Demokrasia ilobagazwa

Mi naona we ndo "mpumbavu." Mada imeeleza vizuri jinsi kamati kuu za vyama zinavyoimpose wagonbea hata wale wasiokubalika kwa raia. Hebu angalia mtu kama Trump kungekuwa na ujinga wa kamati kuu angepita? Lakini mwamba kapita kwa kura za wanachama (wao wanaita primaries).
 
Demokasia ni kwaajili ya watu, wewe JUHA.

Achia chama kisimamishwms ZUZU, halafu wananchi wakimchagua huyo zuzu, wao ndio wenye SHIDA.

Hoja ya msingi ni mfumo wa wananchi kuamua, siyo CHAMA kimechagua zuzu gani.
 
Demokasia ni kwaajili ya watu, wewe JUHA.

Achia chama kisimamishwms ZUZU, halafu wananchi wakimchagua huyo zuzu, wao ndio wenye SHIDA.

Hoja ya msingi ni mfumo wa wananchi kuamua, siyo CHAMA kimechagua zuzu gani.
Hao wananchi wana option? Ikiwa mgombea huru ni marufuku? Tumia kichwa kufikiri
 
Siku hizi inaitwa 'Demokrasia yetu na utamaduni wetu'
 

..tatizo la siasa za Tanzania ni unyama [ utekaji, utesaji, mauaji ]unaofanywa na vyombo vya dola dhidi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani.

..hatuwezi kuwa na ligi ya mpira wa miguu, halafu timu moja kubwa inaingia uwanjani na bisibisi, na kuwachoma wapinzani wao, halafu tukasema tuna ligi iliyo na usawa, ambayo matokeo yake ni halali.

..kuna watu wameuwawa, wametekwa, wameteswa, na inasemekana kuna mpaka ufiraji, na yote hayo yanafanywa kuwawezesha Ccm, halafu wewe unasema tusishughilike na hayo mpaka kwanza tuwe na demokrasia ya kweli ndani Tlp, Tadea, Udp,..?
 
Naamini sio wanachama wote wa Chama Dola wanapenda huo unyama.

Kwa picha ya nje, Chama kinanufaika na huo uhuni Ili kulinda madaraka, lakini kiuhalisia ni kundi dogo sana la wahuni ndani ya chama ndio wanufaika wa huo uovu.
 
Naamini sio wanachama wote wa Chama Dola wanapenda huo unyama.

Kwa picha ya nje, Chama kinanufaika na huo uhuni Ili kulinda madaraka, lakini kiuhalisia ni kundi dogo sana la wahuni ndani ya chama ndio wanufaika wa huo uovu.

..kundi dogo lakini ndilo lenye sauti na maamuzi.

..mambo yaliyotokea na yanayoendelea yamesababisha baadhi ya nchi zisambaratike.

..bahati mbaya sisi tunajaribu kuyapambapamba yaonekane si ya hatari na si mabaya kiasi hicho.
 
Ndio maana katiba ya nchi ilishindwa kumlinda yule jamaa asiliwe kichwa na chama, japo kwa katiba ya nchi alikuwa na kinga.
Huu ndio mimi nauita ujinga mkuu kuliko ujinga mwingine wowote ndani ya katiba yetu, ile mamlaka kuu ya wananchi kwenye katiba yetu, imekasimiwa kwa chama cha siasa, as a result chama ndio kikubwa kuliko katiba ya nchi!.

Je, Wajua Japo Tanzania Ilipaswa Kutawaliwa na Ukuu wa Katiba, Lakini Inatawaliwa na Ukuu wa Chama?. Mbele ya Chama, Katiba si Lolote, si Chochote!​

P
 
Nimekusoma vema ila kuna sehemu pengine hukunielewa Katiba haiwezi kusema Kuhusu Siasa yetu na Upinzani wake bali historia na mazingira ya nchi ndio hujenga Vyama vya Upinzani sio kwa sababu tu vipo duniani basi na sisi tuvitumie. Hata nchi za Ulaya walianza na tawala zao wakatokea Wapinzani wa utawala huo ambao hawakukubaliana na mwelekeo wa Chama tawala wakaunda hizi Itikadi pinzani dhidi ya Chama.

