Deni la Taifa lafika Tril. 52/-

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
SERIKALI imesema hadi kufikia Agosti mwaka huu, Deni la Taifa lilifikia Sh. trilioni 52.303 kulinganishwa na Sh. trilioni 49.283 katika kipindi cha Agosti, mwaka jana.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango, aliyasema hayo jana bungeni jijini Dodoma, alipowasilisha mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21.

“Deni la serikali hadi Agosti 2019, lilifikia Sh. bilioni 52,303.04 ikilinganishwa na Sh. bilioni 49,283.44 Agosti 2018," Dk. Mpango alisema.

Kiwango hicho ni sawa na ongezeko la Sh. trilioni tatu katika kipindi cha mwaka mmoja.

Waziri huyo alibainisha kuwa kati ya deni hilo, Deni la Ndani lilikuwa Sh. trilioni 14.075 na Deni la Nje Sh. trilioni 38.227, akieleza kuwa ongezeko la deni lilichangiwa na kupokewa kwa mikopo mipya kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Desemba mwaka jana, ilionyesha Deni la Serikali bado ni himilivu katika muda mfupi, wa kati na mrefu kwa viwango vya kimataifa.

Dk. Mpango alisema serikali inaendelea kuhakikisha deni linakuwa himilivu kwa kuhakikisha mikopo inayokopwa inaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo yenye tija kwa taifa.

Kuhusu mwenendo wa viashiria vya uchumi, Dk. Mpango alisema uchumi wa taifa umeendelea kuwa imara, akibainisha kuwa katika kipindi cha muongo mmoja uliopita (2009 – 2018), Pato halisi la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 6.4 kwa mwaka.

Alisema mwenendo wa thamani ya shilingi uliendelea kuwa tulivu katika kipindi cha mwaka unaoishia kipindi cha Agosti 2019, kwamba Dola moja ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa Sh. 2,289.1 ikilinganishwa na wastani wa Sh. 2,273.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2018.
Kuhusu maandalizi ya mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka 2020/21, Dk. Mpango alisema matumizi ya serikali yanakadiriwa kuongezeka hadi Sh. trilioni 34.36, sawa na asilimia 21.7 ya Pato la Taifa kutoka Sh. trilioni 33.105 mwaka 2019/20.

Alisema matumizi ya kawaida pia yanakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 4.7 hadi Sh. trilioni 21.660, sawa na asilimia 13.7 ya Pato la Taifa na matumizi ya maendeleo yanakadiriwa kuwa Sh. trilioni 12.699, sawa na asilimia nane ya Pato la Taifa.

Alisema mwaka 2020/21, mapato ya ndani (yakijumuisha mapato ya halmashauri) yanakadiriwa kuongezeka hadi Sh. trilioni 23.456 mwaka 2020/21 kutoka makadirio ya Sh. trilioni 23.045 mwaka 2019/20 na kukadiriwa kuongezeka kwa wastani wa asilimia 8.8 katika muda wa kati.

"Uwiano wa mapato ya ndani kwa mapato yote unatarajiwa kuongezeka kutoka asilimia 68.3 ya bajeti ya mwaka 2020/21 hadi asilimia 73.7 mwaka 2022/23.

Mapato ya kodi yanakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 4.3 hadi Sh. trilioni 19.761 mwaka 2020/21 kutoka Sh. trilioni 18.955 mwaka 2019/20 na kukua kwa wastani wa asilimia 8.9 katika muda wa kati.

"Mapato yasiyo ya kodi (yakijumuisha mapato ya halmashauri) yanakadariwa kuwa Sh. trilioni 3.601 mwaka 2020/21 na kuongezeka kufikia Sh. trilioni 4.34 mwaka 2022/23,” Dk. Mpango alisema.

Mtaalamu huyo wa uchumi alisema mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2020/21 yameandaliwa kwa kuzingatia maeneo manne ya kipaumbele ambayo ni ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda, kufungamanisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu, ujenzi wa mazingira wezeshi kwa uendeshaji wa biashara na uwekezaji pamoja na kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa mpango.

Naibu Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, David Silinde, akisoma maoni ya upinzani kuhusu mapendekezo ya mpango huo umefeli kwa kuwa unaingia sasa mwaka wa mwisho wa utekelezaji wake ilhali malengo yake makubwa hayajafikiwa hata robo.

Alisema lengo kuu la Mpango wa Pili lilikuwa kuhakikisha Tanzania inaingia katika uchumi wa kipato cha kati.

Silinde ambaye pia ni Mbunge wa Momba (Chadema), alisema serikali inapaswa kujipima kama imefikia lengo hilo.

CANCELFORWARD 1 DELETE 1 REPORT 1 REPLY
 
Bado tunakopesheka... Acha tu akenue kwa kicheko cha furaha
IMG-20191105-WA0075.jpeg
 
Hilo ndio tatizo la kufanyia research ofisini badala ya field....hizo takwimu za pato la taifa zimepikwa lakini hazijaiva. Iweje pato likuwe wakati huohuo ugumu wa maisha umeongezeka kwa raia? Kama pato/uchumi unakua, ni kwanini serikali inaendelea kukopa mabilioni ya dola kila uchwao?
 
Haya made ya taifa waga siyaelewi kabisa
Maana ata USA deni lao ni kama uchumi wao wote
Yani wana deni la dolla trilion 22 akat uchumi wao ni dollar trilion 23
 
Hapa tunaambiwa deni linaongezeka kwa sababu ya mikopo iliyochukuliwa ili kutekeleza miradi. Halafu kuna watu wakisimama jukwaani bila aibu wanasema tunatekeleza miradi kwa pesa zetu.

Yaan hayo wanayosema wamekopa Kwa akili ya kufanya shughur za maendeleo ya Nchi....!!
1)hayo maendeleo ni yap.?
2) je zile hela ambazo Mtukufu Rais wetu anasema niza wanyonge na zinafanya shughur za maendeleo zimefanya maendeleo yapi? na hiizo zilizokopwa zimefanya yapi?
 
Hayo madeni yafanyiwe uhakiki kuendana na matumizi ambayo zimefanyia,endapo gharama za miradi hazitoendana na thamani ya fedha,basi kiasi kilichoibwa na kutiwa mifukoni wagawane kulipa washiriki wote wa uchafu huo..
 
Hilo ndio tatizo la kufanyia research ofisini badala ya field....hizo takwimu za pato la taifa zimepikwa lakini hazijaiva. Iweje pato likuwe wakati huohuo ugumu wa maisha umeongezeka kwa raia? Kama pato/uchumi unakua, ni kwanini serikali inaendelea kukopa mabilioni ya dola kila uchwao?
Swali lako likijibiwa nitag
 
Hapa tunaambiwa deni linaongezeka kwa sababu ya mikopo iliyochukuliwa ili kutekeleza miradi. Halafu kuna watu wakisimama jukwaani bila aibu wanasema tunatekeleza miradi kwa pesa zetu.

Ni hela zetu ndio maana tumekopa na sio kwamba tumepewa bure.
Ni sawa na mimi nikukopeshe hela unataka uniambie hapo hizo pesa zitakuwa za kwangu au za kwako?
 
Eti pesa zenu. Hivi unaelewa maana ya hii kauli? "Tunajenga kwa pesa zetu za ndani"
 
Ni za kwetu ndio si tutazirudisha? Au mimi ndio sijui maana ya kukopa.

Ingekuwa tumepewa kama msaada hapo ningesema kweli hizo pesa sio za kwetu ila hiyo ya kukopa mzee aaaah! Hizo ni pesa zetu
 
Back
Top Bottom