kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,315
- 12,614
Angalia nyumbani kwenu, nyumbani kwako na kwenye familia yenu kama kuna demokrasia ya kiasi gani? Je, wazazi wamewapa watoto demokrasia ya kusema, kutenda na kuamua kiasi gani? Je, baba anaruhisiwa kumuoa mtoto wake? Je, baba anaweza kuvumilia matusi ya mtoto wake? Je, Binti anaweza kumleta boyfriend wake kwa wazazi bila shida? Je, mtoto anaweza kulala chumba cha wazazi wake? Je, watoto wanaweza kujivalia nguo yoyote? Je, mke na watoto wanarudi nyumbani muda wowote?
Demokrasia inaanzia ngazi ya familia. Demokrasia ni kama lugha, lugha isiyozungumzwa nyumbani kwenye familia haiwezi kuzungumzwa vizuri kwenye ngazi ya taifa; na demokrasia isiyotendwa kwa ufasaha kwenye ngazi ya familia haiwezi kutendwa kwa ufasaha kwenye ngazi ya kitaifa.
Ndiyo maana hutuwezi kuvumilia demokrasia ya kutukanana kwenye majukwaa kwakuwa huo sio utamaduni wetu huko majumbani tulikolelewa na tulikozaliwa na kukulia.
Maana majumbani hakuna demokrasia, chekechea hakukua na demokrasia, miaka 7 ya shule ya msingi hakukua na demokrasia shuleni, miaka 4 ya secondary hakuna demokrasia, miaka 2 ya A level wanafumzi hawana demokrasia na hata vyuoni hakuna demokrasia ya kusema, kuvaa, kunyoa, Wala kuahirisha mtihani, hivyo hata majukwaani hakuwezi kuwa na demokrasia pana kiasi hicho cha kuporomosha matusi hadharani bila kuulizwa ulitoa wapi hilo.
Tusiwe kama dodoki zoazoa wa demokrasia ya Magharibi na kuleta Huku kwetu kama ilivyo wakati background zetu ni tofauti sana na zao. Demokrasia ya Wazungu imeanzia kwenye ngazi ya familia, watoto wao hawana acha (don't) nyingi kama watoto wetu. Think globally and act locally.
Mwanasiasa msomi lazima analijua hili, kama ukimuona anatukana hadharani viongozi wake lazima analo lingine moyoni na kichwani zaidi ya siasa na demokrasia. Tumvunje kichwa chake mapema kabla hajavunja vichwa vyetu sote.