Upinzani huo ndio ukapewa majina ya itikadi na sera zao zikaweza kuleta baadhi ya mabadiliko ya Katiba na Sheria. Hivyo, Upinzani ni maono tofauti ya Utawala kudai Haki za Wananchi, pamoja na mwelekeo wa maendeleo.yao

Niliposema Ujamaa sii kwa maana uandikwe ndani ya Katiba na muundo wetu wa Kitaifa - Hapana. Hivyo ndivyo tulivyokuwa kabla ya vyama vingi Katiba yetu ya 1977 ilisema tunajenga nchi ya " Ujamaa na Kujitegemea" Itikadi moja ya Azimuo. La Arusha, hivyo tunapounda Vyama vingi vya Upinzani viwe na sababu ya msingi ya kupingana na Itikadi hiyo badala ya kila Chama kujiandikisha wakiwa na Itikadi sawa. Na tulipoanza kuandikisha vya vingi nadhani Chadema walikuwa na sababu kutetea ya watu binafsi kumiliki ardhi na rasilimali (Ubepari) NCCR wakiwa na kati Kiitikadi kisha CUF kutetea maslahi ya Zanzibar.

Mpaka hapo ilitosha maana hakuna Itikadi nyingine inayoakisi Watanzania zaidi ya labda niseme mila, tamaduni na mazingira. Ukitqzama vyama vingine vyote vilivyobakia vinarudia yale yale yaloshikwa na hivi vyama vinne isipokuwa huko nafasi za Uongozi chache hivyo wanaunda vyama vyao. Kati ya vyama 15 vingi vina mrengo wa CCM au Chadema! Zanzibar vile vile ni aidha CUF na ACT kwa kufuata viongozi sio Itikadi wala Sera!

Na Popote Duniani Itikadi na sera zote za Upinzani zimetokana na kutofungamana na malengo ya Itikadi mama na ndio kukaibuka wa Liberali pinzani na mfumo, Demokrasia ikajengwa kwa misingi hii ilinkuwapa Wananchi mamlakanya kuchagua. Wananchi ndio wahanga wa Utawala mbaya, Usawa unapokosekana na Ukiukaji wa haki za binadamu kwa hiyo ni jukumu la.Wananchi Kuchagua Uongozi ambao maono yake (Vision) yamezingatia vipaumbele vyao.

Niliposema Ujamaa ni sababu Ulikuwa mwelekeo wetu wa awali. Azimio la Arusha ndio Siasa mama tuloanza nazo baada ya Uhuru na Muungano, tukavunja vyama vingi vya Siasa na bila shaka Wapinzani wa Siasa ya Ujamaa walijaribu mara kadhaa kufanya Mapinduzi kwa sababu hawakuwa na jukwaa la Kisiasa kupingana na CCM.

Maadam leo tuna vyama vingi basi iwe kwa utaratibu unaokubalika yaani vyama pinzani viwe na Itikadi ambayo wananchi wanaelewa wanapingana Ujamaa (Itikadi na Sera) badala ya kuwa wanapingana na rais!

Upinzani ndio hushinikiza Sheria bora zaidi shidi ya tulokuwa nazo, utasimamia Serikali pale kuna Uongozi mbaya, hakuna Usawa n.k.

Haya yote ni maswala ya mfumo wa vyama.vya Siasa Kiikadi na sera sio Katiba. Bali Katiba itatambua uwepo vyama vya Siasa na tofauti zake sio tofauti za Viongozi wanaogombania kwenda Ikulu.

Viongozi wa aina hiu ndio huzaa Chama kina wenyewe ilihali Vyama. Vina mwelekeo wake. Kiongozi yeyote akienda kinyume cha itikadi na sera za Chama.(Mwelekeo) anakataliwa na hata Wanachama wenzake.

Hii Katiba Pendekezwa au Rasimu ya Katiba sijaisoma yote kwa sababu binafsi sio Muumini wa Serikali 3. Siamini katika Uzanzibar na Utanganyika kutokana na WATU wenyewe, sisi ni wabaguzi kwa jadi.

Vijana wengi wanaongea vitu hawaijui Tanganyika na Zanzibar ya miaka ya 50 na 60 kurudi nyuma ilkuwaje hadi TANU na ASP sikafikia muafaka wa kuunganisha vyama vyote kuwa kimoja na kuunda nchi moja ya Watanzania. Hii haijawahi tokea nchi yeyote ya Afrika na tumu ya pekee tulowahi fanikiwa.

Vita ya kwanza kabisa mwalimu alopambana nayo ni kutuunganisha sote akaondoa Ukabila na Udini na Ujamaa haswa ulilenga kulijenga Taifa kama jamii moja ya Watanzania.

