujifunza kutumia data za miaka iliyopita na kuelewa maana ya Fiscal Responsibility. Lakini kwa viongozi wa Tanzania hili ni somo gumu sana.

  Kitu kingine muhimu hapa ni matumizi ya indicators za uchumi. Indicators kama GDP, debt GDP ratio, inflation etc zimekuwa defined na wachumi wa nchi zilizoendelea ambazo zinajitegemea na uchumi wao hauna noise za misaada. Hivyo tunapotumia hizi indicators kwetu ni lazima tutumie data zingine.

  Hapa Marekani watu wanapiga kelele kuwa deni likifikia 10% ya GDP litaumiza vizazi vinavyokuja. Kwanini basi nchi masikini yenye deni lilofikia 33% ya GDP inajifia kwa kulinganisha na nchi zingine masikini. Kwa Tanzania kuwa na deni lililo 33% ya GDP na kutegemea misaada kwa zaidi ya 50% ilibidi nchi iwe kwenye sera za fiscal responsibility.

  Marekani ni nchi iliyoendelea kwanini iwe na wasiwasi na deni lao na nchi kama Tanzania isiwe na wasiwasi wowote? Swali hili peke yake linaonyesha kuwa tunakopa lakini hatuna intentions za kulipa.

  Quantitatively, deni lolote ambalo nchi haiwezi ku-manage ni kitu kibaya sana kwa uchumi na maisha ya watu. Hata kama deni hilo limetumika vizuri, bado litakuwa ni baya tu.

  Kitu muhimu cha kujifunza ni kuwa deni zuri ni lile ambalo lipo manageable. Mtu, taasisi au nchi yenye kutumia mikopo yake vibaya lakini ikaweza ku-manage madeni ziko kwenye nafasi nzuri kuliko nchi inayotumia mikopo yake kwa nia nzuri lakini haiwezi ku-manage madeni.
   
 14. BooSt3D

  BooSt3D Senior Member

  #14
  Sep 1, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 130
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Litalipwa tuu!, Hii Ni Miujiza, Kila siku naskia tunasamehewa madeni, lakini haya madeni hayaishi. Tanzania imeshakuwa Kilema, na kilema hichi tusipoangalia hakitaisha.

  We Have Long way to go My friends, but Together We Can. Tuangalie vizuri turithishe wajukuu na vitukuu nchi nzuri yenye maendeleo + faraja na sio madeni na uchovu.

  B.
   
 15. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Zakumi,

  Najua wanauchumi ni Bin Maryam na Dilunga aka Kuhani, nilikufanyai uchokozi.

  Lakini you are bringing valid points kwenye mfano wako wa Kenya na it seems Watendaji wengi na Watunga sheria wa Tanzanina (Wabunge) wanapitwa na mengi.

  Mimi ningekuwa mwandishi wa habari kwenye huo mkutano wa Sumari, wangenitumia vijana wa Othman na hata TRA "kunisafisha" kwa Udadisi wangu!
   
 16. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Nilikuwa namsubiri companero atokee huku lakini ameingia mitini.
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Sep 1, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Wee subiri tu atakuja tu na hizo nadharia (njozi) zake za kijamaa na kuanza kuuliza miswali kibao....
   
 18. Companero

  Companero Platinum Member

  #18
  Sep 1, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mchungaji nilikuwa safarini huko kwenye vilivyokuwa Vijiji vyetu vya Ujamaa. Kurudi nikajikita kwenye ishu nzito ya Zitto. Ngoja niisome mada kwa undani nije na solutions ambazo 'runaway mjamaa' anaziita 'utopian'!
   
 19. Companero

  Companero Platinum Member

  #19
  Sep 1, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mchungaji nimepitia mada. Naona hiyo ni medani ya wachumi. Mimi nachojua ni kuwa misaada na mikopo ni usanii wa kidola (art of statecraft). Inatumika kuendeleza mfumo wa Kibeberu tu. Tanzania haina sababu ya kukopa. Uwezo wa kujiendesha wenyewe tunao, sababu ya kujiendesha wenyewe tunayo ila nia ya kujiendesha wenyewe ndio hatuna. Kama huamini rejea ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma iliyosomwa Bungeni mwaka huu na Mheshimiwa Zitto Kabwe (MB).

  Zifuatazo ni baadhi ya dondoo kutoka kwenye ripoti hiyo (hii ni mifano michache tu):

  Miaka 7 iliyopita Shirika [TPA] lililipa zaidi ya Shilingi 133 Milioni kwa Kampuni ya Dunhill ili kununua matairi. Kampuni hiyo haikuleta matairi hayo na suala hilo likaenda mahakamani na kesi bado haijaisha. Hata hivyo Shirika limefuta deni hili katika vitabu vya mahesabu!

  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alibainisha tatizo katika mkataba wa gesi kati ya TPDC na Kampuni ya Pan African Energy. Mkataba wa malipo ya kodi ya makampuni (Corporation tax) kati ya TPDC na Pan African Energy Tanzania Ltd una utata mkubwa sana. Katika mkataba huo endapo kodi ya mapato italipwa na Kampuni ya Pan African Energy TZ Ltd, kodi hiyo itafidiwa kutoka kwenye faida ya TPDC. Hii maana yake ni kwamba kampuni hiyo itapunguzwa kutoka kwenye fedha kutoka mrahaba (royalty/remittances) inayolipa serikalini. Ukaguzi unaonesha kwamba kiasi cha Shilingi 2 Bilioni kilipunguzwa kutoka kweye mapato yaliyotakiwa kuwasilishwa serikalini.

  Mgogoro uliopo hivi sasa kati ya TANESCO na IPTL unahusu kiwango cha malipo ya uwekezaji yaani ‚capacity charges’ ambacho IPTL walikuwa wanalipwa na TANESCO. Kwa mujibu wa mkataba kati ya TANESCO na IPTL, ‚capacity charge’ inapaswa kukokotolewa kwa kuzingatia mtaji wa asilimia 30 na mkopo wa asilimia 22.31. Baada ya maamuzi ya mahakama ya kimaTaifa, ilikubalika kuwa mtaji uliowekezwa uwe ni Dola za Marekani 36 Milioni. Hata hivyo baada ya uchunguzi wa TANESCO iligundulika kuwa IPTL haikuwekeza pesa hizo bali waliwekeza Shilingi 50,000 . Mpaka mwezi Mei mwaka 2008, TANESCO imekwishawalipa IPTL jumla ya Shilingi 221 Bilioni toka waanze uzalishaji mwezi Januari mwaka 2002. Ni dhahiri kuwa Taifa limewalipa zaidi (overpay) IPTL mabilioni ya fedha za umma na kwa hivi sasa TANESCO wameacha kuwalipa IPTL na IPTL nao wameacha kuzalisha umeme kwa TANESCO.

  Kama tunaweza kuliwa hivi na kulipa hizi pamoja na vijisenti vingine vingi tu kwa nini tushindwe kulipa madeni yao na kuanza upya kivyetu, yaani, Kiujamaa na Kujitegmea?
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Hii ndio dawa ya kukomesha matumizi mabaya ya serikali. Hatuna huruma na watu maskini. Ni safari, semina na ununuzi wa magari na furniture tu kila kukicha.
  Hatuna displine kabisa na hela za walipa kodi. Kuhusu deni, ni watanzania ndio tunaolipia yote kwa kodi zetu
   
Loading...