Nimezisoma Ibara hizo mbili kwa haraka, binafsi naona kama Katiba Pendekezwa ina mambo mengi sana yakijirudia rudia kama sii MWONGOZO ulonyooka na rahisi mtu kuuelewa.
Ni hivi, mimi ningeshauri kuipa meno Tume ya Uchaguzi iwe Taasisi HURU yenye mamlaka ya juu kabisa na isofungamana na chama wala Utawala ili wahusike wao na chaguzi zote ndani ya Vyama vya Siasa.
Maadam Vyama.vyote vya Siasa vinataka Tume Huru, budi pia tume hiyo iwe na mamlaka ya Uangalizi wa Chaguzi zote za wagombea Udiwani, Ubunge na Uras toka chini huku chini ngazi ya Vyama, na baadae kusimamia Uchaguzi Mkuu badala ya kuunda muhimili mwingine wa Usimamizi.
Hii itawarahisisha kuwa na records zote za chaguzi nchini na hata mgombea akienda mahakamani wao watasimama kama mashahidi wa kile walichoshuhudia katika Uchaguzi hizo. Naamini mikono mingi katika Upishi huharibu mapishi.
Kitu pekee ambacho natamani kukiona ni kuwa na Vyama Vitatu au Vinne tu vya Siasa nchini badala ya Utitiri tulonao. Kwa kumuenzi Mwalimu, kwanza tuwe na Chama cha Ujamaa kutokana na historia yetu, ambacho kitalinda misingi tuloanza nayo hawa watakuwa Wahafidhina (as Conservative).
Halafu Vyama.vingine vitajipanga Kiitikadi dhidi ya Mrengo wa Ujamaa aidha kuwa Liberali ama Chama kinachokiwa kati Kushoto/Kulia n.k. Hapo tutakuwa wanaoamini katika Ubepari wa Kiafrika. Ndio upi? Watajipanga kwa Itikadi na sera zao.
Kwa wale sasa wanaotaka kujiunga na Siasa wajue wanasimamia nini (Mrengo) badala ta kufuata MTU. Ukiwa Mjamaa ndio imani yako.hata kama hukubaliani na Uongozi uliopo hakuna wakufukuzwa Uanachama ila.anaweza poteza nafasi ya mamlaka ndani ya Chama. Utamfukuzaje muumini ili aende wapi? Kuamini Siasa gani nyingine kama njia bora ya kuwapelekea Wananchi Maendeleo? Kama Mtu anaamini latika.Umamaa utamvuaje Imani hiyo kwa sababu amewakosoa viongozi? Hili ni kosa kubwa la Siasa zetu na tumelifumbia macho kwa muda mrefu sana. Turudi kwenye Uhalisia.
Tukiwa na Vyama vitatu au Vinne, Wagombea Urais waloshindwa Uchaguzi Mkuu wao wanaingia moja kwa moja Bungeni kama wawakilishi wananchi upande wa mrengo wao. Hii itaongeza chachu na umakini zaidi kwa Chama tawala kwa sababu Siasa zitahamia Bungeni badala ya majukwaa ya mikutano na Maandamano. Ndivyo wanavyofanya nchi za Magjaribi.
Swala la Maandamano yataruhusiwa tu kwa Wananchi wenyewe pamoja na Taasisi za Kijamii. Chimbuko la Mikutano ya hadhara na Maandamano kiasili ilikuwa na kusherehekea kama vile Yanga au Simba wanavyo andamana kwanUshindi na hupewa Ulinzi. Sii maandamano ambayo mali za watu ndio zinalindwa! Hizi ni vurugu (strike) na hatari kwa Usalama.wa.Wananchi.
Kisiasa maandamano ni migomo (strikes) ya Wananchi wenyewe kudai haki zao sii Vyama.vya Siasa. Iwe madai ya ongezeko la Mishahara, mazingira ya kazi, mashinikizo ya kudai haki ambazo hutokana na mikataba n.k. Hii habari ya Mikutano na maandamano ya Vyama vya Siasa tena baada ya Uchaguzi Mkuu ndio sababu kubwa ya vurugu zote zinazotokea nchini. Siamini katika.majukwa ya Mikutano ya Kisiasa.kama ni kutafuta Wanachama bali kujenga chuki za Kisiasa.
Niishie hapa kwa leo japo nina mengi sana kichwani ambayo nayaona hayaendi sawa kabisa. Tunatala kuiadhibu Katiba nzima ya mwaka 1977 kwa makosa yetu wenyewe.
Hata hizo Biblia na Kuruan kuna watu wanazikiuka, hivyo hatuwezi sema tuandike Biblia au Kuruan Mpya kwa sababu zimepitwa na wakati. Laa hasha sisi ndio wakosa tinahitaji kumrudia Mungu. Vivyo hivyo kwenye Katiba tunahitaji kujipima Uzalendo wetu sisi wenyewe. Katiba hii tunaibomonda na Tumeibagaza kama sii mwongozo bali kitabu cha Hadith.
