Kusema tuna demokrasia Tanzania ni kudanganyana

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Wadau nawasalimu.

Nimekuwa najiuliza hivi tunaposema Tanzania kuna demokrasia je, hiyo demokrasia ipo kwenye nini? Au kuwa na mfumo wa vyama vingi tu ni demokrasia?

Binafsi siamini kama Tanzania kuna demokrasia kwani bado CCM inahodhi mambo mengi hususani suala zima la uchaguzi kuanzia tume ya uchaguzi wasimamizi wa uchaguzi mpaka vyombo vya kuchapisha fomu za uchaguzi na kutangaza matokeo.

Mbaya zaidi huwezi kuwa na uchaguzi wa kidemokrasia ambao unasimamiwa na watendaji wa serikali ambao ni makada wa CCM na wakati huo huo CCM ni mshiriki wa uchaguzi huo.

Kama kweli CCM ina nia ya dhati ya kuwa Tanzania iwe nchi yenye demokrasia ya kweli basi ifanye haya.

1. Mchakato wa katiba mpya tena katiba iliyojaa maoni na mapendekezo ya wananchi ipatikane.

2. Tume huru ya uchaguzi itakayojumuisha watu mbalimbali wa vyama vya siasa mashirika na taasisi za dini na asasi za kiraia iundwe baada hapo ndio tufanye uchaguzi.

Kinyume chake kufanya uchaguzi chini ya katiba na tume ya uchaguzi iliopo ni kudanganyana.
 
Back
Top Bottom