Deni la Taifa lapaa!

Deni la Taifa lapaa!

Tanzania received debt relief amounting to $3 billion in 2001 thorough the Heavily Indebted Poor Countries (HIPC) Initiative.

Coupled with improved revenue collections and reduced government expenditure the total debt stock decreased from $10 billion in 2006 to $6 billion in 2007. But as revenue started falling due to the power crisis of 2006 the debt stock started increasing from $7.5 billion in 2008 to the current levels
.

nashindwa kushangaa. Yaani huyu rais...
 
Hakuna cha kukua kwa uchumi ila kinachokuwa nimatumizi. Nakipenda kukisoma kitabu kimoja kilichoandikwa na muhubiri mashuhuri nchini, MWALIMU CHRISTOPHA MWAKASEGE,kisemacho utafanyaje? Wakati matumizi yanapozidi kipato kipato chako? Namshauri jk na mkolo wakinunue kitabu hiki na kukisoma kitawasaidia sana kiuchumi. KUMBUKA MWALIMU Christofa Mwakasege ni mtaalamu wa uchumi.
 
Mkuu, data zinachakachuliwa ili kumdanganya mlalahoi. Ndiyo sababu watu wte wenye "something upstairs" na mzalendo wa kweli, anaichukia hii serikali. Hakuna uchumi kukua hapa. Tunachokifanya ni kujidanganya na consequences za huu uongo ni mbaya sana. Itafika wakati huwezi kudanganya tena kama ilivyo sasa. Polisi wanakatwa pesa, shule za msingi nasikia walimu wakuu wanaitwa wilayani watie saini kuwa wamepokea pesa za MMEM bila kupata chochote, etc,etc. Slaa alisema kuwa it is a tragedy to let the guy rule for the next 5 years! Tunayaona wenyewe kwa macho sasa. Na hii ni miezi miwili tu tka uchaguzi.
 
PatPending,
Maongezeko ya revenue ya serikali ukitia na Inflation Rate unakuta kiukweli 'mapato halisi'' yameshuka. Mfano kama mkate ulikuwa Tshs. 100 mwaka 2009 na mkate huohuo ukauzwa Tshs 500 mwaka 2010 basi pesa ya 2010 haina thamani kama ya 2009 ingawa kitarakimu inaonekana nyingi.

Mkuu, mapato ya nchi yameongezeka hata kama ukizirekebisha namba hizi kwa mfumuko wa bei. Ukichukulia ongezeko la bei la jumla la asilimia 93 kati mwaka 2000/01 na 2007 kama ilivyoainishwa na survey ya bajeti/matumizi ya kaya ya mwaka 2007, na kisha ukacheza na figure za mapato za 2006/07 na 2007/08 utaona ya kwamba kwa bei za mwaka 2000/01 mapato yalikuwa ni bilioni 1419.2 na 1883.2 respectively.

Kama nilivyosema awali deni si tatizo maana kila mtu ana madeni na utetezi mkubwa unatumiwa na serikali ni kwamba wanakopa ili kuwekeza katika miradi ya maendeleo ambayo maturity yake ni ya muda mrefu kidogo (kuna ukweli katika hili na pia kuna ufisadi papa katika hili).

Deni la serikali kuzidi bajeti si kitu cha kutisha maana bajeti huakisi tu uwezo halisi wa serikali katika kutekeleza mipango yake na si uwezo wa taifa zima. Cha kutisha na kusikitisha ni kwamba deni hili (trilioni 15) ni asilimia 60.5 ya pato la taifa kwa mwaka 2008 (Statistical Abstract ya mwaka 2009 toka NBS na MOFEA, p.70) ambalo lilikisiwa kuwa ni trillioni 24.781679.

Ukweli ni kwamba tunahitaji mjadala wa kitaifa wa kuzungumzia madudu kama haya hususani katika kipindi kama hiki ambacho uzalishaji unaathirika na matatizo ya upatikanaji wa nishati, ukiritimba mpevu, miundo mbinu duni (Ni aibu kusema kwamba gharama za kujenga kilometa moja ya lami ni kati ya bilioni 1.2 na 2 wakati barabara zenyewe ni wizi mtupu tu na ilihali maeneo kama US kuna barabara kama vile Pennsylvania Turnpike inayojengwa kwa $736,000 kwa maili (1.6km) ), wizi, na matumizi mengine mabaya ya ridhaa za wananchi
 
Itafika wakati huwezi kudanganya tena kama ilivyo sasa. Polisi wanakatwa pesa, shule za msingi nasikia walimu wakuu wanaitwa wilayani watie saini kuwa wamepokea pesa za MMEM bila kupata chochote, etc,etc.
Na hao nao wanakatwa , nilidhani wao haki zao hazigusiki ndiyo maana wanawaweka sawa walalamikaji.
 
Mkuu, data zinachakachuliwa ili kumdanganya mlalahoi. Ndiyo sababu watu wte wenye "something upstairs" na mzalendo wa kweli, anaichukia hii serikali. Hakuna uchumi kukua hapa. Tunachokifanya ni kujidanganya na consequences za huu uongo ni mbaya sana. Itafika wakati huwezi kudanganya tena kama ilivyo sasa. Polisi wanakatwa pesa, shule za msingi nasikia walimu wakuu wanaitwa wilayani watie saini kuwa wamepokea pesa za MMEM bila kupata chochote, etc,etc. Slaa alisema kuwa it is a tragedy to let the guy rule for the next 5 years! Tunayaona wenyewe kwa macho sasa. Na hii ni miezi miwili tu tka uchaguzi.

