Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,996
Kwa miaka tumeambiwa wao ndio waasisi wa demokrasia nchini na ya kuwa wao ndio walinzi wa demokrasia hiyo. Leo hii Taifa letu linaenda kupitia kipindi cha majaribu na tusipoangalia tunaweza kupita kipindi cha giza totoro. Wananchi wetu wamepiga kura vizuri jana na kutulia wakisubiri matokeo yatoke wenye kushinda wawe wameshinda na walioshindwa wawe wameshindwa.
Hata hivyo hali hadi hivi sasa ni tete na kama nilivyoasa masaa kadhaa huko nyuma hali hii ya kutokujua na mambo ambayo yanaonekana kama kulazimisha uongozi uliokatliwa juu ya nchi kana kwamba ni urithi wa watu fulani itapelekea mgongano wa wazi kati ya watawala na watawaliwa.
Demokrasia yetu iko matatani. Ninawasihi vijana kutulia na kuwa na uvumilivu lakini wakati huo huo Tume ya Uchaguzi iwatendee haki Watanzania na kufanya kile walichoapishwa kufanya. Vyombo vya usalama vikae nje sana katika hili na wasiwe wabebaji wa maagizo ambayo yana athari kwa wananchi wa taifa lao. Tutumie hekima kila inapostahili vinginevyo yale tuliyoyahofia kweli yatatokea na tutajikuta tunashindwa hata kumlaumu mtu.
Hadi hivi sasa hata hivyo ni watu wa Tume ya Uchaguzi ndio watasababisha matatizo kwani wanashindwa kufanya kitu kidogo sana kama kutangaza matokeo. Hadi hivi sasa kuna dalili matokeo wanayotaka kutolewa yale ni yale ya CCM kushinda lakini maeneo mengine wanabania. Jamani hii si haki, tunapolilia utaalamu na usomi basi tunatarajia tuone kweli watu wanafanya kazi kisomi na kwa weledi. j
Liacheni litakalokuwepo liwe, Tanzania itakuwepo tu. Heshima ya CCM inaegemea kabisa kwenye matukiio yanayoendelea kutokea sasa hivi nchini. NI katika haya CCM itahukumiwa na historia. Ni katika haya Rais ambaye amependwa na wananchi licha ya tofauti za kisiasa atajikuta anahukumiwa. Naomba tena tusilazimishe ushindi wa kishindo.
Demokrasia yetu ni kubwa zaidi kuliko furaha na hisia za kikundi kimoja cha watu. Kama hawakutaka kuwa tayari kusimama mbele ya hukumu ya Watanzania wasingeitisha uchaguzi jamani ili tuwe na utawala wa kudumu tu. Demokrasia bila uwezekano wa kushindwa siyo demokrasia. Sauti ya wananchi isikike.