Leo tukichukua Serikali 3 amini maneno yangu Muungano utakufa tena wakati mbaya sana ambao leo hii kila.nchi duniani inakataa Wahamiaji wala sii haramu tu hata walokuwa na Sheria wamekuwa targeted.

Sihofii zaidi Zanzibar bali Bara ambako hata Paramagamba alizungumzia! Ogopa sana Watanganyika watakapo dai nchi yao! Bila shaka anajua kitachofuata ni kibaya kuliko haya yanayotokea Zanzibar leo.

Maasalaam
 
Katika hilo mimi nadhani kosa sio Katiba bali sisi wenyewe Mazwazwa. Haiwekzekani Viongozi wanakiuka Katiba wazi kabisa tunabakia kulalamikia mitandaoni kutafuta followers!

Sheria zipo, mahakama zipo basi watokee hao Wapinzani, wanaharakati wapeleke mashtaka mahakamani. Kina Mtikila wakonwapi siku hizi? Iweje Kiongozi akiuke Katiba halafu anatamba kuwa juu ya Sheria tunashindwa ku challenge legally?

Kwa nini kila kosa la Ukiukaji wa Katiba tunalalanika mitandaoni na vijiwe vya waandishi wa habari utadhani ni ya Yanga na Simba!

Kwa mujibu wa Katiba hii mbovu, watu wanaivunja wakidai ni Kitabu halafu tunabaki kuhadithiana kama kwamba Katiba sio Sheria. Sasa hiyo Katiba Mpya nani atailinda kama sio sisi. Laa ni upuuzi kudai Katiba Mpya wakati hii mbovu inavunjwa na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.

Ndio maana Viongozi wanajiona wao wakonjuu ya Wananchi na wananchi wanakubali wale ni Waheshimiwa! Kuna tofauti gani na Utawala wa Kiumla?
 
Katika hilo mimi nadhani kosa sio Katiba bali sisi wenyewe Mazwazwa. Haiwekzekani Viongozi wanakiuka Katiba wazi kabisa tunabakia kulalamikia mitandaoni kutafuta followers!
Naunga mkono hoja, hili la sisi ni mazwazwa nami nimelisema ila mimi sijatumia mazwazwa, mimmi nimetumia neno mazuzu, sisi Watanzania ni mazuzu!,

The Voices From Within: Japo Wamenyamaza Kama Mazuzu, na Hawaulizi Kitu, Ila wana Macho na Masikio,Wanatamani Wawe Wanaelezwa Ukweli, No Matter What!​

Sheria zipo, mahakama zipo basi watokee hao Wapinzani, wanaharakati wapeleke mashtaka mahakamani. Kina Mtikila wakonwapi siku hizi? Iweje Kiongozi akiuke Katiba halafu anatamba kuwa juu ya Sheria tunashindwa ku challenge legally?
Hii ni hoja ya msingi sana, niliwahi kuizungumzia enzi za kilichotokea Uchaguzi wa Zanzibar, Jecha kupindua meza, Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua hatua zozote, pia enzi za ule udikiteta wa yule Blaza wangu, kwenye mkutano fulani wa JF, nilimuuliza Zitto na Wapinzani,
View: https://youtu.be/A_YPEHtM9WM?si=Cu_55vUpUCptb-HZ, Zitto Kabwe na wapinzani wote, kwanini mnapiga tu kelele kuhusu udikteta bila kuchukua hatua zozote? Isn't it a nuisance? Je, 2020 ni CCM pekee? na hata school mate wangu Tundu Lissu, na Chadema walipoasisi UKAWA wakapanga kufanya maandamano nchi nzima kuupinga udikiteta, niliwashauri Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele!
Kwa nini kila kosa la Ukiukaji wa Katiba tunalalanika mitandaoni na vijiwe vya waandishi wa habari utadhani ni ya Yanga na Simba!
Hivi ndivyo Watanzania tulivyo, kazi yetu ni kulalamika tuu bila kuchukua hatua Watanzania ni watu wa maneno maneno, kupiga kelele na kulialia tuu, Tukija kwenye Vitendo ni sifuri, 0, zero, nil, hamna kitu!. Je Tutabadilika?
Ila pia kwenye hili, tusiwalaumu Watanzania wa kawaida, lawama pia zielekezwe kwa sisi mhimili wa 4, hatutimizi wajibu wetu kikamilifu,

