Demokrasia na Maendeleo ndani ya CHADEMA



Siku moja nilimwuliza Dk. Slaa kwamba 'Ikiwa usalama wa taifa uliopo ni dhaifu kwa kiasi cha kugawanyika na sehemu yake kuripoti kwako kama unavyodai, je Chama chako kikiingia madarakani utafikiria kufumua na kuunda upya idara ya usalama wa taifa?' Slaa alikimbia na mods wakahamisha haraka ile thread!
Ndugu m4cjb, usalama wa taifa wanatuchagulia viongozi na wana jukumu la kuilinda serikali iliyopo madarakani, kulinda taifa dhidi ya maadui wa nje na ndani pia. Ni upotofu tu kuikejeli TISS, kama ilivyo kwa taasisi zote za usalama ulimwenguni sisi raia wa kawaida tunajua na kutambua pale failure inapotokea lakini hatujui mafanikio makubwa ya kiusalama yanayotokea daily!
Na kwa timu ya uongozi hapo chadema kwa sasa sifikirii kuwa kuna TISS inaweza kutoa go ahead through Vetting1
 
Last edited by a moderator:
Mimi sifikiri hivyo, Zito aliamua kutofautiana na muelekeo wa chama chake. Haikuwa sawa kuwafukuza akina J. Shonza na wenzake halafu ukamwacha Zito.Kwa wanaoiamini CHADEMA ilikuwa ni swali kubwa sana kumwacha ndani ya CHADEMA Zito. KILICHOFANYIKA MIMI NAONA NI SAWA. KUNA WAKATI KUNA HAJA YA KUCHUKUA MAAMUZI KAMA HAYA.

NI VEMA KUBAKI NA WATU WACHACHE WASAFI KWANI CHAMA KITAFIKA MBALI KULIKO KUBAKI NA WATU WENGI WATAKAOUA CHAMA KESHOKUTWA.

KWANI ZITO LAZIMA AWE CHADEMA ANAWEZA ANZISHA CHAMA AU KUJIUNGA CCM.
 
Rudi ukajifunze kuandika Bwana Le Mutuz.

Akili yako ni ya mtu asiye na mtazamo wa kichambuzi. Ni ya mtu hovyo tu.
 
Ukweli ambao chadema wanapaswa kuelezwa waelezwe tuh,hakuna tena haja ya kuwaficha,

Maji yamekwisha mwagika hayazoleki tena haya
 
It is advisable to settle down after any shock that has struck you.....then you can give what is very useful and fruitful....
Kijana analysis yako ni very poor....kwanza uchambuzi wako kwa kufuata "content analysis" kichwa cha habari hakikufaa kuwa Demokrasia....
Kitu kingine unasema suala la ushahidi wakati wewe mwenyewe hujatoa "evidence" ya kichwa cha habari hapo juu....
Suala la Zitto na Kitila ni suala la muda.....japo nawaunga mkono wasomi na wachambuzi hawa ila nakuomba relax kwanza....tafakari na kufikiri bila jazba....usiwe kama mfiwa,ambae hulaumu dereva wa ambulance,daktari,nesi na hata Muumba.
Thanks.
 
Toka uanze kula buk7 za Lumumba akili yako imevurugika sana... OOK vipi GESI inatoka haitoki?
 
Ukimaliza kusoma huo utumbo wako pia pitia na hii story....na useme ni lini ZZK alikanusha...

VIGOGO kadhaa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wametajwa "kuingilia" Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), MwanaHALISI limegundua.

Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya idara hiyo zinaeleza kuwa vigogo hao wana mahusiano ya karibu na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe.
Anayetajwa rasmi kuwa na mahusiano na Zitto ni Naibu Mkurugenzi wa TISS, Jack Zoka.
Kufichuka kwa taarifa za kuwapo "uswahiba" kati ya Zoka na Zitto kumekuja katika kipindi ambacho CHADEMA kimekuwa kikituhumu maofisa wa juu wa usalama wa taifa kuvuruga uchaguzi mkuu uliopita.
Aidha, kuibuka kwa tuhuma hizi kumekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuchapisha taarifa mbalimbali za mawasiliano kati ya Zitto na Rais Jakaya Kikwete.
Baadhi ya mawasiliano hayo, ambayo Zitto ameyapeleka kwa rais, aliyapeleka pia kwa baadhi ya watuhumiwa ufisadi nchini.
Kwa mujibu wa mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ambaye alitangazwa kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Kikwete; viongozi wa TISS walihusika, kwa kiasi kikubwa, katika kile alichoita, "Kuchakachua matokeo ya uchaguzi."
MwanaHALISI limefanikiwa kupata rekodi ya mshororo wa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka.
Kuna mwingiliano wa simu za mdomo na maandishi (sms) kutoka kwa Zitto kwenda kwa baadhi ya vigogo wa ngazi ya juu serikalini na TISS, hasa Zoka.

Nyaraka za mawasiliano zinaonyesha kuwa Zitto amekuwa akiwasiliana na naibu mtendaji mkuu wa TISS huyo zaidi ya mara tatu kwa siku.
Kwa mfano, Zitto na Zoka walifanya mawasiliano ya simu mara tisa hapo tarehe 8 Agosti. Simu iliyotumika katika mawasilino hayo, ni Na. +255756809535 ambayo hutumiwa na Zitto na +255754787550 ambayo hutumiwa na Zoka.
Wakati mawasiliano hayo yanafanyika, Zitto alikuwa katika maeneo tofauti.
Mawasiliano ya kwanza kati ya Zitto na Zoka yalipokuwa yanafanyika, simu ya Zitto ilisomeka kuwa alikuwa katika maeneo mbalimbali.
Mathalani, wakati mwingine simu ilikuwa ikisomeka kuwa yuko Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam, Kigoma Urban (Mjini), Kigoma Rural (Vijijini), Mtwara, Uwanja wa ndege-Ilala, Oyster Bay, Ukonga, Upanga na katikati ya mji.
Gazeti hili halikuweza kugundua mara moja undani wa mawasiliano ya Zitto na Zoka.
Kinachofanya baadhi ya wachunguzi wa mambo kujenga shaka ni kwamba mmoja ni mwanasiasa, tena kutoka chama kilichopo nje ya utawala; na mwingine ni mtumishi wa idara ya usalama inayolalamikiwa kukandamiza upinzani nchini.
Hata hivyo, taarifa zinaonyesha kuwa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka yalianza kupamba moto kuanzia tarehe 6 Agosti 2010, siku moja baada ya CHADEMA kuzindua kampeni zake za urais.
Kulingana na uchunguzi, siku hiyo, tarehe 6 Agosti, simu ya Zitto ilisomeka kuwa yuko Kigoma Urban.
Katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni, CHADEMA kupitia kada wake mashuhuri, Mabere Marando, iliibuka na lundo la tuhuma dhidi ya vigogo kadhaa wa serikali, CCM na idara ya usalama wa taifa.
Akizungumza na maelfu ya wananchi katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, Marando alisema wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya Benki Kuu ya taifa (BoT), ulifanywa na serikali na washirika wake.
Miongoni mwa vigogo aliodai kuwa walihusika kufanikisha wizi huo, ni rais wa sasa, Jakaya Kikwete, rais mstaafu Benjamin Mkapa, mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na Edward Lowassa.
Akiongea kwa kujiamini, Marando alisema, "fedha za EPA ni wizi uliotiwa baraka na serikali ya CCM na ndio uliomsaidia rais Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005."
Kuanzia hapo hadi sasa, Zitto na Zoka wamekuwa na mawasilino ya mara kwa mara, na karibu kila siku huzungumza kwa simu.
Mawasiliano mengine ya mara kwa mara yalifanyika tarehe 7 Agosti 2010, siku mbili tangu hotuba kali ya Jangwani. Yalianza saa 10:17 na kuendelea tena saa 10:50, saa 10:51:31, saa 11:46:13, saa 12: 14:46, saa 12:26:48 na saa 13:50: 21.
Lakini Zitto alipoulizwa kuhusu sababu ya yeye kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na vigogo wa TISS, alisema hajui na hakumbuki lolote kuhusu kuwapo mawasiliano hayo na Zoka au mkuu yeyote wa idara hiyo.

Zitto amesema yeye, akiwa mwanasiasa na kiongozi, anazungumza na watu wengi kutoka katika taasisi na mashirika mbalimbali ndani na nje ya nchi, lakini hajui kitu kuhusu usalama wa taifa.

Alipobanwa kuhusu mazungumzo yake na Zoka, hasa yale ya 3 Novemba 2010, saa nne na dakika 56 asubuhi, siku mbili baada ya uchaguzi kumalizika, Zitto alisema, "Siku hiyo nilizungumza na watu wengi sana. Siwakumbuki ni akina nani hasa."
Alisema, "Hicho ndicho kipindi ambacho matokeo ya uchaguzi nchini kote yalikuwa yakizuiwa ikiwamo kwetu Kigoma. Na ukumbuke mimi nilipigwa mabomu na polisi na usalama wa taifa. Nakumbuka viongozi wengi wa vyombo vya ulinzi na usalama walinipigia simu kunijulia hali na kupata taarifa ya kilichotokea," anaeleza.

"Sasa kama Zoka naye alinipigia siku hiyo sikumbuki; lakini nilipigiwa na wengi…Naomba uniambie kitu, hivi mnachokitafuta hasa ni nini?" aliuliza.
Katika njia ya kujitetea, Zitto aliuliza, "Mwanasiasa kuongea na wakuu wa vyombo vya usalama ni kosa? Maana, hata kama ningekuwa nimezungumza naye, kosa langu liko wapi?" alieleza mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini.

Alipoelezwa kuwa haoni hiyo ni hujuma dhidi ya chama chake kwa kuzungumza na viongozi wa TISS na kile ambacho amekuwa akikizungumza kikiwa hakifahamiki kwa viongozi wake, Zitto alisema, "Sijawahi kukihujumu chama changu mahali popote, siku yoyote."

Jitihada za gazeti hili kuzungumza na Zoka hazikufanikiwa katika kipindi chote
cha mwishoni mwa wiki, kwa vile kila alipopigiwa, simu yake ya mkononi ilikuwa haipokelewi.

Hata ujumbe mfupi wa maneno uliotumwa kwenye simu yake saa 2:53 asubuhi ya Jumapili; ukieleza sababu za gazeti kuzungumza naye, haukujibiwa.

Aidha, tarehe 2 Novemba, siku moja baada ya kuzungumza na Zitto, Zoka alinukuliwa akikana madai ya Dk. Slaa, kuwa TISS imesaidia kuvuruga uchaguzi.
Katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Zoka alisema, "Dk. Slaa amekuwa akidanganywa na watu wanaojiita maofisa wa usalama wa taifa."
Hata hivyo, kuna meseji mbalimbali kuhusu udini na uamuzi wa CHADEMA kususia hotuba ya rais Kikwete ambazo zilitumwa na Zitto kwa baadhi ya wabunge wa CHADEMA ambazo zinadaiwa kuandaliwa na idara ya usalama wataifa.
Ujumbe huo unadaiwa kuandaliwa kwa ustadi mkubwa katika kukuza suala la udini na kuleta mtafaruki katika chama.
 
Demokrasia bila mipaka ni uhuni.

Fahamu si kila sehemu demokrasia inafaa usaliti alioufanya Zitto ingekuwa jeshini saa hizi angekuwa hayati huko hakuna msamiati wa neno demokrasia.
 


Thank you,

CHAGA DEVELOPMENT MANIFESTOPHSIM TUUNGANE NA KUIKOMESHA MOJA KWA MOJA,

TUSEME KWA PAMOJA SASA KUWA YATOSHA,TAIFA HILI NI LETU SOTE,TUWAKANE WAKANDA NA WAKABILA NA TULIJENGE TAIFA LETU...
 
Na nipigwe tuh.!!

Ikibid waniCHACHAWANGWE TUH..

MAANA SASA TUMECHOKA SASA,WANAJIFANYA WANA HUBIRI DEMOKRASIA HUKU WANAIHUJUMU DEMOKRASIA HIYO HIYO??

Huna lolote mchumia tumbo tu! Gesi imekushinda utaweza ya chadema?
 
TBS,
Ungetulia kwanza mmalize maombolezo na kuanua tanga kisha urudi kwenye jamvi.

Yaani umejichanganya na kujipinga mpaka basi. Rangi zenu, hisia zenu, malengo yenu, mipango yenu nk vyote viko wazi kama jua hivyo huwezi kuelewa maana ya neno "demokrasia". Pia kwa vile bosi wenu na washirika wenzake leo watakuwa na press conference, na kwa vile yeye ndiye mwenye kushikilia akili zenu basi msubiri halafu ufuate atakachosema 100% maana hiyo ndio aina ya demokrasia unayoijua na kuitaka.
 


Thank you,

Waeleze waelewee...
 


Sawa tuh,who cares??

KELELE NA MIZUKA MINGI NDIVO ZILIZO IBADA ZETU SISI WALOKOLE,SO WE USITUSHANGAE SANA,TUACHE NA MAMBO YETU.

NDAN YA CHAMA TUNA UHAKIKA KWA VILE WENYE MAKALI NI NYINYI BASI VITA HII MUMESHINDA,LAKIN NDAN YA TANZANIA NA KWA WANANCHI GAME BADO MBICHI HII,NA WEWE MWENYEW UNAJUA HADI SASA MSHINDI KESHAPATIKANA,CALM DOWN UKWELI UTAFAHAMIKA TUH NA HAKI ITATENDEKA
 
Tunawasomeni wanachadema mnavyogawana kuni, nipo zangu kijiweni nakunywa kahawa.
 

Kumbe ndio maana chadema inaungwa mkono na walokole wengi! Kumbuka chadema ni saccos ya wanaukoo wa mtei!
 
Tunawasomeni wanachadema mnavyogawana kuni, nipo zangu kijiweni nakunywa kahawa.

Mkuu Ritz,inakoelekea inaonekana haka ka saccos ka wanafamilia ya Mtei kanaelekea mwishoni! Hivi,ile nyumba waliopanga ya makao makuu ya saccos yao ni mali ya nani vile?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…