Mkuu
Mkandara, ahsante kwa kuzipitia Ibara hizo na kwa uwazi wa maoni yako. Naomba nikubaliane na wewe kwenye mambo mawili ya msingi kabla sijaeleza kwa nini rasimu imesimama pale ilipo, kisha nijibu pendekezo lako la Tume moja yenye mamlaka yote, kwa mantiki hilo ndilo linalobeba uzito mkubwa zaidi wa kiuundo.
Kwanza, kuhusu urefu na marudio, uko sahihi kabisa. Rasimu hii ina Sura kumi na nne na Ibara mia tatu ishirini na moja, (14/321) na ni ndefu kwa kiwango ambacho hakiwezi kubishaniwa. Marudio unayoyaona si udanganyifu wa uandishi, ni matokeo ya uamuzi wa kimakusudi kwamba kila Ibara imeandikwa iwe na uwezo wa kusomeka na kueleweka bila kumlazimisha msomaji kurudi mara kwa mara kwenye Ibara nyingine ili kuipata maana kamili. Hii ni gharama ya urefu badala ya gharama ya utata. Nakubaliana na wewe kwamba hii inaifanya isiwe rahisi kusomwa mfululizo na mtu wa kawaida, na hilo ni jambo ambalo Muongozo na Uchambuzi tunaouandaa kwa lengo la kuisaidia jamii kuisoma sehemu kwa sehemu unajaribu kulishughulikia, ingawa sikatai kwamba rasimu kamili yenyewe inabaki nzito kwa msomaji wa mara ya kwanza, labda aisome zaidi ya mala moja Ndo utaiona Nyepesi Sana zaidi ya Kuisoma mala moja Tu.
Pili, kuhusu Ujamaa na idadi ya vyama, nako uko sahihi. Rasimu hii haijatamka Ujamaa wala itikadi nyingine yoyote kama msingi wa uchumi au siasa ya Taifa, wala haijaweka ukomo wa idadi ya vyama. Hili si pengo la bahati mbaya, ni uamuzi wa kifalsafa wa makusudi, na naomba nijitetee kwa uwazi kuhusu hilo. Ibara ya 104(6) inatamka waziwazi kwamba hakuna mtu anayeweza kulazimishwa kujiunga na chama fulani au itikadi fulani, wala chama hakiwezi kukataliwa kusajiliwa kwa kigezo cha itikadi yake, Hivyo Basi Kama rasimu ingeweka Ujamaa au itikadi nyingine yoyote kama msingi rasmi wa Taifa, au ingefunga idadi ya vyama view vitatu au vinne, Katiba yenyewe ingekuwa imeshachagua upande mmoja wa mjadala wa kiitikadi kabla mjadala huo haujaanza. Pia Wazo lako la chama cha Ujamaa chenye kumuenzi Mwalimu ni zuri na lina nafasi kamili ndani ya muundo huu, kwa mantiki hakuna kinachokizuia kuanzishwa na kushindana kihalali, Tofauti ni kwamba rasimu haitaki kukilazimisha wala kukikataza, inataka kubaki mahali ambapo kila itikadi, ikiwemo Ujamaa, inaweza kusimama sawa mbele ya wapiga kura.
(Kwa Nyoongeza yangu Rasimu hiyo kwenye Ibara ya 273(5)(a) na (b) Zimetamka Kuhusu Tunu ya Heshima na zimetamka Ofisi mbili za kuwaenzi waasisi wa Taifa, Yaani Karume na JK Nyerere, hii inaweza Kutoa Majibu ya Maswali yako Kuhusu kuwakumbuka waasisi wa Taifa Letu.)
Sasa naomba niende kwenye pendekezo lako zito zaidi, ambalo ni kuipa Tume Huru ya Uchaguzi mamlaka ya juu kabisa juu ya chaguzi zote, kuanzia za ndani ya vyama hadi Uchaguzi Mkuu, badala ya kuunda muhimili mpya wa usimamizi. Hoja yako ina mantiki ya vitendo, kwa mantiki chombo kimoja chenye kumbukumbu zote kingerahisisha ushahidi mahakamani. Lakini hapa ndipo naona hatari ya kimuundo ambayo naomba unipe nafasi ya kuieleza.
Ukiipa Tume moja mamlaka ya kusimamia uendeshaji wa kiufundi wa Uchaguzi Mkuu, wakati huohuo ikawa ndiyo inayosimamia demokrasia ya ndani ya vyama, na ikawa tena ndiyo yenye mamlaka ya juu kabisa isiyofungamana na chombo kingine chochote, umeweka mizigo mitatu tofauti kabisa kimaumbile juu ya bega moja.