Je Wajua Taifa Bila Mhimili wa 4 Huru na Imara ni Taifa Mfu?. Je Watanzania ni Mazuzu?. Gazeti la M/halisi Lisamehewe Kuandika Ukweli au ni Zuzu Tuu?​

Hakuna tofauti!, ila kwa vile haya yote yamesabibishwa na katiba mbovu yenye imperial president, tukipata katiba mpya tutapunguza madaraka ya rais, Je, wajua kuwa Rais wa JMT ndie Serikali, Bunge na Mahakama? Yuko juu ya Mihimili yote 3. Je, kuna uwezekano Rais wa JMT pia yuko juu Katiba? na hatutaruhusu ujinga huu kwenye katiba mpya Je, Wajua Japo Tanzania Ilipaswa Kutawaliwa na Ukuu wa Katiba, Lakini Inatawaliwa na Ukuu wa Chama?. Mbele ya Chama, Katiba si Lolote, si Chochote!

Mzee Pasco.
 
Hivi niulize kitu - Tunataka kupunguza madaraka ya rais kama yapi? Maana lazima kuwepo na mtu au Watu waliokabidhiwa hayo madaraka!

Je huyu mtu au hao Watu wakiyatumia vibaya itakuwaje? Ujue sisi Waafrika tukipata Cheo kikubwa au Utajiri huwa tunabadilika kabisa, ni hulkanya watu wote maakini wakipata makalio hulia mbwata! Mtu wako kabisa akipaya utashangaa kama ndiye yule ulokuwa unamjua. Sisi wote tunajua hulka zetu na ndio kama ndoto, ukipata watakukoma!

Kwa hiyo kama tunamuondolea madaraka rais ya Kuchagua viongozi wa mihimili au taasisi nyingine, hao viongozi wa huko watakuwa answerable kwa nani kama hawawajibiki kwa rais, Watawajibisha na nani?

Maanake ikiwa leo hata Mkuu wa Wilaya, Mkoa au Waziri anadiriki kuvunja Katiba, Je siku waru hama hawa tukiwapa mamlaka alokuwa nayo rais atakuwaje hata kama hataitwa Wwziri au Mkuu wa Mkoa maana mtu ni yule yule kapewa mamlaka.makubwa zaidi.

Mimi nadhani tunatakiwa sisi kubadilika na Sheria iwe kali kwa yeyote mwenye Mamlaka kukiuka Sheria hata kama yanabaki kwa rais ni lazima Sheria ya nchi imuongoze.

Chukulia mikataba! Kwa mujibu wa Katiba hii mbovu, viongozi wamekuwa wakiingia mikataba mikubwa nje au mahotelini ya Uwekezaji bila Kufikishwa Bungeni ama Wananchi kuafiki uwekezaji huo.

Na Sheria inasema lazima Mikataba ya aina hii ipitishwe na Bunge lakini unashangaa kusikia inaenda Bungeni baada ya kusainiwa! Tunaanza kubishana nanwengine kuiwekea kinga Yanaishia japo hapo.

Sheria inasema asikamatwe mtu na kuwekwa kizuizini kwa zaidi ya masaa 48 lakini wanakaa wiki hadi mwezi, tunalalamika mitandaoni!

Kwa nini mtuhumiwa anakamatwa na kufungwa jela wakati Upelelezi bado haujakamilika ilihali Sheria inataka mtuhumiwa akamatwe baada ya Ushahidi kukusanywa? Masaa 24 apelekwe mahakamani!. .

Kutuhumu mtu kwa makosa ya jinai anaweza kuhojiwa, akikutwa hana hatia ama ahusiki aachiwe! Haifantiki mpaka utoe kitu! Na yule anayekatwa na kufungwa jela inatakiwa Upelelezi tayari umeshakamilika -Haifanyiki, tatizo ni nini?

Haya kuna uvamiaji wa Polisi majumbani wakijitambulisha kama wao ni Askari, wanapekua nyumba, Search warrant hawana, wanamkamata mtu hawana arrest order basi hata kumsomea mashtaka kabla hawajamtia pingu hakuna!

Hawa Wasiojulikana wametokea wapi? Je, ni yale makundi ya Ulinzi ya Vyama vya Siasa? Tutawezaje kuwakabiri kwa mujibu wa Katiba! Nini kinazuia utekelezaji kwa mujibu wa Sheria nchini? Sidhani kama ni mamlaka makubwa ya rais bali kuna kasumba fulani ya viongozi kujiona wapo juu ya Sheria. Utawezaje kubadilisha kasumba hii?