MWEEN uko sahihi kabisa, cha mno tuache watu wengi wa feel hii situation ili hata ukiwaambia waweze kuielewa! maanake Dr. Slaa alipokuwa anasema watu walidhani ni uongo! hasa ambao uelewa wao ni mdogo! samahani kwa kutumia neno hilo.
 
OP, Je una nia dhabiti ya kupata jibu la swali lako au una ajenda nyingine? Jibu ni kwamba deni halijaathiri uwezo wa nchi wa kuzalisha na ndio maana limeongezeka ilihali uchumi umekuwa. Hivi ni vitu vya kawaida kabisa hata katika maisha yetu wanadamu, mtu unakuta anaendelea kukopa benki lakini pia huku biashara zake na pato lake linalotokana na uzalishaji likiongezeka.

Mifano mingine mizuri na slightly high profile ni madeni ya makampuni na ukuaji wa uzalishaji na mapato ya hizi kampuni kama vile klabu ya mpira wa miguu ya Manchester United iliyokuja kupata madeni in excess of £768mil ilihali bado ilikuwa kibiashara (i.e mapato na njia mpya za mapato kuongezeka)
 
Mungu alisababisha njaa itokee duniani ili tu Yusuph awe waziri mkuu huko Misri.......Acha uchumi uporomoke tumpate Yusuph wa Tanzania! Mungu si dhalimu ingekuwa hivyo ningeacha siku nyingi ku mwabudu!
 
kuna tofauti kubwa sana ya kikwete na Mkapa, at least mkapa anajua nini maana ya uchumi kikikwe hajui na hapendi kutumia wataalam waliopo kumshauri mambo ya kiuchumi badala yake anawapa marafiki na wakwa zake sehemu muhimu bila kuangalia uwezo ki taaluma
 
Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa! Na bado tu hawa mafisadi wanazidi kukopa na hatimaye wataitumbukiza nchi kwenye mgogoro wa madeni. Hivi ni lini CCM wataacha kuiingiza nchi kwenye matatizo ya kipuuzi kama haya?
 
Tanazania inatia aibu kwa kuwa na deni kubwa la Taifa. Naambiwa na wanahisabati kuwa kwa wastani kila mtanzania anadaiwa si chini ya 490,000/=!!

Ili kujitoa katika aibu hii mimi binafsi niko tayari kulipa sehemu ya deni langu; Viongozi wa Serikali wanielekeze pahala pa kulipa sehemu yanu ya deni.

Mtanzania Halisi
 
Ngoja nikutumie Mpesa urushe sasa hivi...ubarikiwe mkuu...:A S 13:
 
Benki ya dunia ina wasiwasi na deni la taifa kuwa kubwa wakati huohuo Serikali inasema deni bado linakopesheka, hivi Serikali yetu imekosa kabisa namna ya kupata vyanzo vya mapato na kuendesha nchi hadi tuishi kwa kutegemea mikopo ya benki ya dunia?
 
Mikopo yenyewe ya siri baadae wanasema bungen serikali inadaiwa tilion kadhaa wabunge was ccm wanapiga makofi
 
Benki ya dunia ina wasiwasi na deni la taifa kuwa kubwa wakati huohuo Serikali inasema deni bado linakopesheka, hivi Serikali yetu imekosa kabisa namna ya kupata vyanzo vya mapato na kuendesha nchi hadi tuishi kwa kutegemea mikopo ya benki ya dunia?
Vyanzo vya mapato kama vipi ndugu yangu gfesto wakati vyanzo vya mapato kama vile migodi yetu ya madini na maliasili nyingine unazozifahamu wewe zote wamegawana watawala wetu pamoja na ndugu zao???? Hii ndo tanzania zaidi ya uijuavyo wewe...............
 
Mikopo yenyewe ya siri baadae wanasema bungen serikali inadaiwa tilion kadhaa wabunge was ccm wanapiga makofi

Naweza kusema wanapiga makofi pasipo kujitambua kwamba walichaguliwa na wananchi na siyo chama.
 
Migodi tu na rasilimali kama mbuga za taifa na hifadhi vilikua vyanzo tosha sana kuendesha nchi hii. Ila tu kama pangekua na usimamizi madhubuti. Matokeo yake, hela yetu ileile tunayoibiwa hapa inarudishwa kama mkopo/msaada. Tunatawaliwa bila kujua, matokeo yake, anayekupa mkopo anaweza kukupangia atakavyo, kuanzia bei za bidhaa zako nk. Hatuwezi fika hata kdg....
 
Vyanzo vya mapato kama vipi ndugu yangu gfesto wakati vyanzo vya mapato kama vile migodi yetu ya madini na maliasili nyingine unazozifahamu wewe zote wamegawana watawala wetu pamoja na ndugu zao???? Hii ndo tanzania zaidi ya uijuavyo wewe...............

Kweli kaka hawana uchungu na nchi ila maisha yao tu. Wamebaki kupiga kelele na Kagame ile khali Kagame anahangaikia nchi yake. Wao blaablaa ndo kibao!. Eti bajeti ya Serikali inategemea vinywaji, vivuto na mafuta, vingine hamna saana maneno tu ndo yanakuwa mengi.
 
Serikali ya CCM imeshindwa lazima tuipige chini 2015 kama tunataka mabadiliko
 
Tusitegemee mabadiliko kama tuntumia Serikali ileile,chama kilekile na viongozi walewale
 
Back
Top Bottom