1.
Usimamizi wa kiufundi wa upigaji kura ni taaluma ya uendeshaji na Utendaji wa Tume huru ya uchaguzi.
2.
Uamuzi wa haki kati ya mwanachama na Kamati Kuu ya chama ni taaluma ya kimahakama.
3.
Usimamizi wa Misingi ya Demokrasia ni swala la Baraza la Usimamizi wa Taifa. (Naomba nikufafanulie hapa, Baraza la Usimamizi wa Taifa Kazi yake ni Kusimamia Misingi yote ya taifa, Yaani Misingi yote inayolifanya Taifa liwepo, Hivyo Basi miongoni mwa
Misingi ya Demokrasia ni
Uchaguzi ulio Huru, kweli na Haki na hapa ndipo Baraza linaingia kutoa Tathimini yake, au muongozo lakini alijihusishi wala kuingilia Utendaji wa Kila siku wa
Tume. Pia naomba niendelee kufafanua kwamba
Baraza linasimamia Misingi ya Demokrasia sio Utendaji wa
Tume Huru ya Uchaguzi, lakini pia Haki ya mwanachama wa chama cha Siasa Husika inapatikana
Mahakamani hasa
Mahakama ya Katiba kama Rasimu yenyewe ilivyowekwa. Kwa kuongezea hapa ni kwamba "
Baraza hilo lina kazi zaidi ya moja na kusimamia misingi ya demokrasia ni sehemu ya kazi zake si
Kazi pekee iliyowekwa na katiba", )
NAOMBA KUENDELEA KIDOGO HAPA.
Ukiviunganisha vyote vitatu kwenye chombo kimoja, na kikaishiwa kufungamana na mtu yeyote, tatizo halipotei, linahama tu.
Embu jiulize What if.! Tume hiyo moja itatekwa siku moja, na Chama Fulani cha Siasa, kikundi cha Maslahi Binafsi au vyovyote, na hakuna mahali pa kukimbilia, kwa mantiki umeondoa uwiano wa kuangaliana uliokuwepo hapo awali.
Ndiyo maana rasimu imeamua kugawa mizigo hii mitatu kwa vyombo vitatu tofauti vinavyoangaliana.
1. Tume Huru ya Uchaguzi inabaki na jukumu lake la kiufundi la kuendesha Uchaguzi Mkuu.
2.
Mahakama ya Katiba, kupitia Ibara ya 176(2)(b)(II), inabaki na jukumu la kuamua haki kati ya mwanachama aliyepokonywa ushindi na Kamati Kuu ya chama chake.
3.
Baraza la usimamizi wa taifa kwa kupitia kwa Kamati ya Malezi ya Vyama vya Siasa, iliyoko ndani ya
Ofisi ya Haki, Miiko na Udhibiti wa Demokrasia chini ya
Baraza, inabaki na jukumu la kufuatilia afya ya kidemokrasia ya vyama kwa muda wote, si wakati wa uchaguzi pekee. Yaani Haki za kidemokrasia, maadili ya taifa, miiko na udhiti hili siasa isitumike kuathili usalama wa taifa au kuchota tamaduni za njee zisizo njema kwa taifa letu.
Kwenye Muundo Huu Kila chombo kina mamlaka finyu (Separation of power), lakini vyote vitatu vinasimama kwenye Mipaka yake na vinakuwa bora, hivyo Basi kutekwa kwa Chombo kimoja hakuvunji mfumo mzima, Bali itasaidia Kutambua Kwa Haraka shida hipo wapi.
Kuhusu mlinganisho wako wa mwisho, kati ya Katiba na vitabu vya dini, naomba nikupe mtazamo mwingine wa kuuangalia.
Vitabu vya dini vinaongoza dhamiri ya mtu binafsi, na uvunjaji wake huwa kati ya mtu na imani yake, Yaani Leo Mimi nikitenda dhambi ya uzinifu ni Mimi na Mungu wangu, na wala Jamii yangu haiwezi kuathilika na dhambi niliyofanya.
Lakini Katiba ina kazi tofauti kabisa, yaani Mwenye Madaraka anapokula Mali ya Umma unaoathilika ni Umma wote sio yeye Binafsi, au Mtu mmoja, hivyo Basi kazi ya Katiba si Tu Kutoa muongozo wa mambo mbali mbali ya Taifa lakini pia kwenye mada hii ni kumfunga mwenye madaraka hata pale asipokuwa na dhamiri njema.
NAOMBA NIKWAMBIA HAYA KWA UZITO MKUBWA KWAMBA.
Mfumo unaotegemea uzalendo wa watu peke yake, bila muundo wa kuwabana wale wenye tabia mbaya, ni bahati nasibu, si mpango wa kudumu.
