Deni la Taifa; Kila Mtanzania anadaiwa 332,000/- na litaongezeka kwa 54,000/= 2011

Paul Mabuga

Member
Nov 25, 2010
10
2
Kesho katika kipindi cha Tuongee Asubuhi Star TV pamoja na Wageni wangu nitajadili uhalali wa Serikali kukopa kwenye Benki za Biashara.

Hadi sasa kulingana na ukubwa wa deni la Taifa kila mtanzania ana deni la shilingi 332,000/=
na kama bajeti ya 2010/11 itakwenda kama ilivypangwa deni hili litaongezeka kwa shilingi 54,000 na hasa baada ya seriklai kukopa kwenye Benki za Biashara.

Lakini pia katika kila shilingi moja ambayo TRA wanakusanya katika mapato ya kodi na yale yasiyo ya kodi serikali inatumia shilingi 1.90 (Kwa mujibu wa taarifa ya TWAWEZA) na hivyo kulazimika kukopa ama kupata msaada wa senti tisini katika kila shilingi.

Je kuna uhalali wa serikali yetu kukopa! Athari za yote haya ni nini katika huduma na hususani kwa mwananchi wa kawaida! Je walitupa sababu za maana kutuingiza katika changamoto hizi?

Wana JF naomba michango!
 
Ili kujikwamua ushauri wako kwa Serikali ni upi? Hili deni la TShs.332,000 ni pamoja na watoto na wagonjwa?
 
Yaani kila mtu kulingana na hao watafiti na wachambuzi wa matumzi ya rasilimali za umma

Wengine hatupendi kudaiwa, waambie watupe Akaunti namba wasiopenda kudaiwa watalipa madeni yanayolingana na idadi ya watu walio katika familia zao
 
Hii kali ngoja nifikiri lakini kwenye mapato ya madini peke yake yakitumika effective hilodeni litalipwa kwani kwe almasi tu kuna ufisadi balaa hadi unaweza kulia.
 
Kupanga ni kuchagua. Kila mara nawahimiza wenye watoto wawafundishe watoto wao jinsi ya kuishi within a budget tangu wakiwa wadogo shuleni maana huku ndiko tatizo linakoanzia.Tatizo la viongozi wetu wamekaa kufikiri kuna mzungu atakuja kesho kuwaletea furushi la hela so they keep spending bila kujali wamengiza nini. Huu ni ugonjwa wa kitaifa ambao kizazi hiki lazima kipambabe kuumaliza na ni kwa njia ya kuwafunza vijana wetu kuishi kwa bajeti tu ndio tutataua hili tatizo vinginevyo ni kujisumbua. Aina ya viongozi tulionao kwa sasa hawana wanachoweza kufanya kupunguza hili deni maana tayari wana mlolongo wa ahadi kwa wapiga kura wao ambazo itabidi wazitekeleze hata ikiwa ni lazima kukopa. Hali hii ukijumlisha na matumizi yao yasio na udhibiti inakuwa mzigo wa msalaba kwa masikini wa Tanzania. Cha kufanya ni kuithibiti serikali isitumie zaidi ya inavyo kusanya...lakini how? Wao ndio kila kitu. It's pathetic
 
Tunajua kwamba serikali inaingia katika madeni kwa kujitakia? Si kwamba serikali haijui kwamba ni makosa kukopa bila ya kuwa na mkakati ambao mkopo huo utatumika kuongeza uzalishaji, ajira, uwekezaji wa ndani ambapo serikali itaongeza ile Tax base yake ili kupata fedha zaidi za kulipa madeni na ziada kuendesha shughuli muhimu za serikali.

Ni kwanini serikali yetu haifanyi hivyo? Sababu kubwa ni kwamba endapo fedha zitatumika vizuri kukuza uchumi watakaonufaika ni watanzania wa kawaida na hilo sidhani kama serikali yetu inapenda kuona linatokea badala yake wanakopa na kufanya biashara za ununuzi wa vitu (consumer goods) kutoka nchi za nje ambazo haziongezi pato la taifa. Badala yake kama serikali ingejikita katika kununua productive goods tungeongeza uzalishaji ndani ya nchi ambao ungeleta ajira na kuongeza pato la taifa kwa uzalishaji na utumiaji wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi.

Serikali ingelijaribu kufanya jambo kama hili-vijana wa kitanzania wanaomaliza Highway, Civil Engineering katika chuo cha Dar peke yake wanaweza kufikia mia au pungufu kidogo kwa mwaka. Vijana waliofanya vizuri katika fani hizo wangalijengewa uwezo wa kiutawala na kiutengaji na kuwezeshwa na serikali kwa kupewa mitaji na usimamizi wangeliweza kuingia katika biashara ya kutengeza mabarabara yetu, kuingia katika sekta ya ujenzi wa majengo makubwa na madogo tunayoona yakiongezeka kila siku na kwa kufanya hivyo ukopaji wa serikali ungekuwa wa TIJA. Tungeongeza ajira, matumizi ya bidhaa za ndani kama cement, na vinginevyo, watu wangepata pato la kununua bidhaa zinginezo kutokana na ajira. Lakini kwa kukosa akili tunakopa halafu tunawapa wachina(Mfano kampuni ya China Railway) fedha zetu wananunua mitambo kutoka kwao faida inakwenda kwao sisi tunabaki watupu? Tuendelee kulipia madeni mpaka vitukuu vyetu endapo tutashindwa kumwajibisha mkwere na wenzake hiyo ndiyo hatma yetu watz>
 
Ili kujikwamua ushauri wako kwa Serikali ni upi? Hili deni la TShs.332,000 ni pamoja na watoto na wagonjwa?

