Paul Mabuga
Member
- Nov 25, 2010
- 10
- 2
Kesho katika kipindi cha Tuongee Asubuhi Star TV pamoja na Wageni wangu nitajadili uhalali wa Serikali kukopa kwenye Benki za Biashara.
Hadi sasa kulingana na ukubwa wa deni la Taifa kila mtanzania ana deni la shilingi 332,000/=
na kama bajeti ya 2010/11 itakwenda kama ilivypangwa deni hili litaongezeka kwa shilingi 54,000 na hasa baada ya seriklai kukopa kwenye Benki za Biashara.
Lakini pia katika kila shilingi moja ambayo TRA wanakusanya katika mapato ya kodi na yale yasiyo ya kodi serikali inatumia shilingi 1.90 (Kwa mujibu wa taarifa ya TWAWEZA) na hivyo kulazimika kukopa ama kupata msaada wa senti tisini katika kila shilingi.
Je kuna uhalali wa serikali yetu kukopa! Athari za yote haya ni nini katika huduma na hususani kwa mwananchi wa kawaida! Je walitupa sababu za maana kutuingiza katika changamoto hizi?
Wana JF naomba michango!