Nazungumzia huku Chini mtaani kwa mamilioni ya Wananchi wala hakuhusiani na mamlaka alokuwa nayo rais. Wananchi wanahofia zaidi maisha yao mtaani pengine.hata rais hajui wala hajali. Hii Kumpunguzia Mamlaka rais itaondoaje Adha hizi wanazopata Wananchi wengi kila siku mtaani?

Nimalizie kwa kuuliza. Polepole kapotea mpaka leo hajulikani alipo, ni muendelezo wa mengi yalitokea nyuma. Katiba hii Mpya itawalindaje Wananchi mtaani dhidi ya vikundi hivi vya Wasiojulikana?

Nawakilisha hoja yangu..
 
Dah!... inasikitisha sana.

Hivi vikundi vya 'wasiojulikana' vimekuwa na nguvu kuliko hata vyombo vya Dola, wengine ndio walipita mtaani kuua raia hovyo baada ya kile kilichoitwa 'Uchaguzi' Mwaka 2025.
 
Mkuu Mkandara, kabla ya kuendelea na hoja ya itikadi, naomba niguse jambo moja ulilolisema ambalo naona limejenga msingi wa upinzani wako mzima dhidi ya rasimu hii, kwa mantiki nadhani kuna mkanganyiko wa kiukweli hapo unaostahili kunyooshwa.

Umesema hujaisoma rasimu kwa ukamilifu kwa sababu si muumini wa Serikali Tatu, na kwamba huamini katika Uzanzibar na Utanganyika kutokana na tabia zetu za kibaguzi.

Naomba nikuhakikishie kwa uwazi kabisa:
Rasimu hii SIYO Serikali Tatu, Ni Serikali Moja, yenye Mihimili minne, ambapo Serikali, Bunge na Mahakama ni vyombo vya Jamhuri ya Muungano kwa ujumla wake, bila kugawanywa kati ya Tanganyika na Zanzibar kisha Muhimili wa nne, Baraza la Usimamizi wa Taifa, ndio pekee wenye uwakilishi wa pande mbili, kupitia Marais wawili wa Baraza, lakini hii si kwa lengo la kuunda serikali tatu, ni kwa lengo la kuhakikisha usimamizi wa misingi ya Taifa unabaki na usawa wa pande zote mbili bila upande mmoja kumeza mwingine.

Kwa hiyo hofu yako ya kuuvunja Muungano kwa muundo wa serikali tatu, ambayo naiona ni hofu ya kweli na yenye uzito, haihusiani na rasimu hii, kwa mantiki inashughulikia tatizo tofauti kabisa. Naomba ukisome kwa jicho hilo jipya, ikiwezekana ukianzia Sura ya Nne, ndipo utaona kwamba badala ya kuigawa Tanzania kuwa nchi tatu, rasimu inaimarisha Taifa moja huku ikilinda hofu yako ile ile ya ubaguzi kwa kuweka usimamizi wa usawa katikati.

Sasa naomba nirudi kwenye hoja yako ya itikadi, ambayo umeieleza kwa ufasaha wa hali ya juu.

Umenifundisha kitu kizuri:
kwamba upinzani wa kweli huzaliwa kutokana na historia na mazingira ya Taifa, siyo kwa kuiga mifumo ya nje bila sababu. Naafiki msimamo wako kwamba vyama vingi vilivyopo leo vimekuwa vikundi vya watu badala ya vikundi vya itikadi, na kwamba hili ni tatizo la kweli la afya ya demokrasia yetu.

Lakini naomba nieleze kwa nini rasimu bado inasimama pale ilipo hata baada ya kukubaliana na uchunguzi wako. Wewe unatamani vyama vipangwe kiitikadi, na hilo ni tamanio jema.

Lakini swali la kikatiba ni tofauti kidogo:
Je Katiba ndiyo yenye jukumu la kuvipanga vyama kiitikadi, au ni jukumu la wanachama wenyewe.?

Mimi naona ni la wanachama kwasababu kuna Watanzania wanaamini kwenye itikadi za ujamaa, wengine Demokrasia, wengine Uwajibikaji wa Pamoja, wengine chakula (wazee wa ubwabwa "CHAUMA") na wengine Biashara na Viwanda.