Nimefurahi kukutana na wewe, kabla sijachangia naomba sana unambie kama this time utakua upande upi kwani mimi binafsi sikupendezwa na jinsi mnavyoi-defend CCM kwenye mijadala yenu!!! haya nitakupa kampani kimtindo ila hilo deni ni tofauti na la PEDP na SEDP maana kuliko nako tunadaiwa, ni deni lile tunatakiwa tulipe, uligusie nalo hilo!!
 
Kesho katika kipindi cha Tuongee Asubuhi Star TV pamoja na Wageni wangu nitajadili uhalali wa Serikali kukopa kwenye Benki za Biashara.

Hadi sasa kulingana na ukubwa wa deni la Taifa kila mtanzania ana deni la shilingi 332,000/=
na kama bajeti ya 2010/11 itakwenda kama ilivypangwa deni hili litaongezeka kwa shilingi 54,000 na hasa baada ya seriklai kukopa kwenye Benki za Biashara.

Lakini pia katika kila shilingi moja ambayo TRA wanakusanya katika mapato ya kodi na yale yasiyo ya kodi serikali inatumia shilingi 1.90 (Kwa mujibu wa taarifa ya TWAWEZA) na hivyo kulazimika kukopa ama kupata msaada wa senti tisini katika kila shilingi.

Je kuna uhalali wa serikali yetu kukopa! Athari za yote haya ni nini katika huduma na hususani kwa mwananchi wa kawaida! Je walitupa sababu za maana kutuingiza katika changamoto hizi?

Wana JF naomba michango!

Karibu mkuu nashukuru umeingia hapa, huwa nakukubali kwa kujitahidi kuwa objective katka komments zako, endelea hivyo hivyo. michango hapa ndo nyumbani ila uwe mvumilivu vile vile!

Nimeipenda topic ila sitaki kukurupuka kuijibu ngoja niingie msituni ili nikiridi nije kiutu uzima!
 
Licha ya deni la taifa kuongezeka na kufikia Sh27 trilioni mwaka jana, Serikali imesema bado ina sifa za kuendelea kukopa kutokana na mapato ya ndani kuwa madogo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya alisema jambo linalozingatiwa na Serikali ni kuhakikisha fedha za mikopo zinatumika kwa shughuli za kukuza uchumi.

“Deni la taifa linajumuisha deni la Serikali kutoka vyanzo vyake vya mapato ya ndani na nje ya nchi pamoja na deni la nje ambalo Serikali imelidhamini kwa sekta binafsi,” alisema Mkuya.

Alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana, deni la taifa lilifikia Sh27 trilioni, kati ya kiwango hicho deni la nje ni Sh20.2 trilioni na ndani ni Sh6.8 1 trilioni, huku deni la nje la sekta binafsi likifika Sh3.5 trilioni.

“Tunaendelea kukopa na deni linaongezeka. Linaongezeka kwa mikopo inayochukuliwa na ile ambayo haijalipwa,” alisema.

Akitaja sababu za kuongezeka kwa deni hilo alisema: “Linaongezeka kwakuwa nchi bado inaendelea kukopa, kuendelea kuwepo kwa madeni ya nyuma kutokana na muda wake wa kuyalipa kutofika, kuongezeka kwa watu na shughuli za kiuchumi pamoja na kuwepo kwa madeni ambayo kwa mujibu wa mikataba yanatakiwa kusamehewa.”

Alisema kutokana na kuwepo kwa orodha ndefu ya nchi zinazokopa, hivi sasa Tanzania imejikita zaidi katika kukopa mikopo yenye masharti ya kibiashara ambayo ni tofauti na mikopo yenye masharti nafuu.

Hata hivyo, Mkuya alisema kila mwaka Serikali inafanya tathmini kama inaweza kuhimili deni kutokana na shughuli za kiuchumi ndani ya nchi. “Tathmini ya mwisho tumefanya Septemba mwaka jana, haifanywi na Serikali pekee, inahusisha pia Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) na Benki ya Dunia (WB),” alisema Mkuya.

Waziri huyo alivitaja viashiria vinavyoonyesha kuwa nchi ina uwezo wa kuhimili deni kuwa ni thamani ya deni la nje ikilinganishwa na uchumi wa nchi (GDP),”

“Deni la nje sasa hivi ni asilimia 25 ambayo ni sawa na asilimia 24.8 ya uchumi wa nchi. Lakini ukomo wa kukopa kwa kutumia kiashiria hiki ni asilimia 50 ya deni, hivyo bado tuna vigezo vya kukopa maana tupo katika asilimia 24.”

Alisema thamani ya leo la deni lote la taifa kwa uchumi wa nchi ni asilimia 40.5 na kwamba ukomo wake ni asilimia 74.

“Lakini hilo halitufanyi kukopa zaidi, ila kutokana na hali ya uchumi tutakopa katika vyanzo nafuu,” alinena

MY TAKE
27trillion/45,000,000tanzanian =600,000/= kila mtu pamoja na watato hatari sana hii.

Karibu mkuu nashukuru umeingia hapa, huwa nakukubali kwa kujitahidi kuwa objective katka komments zako, endelea hivyo hivyo. michango hapa ndo nyumbani ila uwe mvumilivu vile vile!

Nimeipenda topic ila sitaki kukurupuka kuijibu ngoja niingie msituni ili nikiridi nije kiutu uzima!
Mkuu hujatoka tu msituni tangu 2010?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom