Demokrasia na maendeleo: Tusipotoshe ushahidi wa kisayansi

nchiyetutztz

Member
Oct 29, 2018
13
12
Upotoshaji mkubwa kwa baadhi ya posts hapa jamii forum unaendelea. Ushahidi wa kisayansi (credible scientific/empirical evidence) unaonyesha kuwa bado hakuna muafaka kwenye mahusiano ya moja kwa moja kati ya haya mawili. Robo tatu ya tafiti zimethibitisha demokrasia inachangia maendeleo.

Robo tatu ya tafiti pia inaonyesha demokrasia haichangii maendeleo, na robo tatu iliyobaki inaonyesha hakuna mahusiano kati ya haya mawili (insignificant correlation). Kwa hiyo haya mahusiano bado ni ‘highly contested debate’ kwenye scientific society.

Lakini kitu ambacho ushahidi wa kisayansi uko "solid" ni kuwa hata kama kukua kwa uchumi kutapatikana ndani ya authoritarian regimes (kukosekana kwa demokrasia) ukuaji huo utakuwa unasumbuliwa na frequent boom and bust kuliko mazingira yanayotawaliwa na demokrasia.

Ushahidi pia unaonyesha kuwa ni vigumu kwa democrasia kuwa sustained kwenye mazingira ya kipato cha chini/umaskini kuliko kwenye mazingira ya kutokuwepo kwa umaskini. Nahitimisha kwa kusema: Tutaisaidia sana nchi yetu (in the medium and long run) kwa malumbano yetu kujikita zaidi kwenye sayansi na kuepuka hisia na ushabiki.
 
Hakuna Nchi yoyote duniani (zaidi ya City States) iliyowahi kuendelea kwa sababu ya kukumbatia demokrasia, isipokuwa kinyume chake. Hakuna Nchi yoyote duniani iliyoshindwa kuingia kwenye demokrasia baada ya ku-undergo maendeleo ya kiuchumi, full stop.
 
Your assertion has no backings
 
Hakuna Nchi yoyote duniani (zaidi ya City States) iliyowahi kuendelea kwa sababu ya kukumbatia demokrasia, isipokuwa kinyume chake. Hakuna Nchi yoyote duniani iliyoshindwa kuingia kwenye demokrasia baada ya ku-undergo maendeleo ya kiuchumi, full stop.
Ukiweza kutofautisha kati ya journalistic articles/arguments na scientific articles/arguments ungenielewa,,,, pia tofautisha kati ya political liberalisation na democracy,,,,, point yako ya mwisho ni dhaifu sana na kithibitisho cha nilichoeleza - tatizo la kujibu hoja kwa hisia,,, jiuliza China baada ya ku-undergo maendelea ya kiuchumi imeingia kwenye democracy?
 
Kuna watu wamejijengea uelewa potofu kuwa demokrasia ni sawa na anarchy (uholela/ vurugu/ ukosefu wa nidhamu). Kwa hawa watu nasema pole sana - siyo kosa lao bali ni mfumo wetu wa elimu.

Falsafa za Adam Smith, ambazo ni msingi wa uchumi endelevu katika nchi zinazofuata demokrasia, unajikita katika dhana ya uhuru wa mtu binafsi, na uhuru wa watu kutafuta na kuhodhi mali/ utajiri kwa kadhri ya uwezo wao. Hizi falsafa zinatafakari kuwa kila mtu akijituma kutafuta utajiri, basi nchi kwa ujumla nayo inaneemeka. Ni kutokana na uhuru huu wa mtu binafsi tunapopata utaratibu wa utawala wa kidemokrasia, ambao nia yake ni kuwezesha watu huru ku-influence wanavyotawaliwa, ili isije ikatokea tawala dhalimu itayoingilia uhuru wa watu binafsi.

Katika utaratibu wa demokrasia, nguvu zote zinatokana na ridhaa ya watu huru. Hakuna mtu atayepewa uwezo juu ya wenzake bila idhini ya watawaliwa. Hakuna sheria itayopitishwa bila idhini ya watawaliwa.

Pole sana kama haujaelewa, siyo kosa lako. Hebu nikupe haka ka video labda utaelewa kidogo, jap[o nako ni ka kisomi somi;
 
Attachments

  • Morality Markets - Man of Systems.mp4
    16.6 MB · Views: 14
Hizo robo tatu ukizinguanisha zinazidi asili ambayo ni 1.Hesabu za wapi hizo?
Kumbe na wewe umeliona hilo kosa.
Au alimaanisha moja ya tatu (1/3) au theluthi moja kwa lugha nyingine.

Ukifanya moja ya tatu(theluthi) ukijumlisha hizo zote ndio utapata asilimia mia moja yani kitu kamili.
 
Umejiunga jana huo upotoshaji umeusoma wapi?!

Huyu jamaa alietoa haya maoni anaakili sana za kusoma na kuelewa hakika waelewa hawapo siasani

Kuna watu wamejijengea uelewa potofu kuwa demokrasia ni sawa na anarchy (uholela/ vurugu/ ukosefu wa nidhamu). Kwa hawa watu nasema pole sana - siyo kosa lao bali ni mfumo wetu wa elimu.

Falsafa za Adam Smith, ambazo ni msingi wa uchumi endelevu katika nchi zinazofuata demokrasia, unajikita katika dhana ya uhuru wa mtu binafsi, na uhuru wa watu kutafuta na kuhodhi mali/ utajiri kwa kadhri ya uwezo wao. Hizi falsafa zinatafakari kuwa kila mtu akijituma kutafuta utajiri, basi nchi kwa ujumla nayo inaneemeka. Ni kutokana na uhuru huu wa mtu binafsi tunapopata utaratibu wa utawala wa kidemokrasia, ambao nia yake ni kuwezesha watu huru ku-influence wanavyotawaliwa, ili isije ikatokea tawala dhalimu itayoingilia uhuru wa watu binafsi.

Katika utaratibu wa demokrasia, nguvu zote zinatokana na ridhaa ya watu huru. Hakuna mtu atayepewa uwezo juu ya wenzake bila idhini ya watawaliwa. Hakuna sheria itayopitishwa bila idhini ya watawaliwa.
 
Umejiunga jana huo upotoshaji umeusoma wapi?!

Huyu jamaa alietoa haya maoni anaakili sana za kusoma na kuelewa hakika waelewa hawapo siasani

Kuna watu wamejijengea uelewa potofu kuwa demokrasia ni sawa na anarchy (uholela/ vurugu/ ukosefu wa nidhamu). Kwa hawa watu nasema pole sana - siyo kosa lao bali ni mfumo wetu wa elimu.

Falsafa za Adam Smith, ambazo ni msingi wa uchumi endelevu katika nchi zinazofuata demokrasia, unajikita katika dhana ya uhuru wa mtu binafsi, na uhuru wa watu kutafuta na kuhodhi mali/ utajiri kwa kadhri ya uwezo wao. Hizi falsafa zinatafakari kuwa kila mtu akijituma kutafuta utajiri, basi nchi kwa ujumla nayo inaneemeka. Ni kutokana na uhuru huu wa mtu binafsi tunapopata utaratibu wa utawala wa kidemokrasia, ambao nia yake ni kuwezesha watu huru ku-influence wanavyotawaliwa, ili isije ikatokea tawala dhalimu itayoingilia uhuru wa watu binafsi.

Katika utaratibu wa demokrasia, nguvu zote zinatokana na ridhaa ya watu huru. Hakuna mtu atayepewa uwezo juu ya wenzake bila idhini ya watawaliwa. Hakuna sheria itayopitishwa bila idhini ya watawaliwa.

Kwanza, mtu yeyote anaweza kusoma posts za jamii forum bila kuwa member, atakachoshindwa kufanya ni to comment and/or to submit posts. Hisia zako kuwa kama sio member huwezi kusoma posts sio sahihi. Tuepuke hisia zisizo na msingi.

Pili, tofautisha kati ya philosophical, theoretical, na empirical arguments/evidences. Hivi ni vitu tofauti inapokuja kwenye scientific research, wengi huwa wanasoma philosophical arguments na kufikiri kuwa ni empirical/scientific arguments - na hilo ni kosa kubwa sana kisayansi. Mahusiano ya hivi vitatu ni kuwa philosophical and theoretical arguments zinatumika kujenga hypothesis ambazo zinakuja kuwa tested kwenye empirical studies. Post yangu imejikita kwenye empirical researches using complex statistical modelling to test possible correlation/causality kati ya democracy na maendeleo kwa tafiti zilizotumia taarifa/data za cross country.

Tatu, kutokana na kutokuelewa haya, post yako imeongelea mambo ambayo sijayaongelea wala hoja yangu haikuwa kwenye philosophical arguments za demokrasia. Nne, umeanza na personal attack kuwa nimejiunga jana kwa hiyo nisingeweza kujua post za nyuma. Sisi binadamu, ukiona instant response yako ya hoja ni personal attack then ujue kuna tatizo hapo. Tujikite, kwanza, kuelewa hoja, pili kutafakari hoja ambazo zinaweza kuwa tofauti na tuliyokuwa tumeamini au kuaminishwa kwa miaka mingi, tatu, kujibu hoja kwa hoja, na nne, kujifunza one or two things kutoka hoja za wengine. Implicit conclusion ya post yangu ni kuwa si sahiihi kwa watu kuhalalisha hoja zao za umuhimu au usio umuhimu wa demokrasia kwenye hoja ya maendeleo ya kiuchumi. Philosophical arguments zinaweza kabisa kutetea au hata kupinga democracy kwa misingi ya maendeleo - lakini ukweli unabaki kuwa bado hakuna scientific empirical consensus kwenye hilo.
 
DHANA YA “UJAMAA NA MAENDELEO YA VIWANDA” PAMOJA NA DHANA YA IPO SIKU TUTAITUMIA KWA MAENDELEO ENDELEVU

Kama ilivyo wanadamu tuna mahitaji mengi ya msingi na tukiwa tumetimiza miaka 19 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, ni vyema tukatafakari kama taifa lenye watu wapatao 59,000,160 litawezaje kujikimu katika masuala ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni. Hapo ndipo utangundua ni ukweli usiopingika kuwa muda wa serikali kutekeleza falsafa ya ujamaa ulioboreshwa umefika ili kutengeneza ajira, na nchi kupiga hatua kubwa kuelekea uchumi wa kati 2025.

Ili kufikia dira hiyo, kwa kipindi cha miongo kadhaa watanzania imekuwa ikijikita kwenye uchumi wa kutoa huduma badala ya uzalishaji mathalani uchumi wa nyumba za kupanga, bodaboda, simu n.k. Hali iliyopelekea vijana wengi wasomi wakiwa mitaani bila ajira pamoja na kuwa tegemezi kwa jamii. Kutokana na hali hiyo, kuna haja kwa viongozi kuweka mazingira yatakayofanikisha sera ya ujamaa pamoja na sera ya ubepali kutumika ili kufikia azma ya serikali ya viwanda na kufanya miundombinu ya reli na barabara kutumika ipasavyo. Madhalani, Serikali inaweza tumika taasisi zake ikiwemo NHC kujenga jamii zenye nguvu (Communities) kwa kujenga nyumba (miji) yenye tija katika maeneo ya uzalishaji na kuajiri vijana kama ilivyoanzishwa taasisi ya Kilimo (Mbeya) na Mpwapwa (Dodoma).

Utekelezaji makini wa Sera ya Mixed Economy nchini kutasaidia kuondoa tatizo la ajira kwa vijana wa kiwango cha medium zone pamoja na kuongeza uzalishaji utakaosadia kuongeza bidhaa, utulivu wa shilingi, utulivu wa kisiasa na kudumisha amani nchini.hivyo ni vyema wanasiasa mkasaidia maandalizi ya kuanzisha vituo vya uwekezaji kulingana na mahitaji ya eneo na wakati husikakwani ni ukweli usiopigika kuwa tatizo la ajira linaathari siyo katika jamii ya Tanzania pekee pia hata nchi zilizoendelea hivyo ni wakati wa kufunga mkanda (Benjamini Willium Mkapa) kwa maendeleo endelevu.

TATIZO LA VIJANA WALIOWENGI NI NYUMBA (kulipa kama bia kuelekea kwenye umiliki wake) + TRACTOR

MORE STRATEGIES (attached)
 
Back
Top Bottom