Mimi Kwa Maoni yangu sikubaliani kwamba tatizo ni sisi wenyewe pekee bila muundo kuhusika, kwa mantiki hata watu wema wanahitaji mfumo unaowazuia Ili wabaki wema wakati wote, na ndipo thamani ya urefu wa Ibara hizi mia tatu ishirini na moja 321 inapoonekana, japo naelewa kabisa unavyoona uzito wake.
OMBI LANGU KWAKO MKUU NI HILI.
Binafsi nimeona wewe si tu msomaji wa kawaida wa Mada hii Bali Unatafuta kitu kilicho bora zaidi, Mimi sitaki kukuaminisha kwamba Rasimu hii ni Bora moja kwa moja Bali ninachoitaji ni kukuongoza sehemu za kusoma Hili kuamua kurudi hapa na kusema kwamba Rasimu hiyo ni Bora Basi usome Kwa Moyo Wako wote, si kukuaminisha kabra ujasoma wewe mwenyewe.
Kwanza kabisa na Kwa ukweli kwamba Rasimu hiyo ni ndefu Sana nakuomba nikupe muongozo wa wapi pa kuanza kusoma Hili Kuisoma mala moja Tu Uweze kuielewa Haraka zaidi.
Anza Ibara ya 286(1) Mwanzo kabisa kuna mambo yaliyowekwa Kuhusu Namna Katiba hiyo ilivyoandikwa, Yaani "Ibara, Ibara ndogo, Aya, kipengere na Aya ndogo. Pia kuna kitu kama vile
kikao cha Ufafanuzi maana yake ni nini...? Na kinakaa wapi.? kwenye Rasimu kinaonekana ndani ya maneno yaliyowekewa Kati Kati ya
[+......].
Kisha Ibara Hiyo hiyo, Yaani 286(2) kuna muongozo wa Katiba yote, Mipaka ya Jumla na Ufafanuzi wa Jumla wa Katiba.
All in all Ibara ya 286 ni Ibara ya Ufafanuzi wa Katiba yote, Yaani maneno yaliyotumika, na Nyoongeza nyingine kama vile bodi ya Kikatiba n.k
Ukishasoma Ibara Hizo pia soma Ibara ya 98 mbaka 116 Kuhusu Baraza la Usimamizi wa Taifa maana ndicho kitu kigeni zaidi kwenye Katiba hii na Kiukweli Ndio Muhimili wa Nne Wenyewe, hivyo umeelezewa kiundani kabisa kwenye Ibara Hizo Hapo Tajwa.
Baada ya hapo sasa kuanza Mwanzo Ibara ya 1 mbaka ya 321 unapata picha Kamili na kuelewa ubora wa Rasimu Hiyo ya Katiba.
Naomba niendelee kusema kwamba Rasimu hii ni ndefu hasa wingi wa Ibara zake lakini Naona ni muhimu kuwa Hivyo Kwa sababu pia Baraza Ndio Mamlaka ya Kimuungano Kati ya Tanganyika na Zanzibar hivyo Rasimu hiyo imetoa Majibu ya Maswali ya Muundo wa Muungano, Yaani Serikali Moja, mbili au Tatu. Yaani Rasimu hii imeweka Serikali Moja na kuongeza Muhimili wa Nne ambao Ndio unawakutanisha Tanganyika na Zanzibar kusimamia Misingi yote ya Taifa na hapo ndipo Mihimili mingine iliyobaki inakuwa Mihimili ya Jamhuri ya Muungano na Muungano Kati ya Pande Hizo mbili unapewa Mamlaka ya kusimamia Misingi yote.
Hivyo basi Rasimu hiyo ina mihimili minne ya kitaifa, yaani.
1.
Baraza l usimamizi wa Taifa.
2.
Serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania.
3.
Bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania.
4.
Mahakama ya jamhuri ya muungano wa tanzania.
Mihimili yote minne imetamkwa kwenye
SURA YA NNE ya Rasimu hiyo ya katiba kwa kuanzia na Baraza na kuendelea mihimili mingineyo.
Nilisema Misingi yote ya Taifa maana yake ni Misingi yote ya Demokrasia, Misingi ya Muungano wetu, Misingi ya Ukuu wa Katiba, Misingi ya utawala wa Sheria, Misingi ya Maendeleo na Mengineyo mengi, kwaiyo baraza la usimamizi wa misingi ya taifa kazi yake ni kuhakikisha misingi hiyo inaendelea kuwepo na isiweze kudhoofishwa kwa maslahi ya chama cha siasa, kikundi cha maslahi binafsi au mtu mmoja.
Rasimu Kamili ya Katiba Hipo kwenye Tovuti ya
www.katibampya.com