Mfano mzuri ni kwamba Kama wewe na wenzako mkiamua leo kuunda chama chenye itikadi safi ya Ujamaa kinachopingana waziwazi na mielekeo mingine, hakuna kizuizi cha kikatiba kinachowazuia, kwasababu Katiba haijasema itikadi Fulani Ndio Msingi Mkuu wa itikadi Bali umesema kwamba itikadi zote zitakubalika Endapo Tu hazitoenda njee ya Masharti haya, ambayo kwenye Katiba hiyo ni kama vile.
1. Chama cha Siasa kisiwe na itikadi ya kuanzisha vita na Mataifa rafiki au Wenyewe Kwa Wenyewe.
2. Kuzalau na Kudumisha udini, Ukabira na vitendo vya Uvunjifu wamaadili ya Taifa.
3. Vitendo vyote viovu Kwa mujibu wa Katiba na Sheria.
Haya niliyoyaweka Hapo ni Baadhi ya Masharti ya Chama cha Siasa hakitosajiriwa ikiwa inajinathibisha moja kwa moja na hayo lakini si Masharti Pekee yapo zaidi ya Hayo. Masharti kama haya pia yamewekwa kwenye ibara ya 11 ya katiba hiyo.

Kwaiyo hapa ni kwamba Kila itikadi ya Chama cha Siasa itapewa kipaumbe isipokuwa Kwa mujibu wa Masharti na wala Katiba haijasema wala kushinikiza kwamba itikati Fulani itakuwa na kipaumbele kupita nyinginezo.

Jambo lingine ambalo ni Tatizo halisi ulilolibainisha ni kwamba vyama vinavyofanana na kutofautiana kwa majina ya viongozi tu. Jibu langu ni kwamba Hilo ni tatizo la soko la kisiasa, siyo la Katiba.

Hivyo Basi kuna Baadhi ya Vyama vinaamini kwenye fikra za Kiongozi wao, mfano "Fikra za Mwalimu zidumu", watu waliitikia "zidumu", N.B nadhani unakumbuka kauli Hizo Kipindi Kile cha Nyerere. Sasa hakitokea Mtu mwengine hakisema itikadi za kumtukuza Mtu kama Mungu sio sahihi yeye atakuwa na itikadi yake ambayo Wananchi wataamua Wenyewe kwenye Uchaguzi Mkuu na kuwapigia Kura na kuunga mkono hiyo itikadi.

Katiba inaweza kuweka mazingira ya haki, kama Ibara ya 176 tuliyoijadili, lakini haiwezi kulazimisha wananchi kuchagua itikadi badala ya utu wa kiongozi, kwa mantiki hilo lingekuwa jukumu la wananchi wenyewe kuchagua vitu vilivyokuwa vizuri.

Naomba niendelee kukusoma kwa makini kadri unavyoendelea kuchangia, kwa mantiki hoja zako zinaonyesha mtu aliyeifikiria sana nchi hii.

Ninakuomba tu, kwa heshima kubwa, uipe rasimu hii nafasi ya pili ukiwa na uelewa mpya kwamba si Serikali Tatu ni Serikali Moja isipokuwa kuna Muhimili Mpya wa Nne "Baraza la Usimamizi wa Taifa", ambalo ndilo Lenye Wawakilishi wa Pande zote za Muungano na Kazi Yao ni kuhakikisha Usawa kwenye jamhuri ya Muungano, (nikikazia hoja yangu hapa ni Hivi, Mihimili mitatu yaani Serikali, Bunge na Mahakama ni Mihimili ya pamoja inayosmamiwa na Muhimili wa Nne Baraza Hili kusiwepo na ubaguzi wa upande wowote wa Muungano).

Naombanimalize kwa kusema kwa mantiki naamini utaikuta ikijibu baadhi ya hofu zako, hata kama hautakubaliana na kila neno lake.

Rasimu kamili hipo kwenye tovuti ya www.katibampya.com
 
Nitakujibu baadae hoja hii lakini nikikuongoza moja kwa moja kwenye rasimu yetu ya katiba iliyopo kwenye tovuti ya www.katibampya.com hasa kwenye swala la Muundo wa polisi Tanzania. Ibara ya 213 na 187 zimeweka muungozo wa kujibu maswali yako kalibia yote uliyoouliza hapa. Na nitarudi na uchambuzi wa kina kabisa kwa kila swali lako.
 
Swali moja - Unaweza nambia kwa nini Kiutawala tunahitaji Vyama vingi vya Siasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…