Demokrasia ndani ya CCM imekwenda wapi?

Demokrasia ndani ya CCM imekwenda wapi?

adui yako mpende bial tatizo na kinachotia huruma ni mweleka wa mende miguu juu.
 
Kuna maswala mawili ya kujadili hapa:
  1. Ama ndugu hawa wa viongozi wa CCM ni very bright na hivyo kuwapiku wapinzani wao wengi katika uchaguzi; au
  2. Wana CCM wanaathirika kiakili na busara pindi wanapokutana na majina ya vigogo wao katika uchaguzi.

Tafakari!
 
Kitu chochote hapa ulimwenguni kikifikia mwisho hapana jinsi ya kukifufua na cha kushangaza kila utakapozidi kukiamsha ndivyo utakapozidi kukipoteza,maana waliopo kwenye hicho kitu huwa hawazioni kasoro zilizowazunguka.
 
CCM imeshaoza sasa sio kunuka!

CCM hakuna tena waasisi ambao wanaweza kukemea uozo wa kukifanya chama mali ya familia ya Kikwete; wakina Kisumo sio kama walivyokuwa wakina Rajab Diwani, Masudi Mtandika na Enos Mwangoka. Hawa waliobaki wote wamenunuliwa na wenye fedha na wao wamekuwa madalali hivyo hawawezi kukemea uoza wa chama!!
 
Soma signature hapaaaaaaa....

Wenzio tunatembea na NDIZI na PILIPILI tukiskia tu kuna hitma ya CCM tunaenda kula wali,,, kimsingi tumekaa mkao wa kula
 
George Bush, Snr
George Bush, Jr

Jamani, sio Tanzania tu. Ukweli utabaki kuwa wanasiasa huwaandaa watoto wao kushika uongozi tangia wakiwa wadogo. Watoto nao huanza kuona raha ya uongozi wakiwa wadogo, na hivyo hupania kuwa viongozi ili kuendeleza "utajiri" wa wazazi wao.

Samahani nikisema kuwa, hata vyama vingine vya siasa havitaepa kawaida hii. Mjadala hapa ni je wamepatikana "by merits" na kwa njia zilizo wazi na bila upendeleo? Mfano, CHADEMA tunao wabunge wawili Nyerere na wawili Lisu, je hilo ni kosa? Binafsi sioni kama ni kosa, ili mradi wamepatikana kwa "merits" zao na kwa vigezo vilivyo sahihi.

Hata hivyo, haipendezi kuona msululu wa viongozi katika chama au katika serikali wanatoka katika familia moja, na hasa kama hawana uwezo zaidi ya wengine. Ninaona huu ni mtihani mkubwa kwa CHADEMA katika chaguzi tunazozitegemea ndani ya chama. Nitasikitika sana kama CHADEMA kitaingia katika mtego wa "undugu".
 
Kuna maswala mawili ya kujadili hapa:
  1. Ama ndugu hawa wa viongozi wa CCM ni very bright na hivyo kuwapiku wapinzani wao wengi katika uchaguzi; au
  2. Wana CCM wanaathirika kiakili na busara pindi wanapokutana na majina ya vigogo wao katika uchaguzi.

Tafakari!

tunaweza kusema imperialism regime,that watu wana rithishana madaraka.Huu ni mpango kabambe kuweza kuwaandaa watoto wa vigogo kuchukua madaraka na kuficha uchafu na madhambi ya wazazi wao.Ndo maana hata ile dhanma ya kuwafanya vijana kama dodoki kwa kuwasafishia njia walafi inahitaji kuangaliwa mara mbili mbili
 
kuna siku niliwahi kuwaeleza CDM wasije wakabweteka na umati wa wanachama wanaoingia baada ya majeraha ndani ya CCM.Lakini fimbo inayotumika kupigia nyoka iangaliwe kwa makini isije ikawa bakora mujarabu kuwa wachapa wapinzani kwa kubweteka mara baada ya kuona wao ndiyo kimbilio la wanyonge na hakuna mbadala.
 
hata ule utaratibu wa kubadilisha kanuni ili ujumbe wa NEC ugombewe wilayani ilikuwa ni mkakati wa kuhakikisha kila kigogo anweka mwanae NEC he heh heh eh... Manna wangegombea kwa utaratibu wa zamani wasinge sinda kihivyo.

Pia mbona wengine umewasahau wanakuja kupitia kapu la dodoma ndio wameachiwa huko maana baba, ndugu au wao wenyewe ndio wanasimamia matokeo na uchaguzi huo wa DOM so lazima wajipitishe...nao ni...

malima....
makamba..
mwinyi mwingine...
kawawa...
ila hautasikia nyerere maana ni mwiba kwao ukoo huo
 
hata ule utaratibu wa kubadilisha kanuni ili ujumbe wa NEC ugombewe wilayani ilikuwa ni mkakati wa kuhakikisha kila kigogo anweka mwanae NEC he heh heh eh... Manna wangegombea kwa utaratibu wa zamani wasinge sinda kihivyo.

Pia mbona wengine umewasahau wanakuja kupitia kapu la dodoma ndio wameachiwa huko maana baba, ndugu au wao wenyewe ndio wanasimamia matokeo na uchaguzi huo wa DOM so lazima wajipitishe...nao ni...

malima....
makamba..
mwinyi mwingine...
kawawa...
ila hautasikia nyerere maana ni mwiba kwao ukoo huo

Makongoro Nyerere aliwahi kuwashukurun wabunge wa CDM akisema yeye hakuwa na pesa za kuwahonga wabunge ili wamchague,alifika mbali zaidina kufunguka kwa kusema alimuomba Mungu usiku na mchana kuhakikisha ana legeza mioyo ya wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni vinginevyo ubunge huo angeusikia kwenye Luninga.
 
Pasipo kuchukuwa hatua sasa wakati wa uchaguzi wa ndani ya chama hakutakuwa na namna ya kurekebisha wakati wa uchaguzi mkuu ujao 2015.

Rushwa si ya kuichekea hata kidogo!!


Kinachofanyika hivi sasa ni ile methali ya wazee wa kale sikio la kufa halisikii dawa.
 
Back
Top Bottom