Ndio nataka tuangalie vizuri hili deni la nje na deni la ndani..
Mzee Mwanakijiji,
Nakubaliana hii thread ni muhimu kuchangiwa kwa kina, kuhusu masuala ya deni la nje na la ndani.
Kwa Tanzania ni dhahiri kabisa serikali haina lengo (target) iliyojiwekea kuhusu deni la nje na la ndani wala mfumuko wa bei usizidi kiasi fulani kwa mwaka wowote wa fedha. Ndiyo maana vitu muhimu kwa mahitaji ya mtanzania kama vyakula, nishati n.k huwa vinapaa huku serikali ikiwa haistuki na pia deni la ndani na nje lilizidi kukua kwa kasi zaidi!
Nini kifanyike:
kwanza
Mimi nadhani Benki ya Tanzania pamoja na gavana wake wapewe mamlaka kamili ya kufanya kazi zao bila kuingiliwa na serikali hapa sheria ipitishwe kukazia jambo hili. BoT wawe wanatoa taarifa zao za kitaalamu bila kuchakachuliwa na serikali.
Pili
Waziri wa fedha pia awe ni mtu ambaye pia ana mamlaka kamili ya kazi yake, akiona pesa zinataka kufujwa bila bajeti iliyopangwa ambayo imepitishwa bunge, waziri wa fedha awe na mamlaka kamili ya kukataa kuburuzwa na wakubwa wake. Ikiwa waziri wa fedha anadhani hasikilizwi basi awe mwepesi kujiuzulu kama alivyofanya Mzee Edwin Mtei walipotofautiana ki-sera na Mwalimu Nyerere. ( hapa Waziri wa fedha angetoka kambi ya upinzani na siyo chama tawala).
Tatu
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu wa serikali (CAG) awe anatoa ripoti kuelezea matumizi ya serikali kufuatana na dhana ya 'Value for Money' yaani matumizi yenye manufaa. Mfano
-
magari ya mashangingi hayana 'value for money' ktk matumizi ya serikali.
- safari nyingi za kiserikali mikoani au nje ya nchi iwe za kirafiki, makongamano, kujifunza, kujitambulisha hazina 'value for money' ktk matumizi ya serikali
- vyeo kama vya DC( district commissioner) ni kuiingiza serikali ktk matumizi yasiyofaa.
Nne
Mambo hayo hapo juu hayawezi kutekelezwa na serikali za CCM iwe ya awamu ya IV au ya VI, hivyo utawala mpya kabisa nje ya CCM ndiyo unaweza kutekeleza mambo namba mmoja mpaka tatu hapo juu.
Kwa faida ya majadiliano nimeweka kazi kuu za Benki ya Uingereza hapa chini:
BANK OF ENGLAND
Core Purposes - Monetary Stability
Price stability and monetary policy
The first objective of any central bank is to safeguard the value of the currency in terms of what it will purchase at home and in terms of other currencies. Monetary policy is directed to achieving this objective and to
providing a framework for non-inflationary economic growth. As in most other developed countries, monetary policy operates in the UK mainly through influencing the price at which money is lent, in other words the interest rate.
The Bank's price stability objective is made explicit in the present monetary policy framework.
It has two main elements: an annual inflation target set each year by the Government and a commitment to an open and accountable policy-making regime.
Setting monetary policy - deciding on the level of short-term interest rates necessary to meet the
Government's inflation target - is the responsibility of the Bank.
In May 1997 the Government gave the Bank operational independence to set monetary policy by deciding the short-term level of interest rates to meet the Government's stated inflation target - currently 2%.'' Bank of England | About the Bank | Core Purposes | Monetary Stability